Tafuta

Papa amewatia moyo watoto milioni moja kwa ajili ya kusali Rozari

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana amekumbusha juu ya Kampeni ya Watoto milioni 1 kusali Rosari iliyoandaliwa na Chama cha Kipapa cha Kanisa Hitaji kwa kuhamasisha taasisi za kielimu,familia na parokia zote kusali kwa ajili ya umoja na amani:amekumbuka wenyeheri wapya huko Hispania.Amewaombea waathirika wa mashambulizi ya kigaidi huko Norway,Afghanistan, na Uingereza.Papa amekumbