Tafuta

2021.10.17 Maaskofu wapya waliowekwa wakfu 2021.10.17 Maaskofu wapya waliowekwa wakfu 

Papa amewaweka wakfu Askofu Andrès Moreira na Askofu Marini

Papa Francisko amewawekwa wakfu Monsinyo Andrès Moreira kuwa Askofu na ambaye ni Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Wakleri na monsinyo Marini kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Tortona Italia.Katika mahubiri yake amewahimiza kuwa na ukaribu wa aina nne:kwa Mungu katika sala,Watu watakatifu wa Mungu,kwa maaskofu wenzao na mapadre.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameadhimisha misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Dominika tarehe 17 Oktoba 2021 na kuwaweka wakfu Monsinyo Andrés Gabriel Ferrada Moreira ambaye ni Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la  Wakleri  na Monsinyo Guido Marini  aliyekuwa mshereheshaji wa kipapa kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Tortona, Italia. Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake amekazia juu ya kutangaza Neno la Mungu kwa kila fursa, ili waowaonye, wakemee, washauri kwa moyo, wafundishe na kujifunza. Hawa watakuwa walinzi wa imani, huduma, upendo kwa Kanisa na kwa maana hiyo kuwa karibu sana na wafikiri kwamba ukaribu ndiyo njia kuu na asili ya  Mungu. Katika Kitabu cha Kutoka, Papa Francisko amesema kwamba Mungu mwenyewe alisema 'ni nani aliye karibu zaidi na watu wake kuliko yeye?' Kwa maana hiyo Ukaribu wa kiaskofu una sehemu mbili katika kuwasindikiza watu wa Mungu na ambao ni 'huruma na upole'.

Papa ameongoza misa na kuwaweka wakfu maaskofu wawili katika Kanisa kuu la Mt. Petro
Kuwekwa wakfu kwa maaskofu wawili katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.
Kuwekwa wakfu kwa maaskofu wawili katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Baba Mtakatifu amewaomba maaskofu wasiache kuwa na ukaribu huo  daima kwa Mungu katika sala,  kwa watu, kwa maaskofu na mapadre. Hizo ndizo njia nje nne za ukaribu wa kiaskofu yaani: “kukaribia watu wa Mungu, kumkaribia Mungu, kuwakaribiana maaskofu wenzao na kuwakaribia mapadre”. Papa Francisko amefafanua kuwa Askofu ni mtu wa ukaribu na Mungu katika sala. Lakini mara nyingi mwingine anaweza kusema kuwa ana mambo mengi ya kufanya na hivyo hawezi kusali. Mitume walipoanzisha huduma ya ushamasi, Papa ameongeza kusema, Petro alisema: “sisi maaskofu tunapaswa kusali na kutangaza Neno. Kwa maana hiyo “kazi ya kwanza ya kiaskofu ni kusali na siyo kusali kama kasuku, hapana ni kusali kwa moyo. Hakuna cha kusema kwamba hana muda”. Papa amewaomba kutoa mambo mengineyo, lakini cha kwanza kama askofu ni kusali. Papa akifafanua juu ya ukaribu wa askofu wa kukaribiana na maaskofu wengine, amebainisha kwamba  "si wale ambao wanafanya vyama, kwa kuchagua hiki na kile". Wao ni maskofu, watakuwa na mjadala kati yao lakini ni kama ndugu na ukaribu.

Kuwekwa wakfu kwa maaskofu wawili katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.
Kuwekwa wakfu kwa maaskofu wawili katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Papa akiendelea na msisitizo ametoa onyo kwamba kusengenyana kama maaskofu kamwe isitokee,  bali uwepo ukaribu kwa maaskofu na kiungo cha maaskofu wengine. Papa amehimiza wasisahau kuwa mapadre wao wako karibu sana. “Lakini je ni mara ngapi yanasikika malalamiko ambayo mapadre wanasema. “mimi nilimwita Askofu, lakini katibu wake akaniambia kuwa ajenda yake imejaa na labda ndani ya siku 30 anaweza kunipokea” …. Papa ameongeza kusema: “hii siyo sawa”. Ikiwa askofu anapata habari kuwa padre mmoja amemwita, lazima siku hiyo hiyo au siku nyingine askofu mtafute padre wake.  Kwa kufanya hiyo Padre huyo atajua jinsi alivyo na baba. Ukaribu wa mapadre ndiyo aina ya tatu wa kiaskofu ambayo Papa Francisko ameifafanua kwa kusisitiza kwamba ikiwa mapadre hawendi kwa maaskofu, basi askofu anapaswa kwenda yeye mwenyewe kuwatembelea kwa ajili ya ukaribu huo.

Kuwekwa wakfu kwa maaskofu wawili katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.
Kuwekwa wakfu kwa maaskofu wawili katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Ukaribu wa nne wa kiaskofu ni ule wa kukaribia watu watakatifu wa Mungu. Kile ambacho Paulo alisema kwa Timoteo kwamba:“ kumbuka mama yako, bibi yako…” ni swa na kusema kwamba wao wasisahau kuwa wao wamechaguliwa kutoka ndani ya zizi, na si kwa kwa sababu ya kisomo  ambacho walijikita nacho,au  sifa nyingi ambazo zimewafanya wawe Askofu. Hapana, bali ni kutoka katika zizi. Kwa njia hiyo maaskofu hao wasisahau ukaribu huo wa wa kukaribia watu wa Mungu. Na Bwana wasaide kukua katika njia hiyo ya ukaribu na kwa kufanya hivyo  wataweza kuiga vema Bwana, kwa sabababu Yeye daima yuko karibu na daima atakuwa karibu nasi na kwa ukaribu wake ambao ni ukaribu wa huruma na upole unaotufanya kwenda mbele. Na  Mama Maria awalinde! amehitimisha Papa.

Kuwekwa wakfu kwa maaskofu wawili katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.
Kuwekwa wakfu kwa maaskofu wawili katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Itakumbukwa hivi karibuni, Papa Francisko alimteua Monsinyo Andrés Gabriel Ferrada Moreira kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Wakleri na hivyo kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu, uteuzi ambao ulianza rasmi tarehe 1 Oktoba 2021. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mteule Andrés Gabriel Ferrada Moreira alikuwa ni Afisa mwandamizi kwenye Baraza la Kipapa kwa ajili ya Wakleri.Askofu mkuu mteule Andrés Gabriel Ferrada Moreira alizaliwa huko Santiago de Chile tarehe 10 Juni 1969. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 3 Julai 1999 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre, Jimbo kuu la Santiago de Chile. Baadaye alijiendeleza kwa masomo ya juu na hatimaye, mwaka 2006 akatunukiwa Sahada ya Uzamivu katika Taalimungu kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian. Kabla ya kuitwa kutekeleza dhamana na utume wake mjini Vatican kunako mwaka 2018, aliwahi kushika nafasi mbalimbali za utume Jimbo kuu la Santiago de Chile. Aliwahi kuwa Mwadili mkuu wa wanafunzi na mkuu wa kitivo cha Taalimungu Seminari kuu ya Kipapa ya Malaika Walinzi, Jimbo kuu la Santiago de Chile: “Seminario Pontificio Mayor de los Santos Ángeles Custodios, Santiago de Chile.”

Askofu Mkuu Ferrada Moreira
Askofu Mkuu Ferrada Moreira

Vile vile mnano tarehe 29 Agosti 2021, Papa  Francisko  alimteuwa Monsinyo Guido Marini (56) kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Tortona, nchini Italia. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule Guido Marini alikuwa ni Mshereheshaji mkuu wa Ibada za Kipapa mjini Vatican. Askofu mteule Guido Marini alizaliwa tarehe 31 Januari 1965 huko Genoa, Kaskazini mwa Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 4 Februari 1989 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre na Kardinali Giovanni Canestri. Baadaye alijiendeleza kwa masomo ya juu katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Lateran na kujipatia Shahada ya Uzamivu Kuhusu Sheria za Kanisa na Taratibu za Uendeshaji wa Kesi Mahakamani. Na mwaka 2007 alijipatia Shahada ya Uzamivu katika Saikolojia ya Mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Salesianum.

Maaskofu wapya wakitoa shukrani kwa Baba Mtakatifu
Maaskofu wapya wakitoa shukrani kwa Baba Mtakatifu
MAHUBIRI YA PAPA KWA KUWEKA WAKFU
17 October 2021, 11:04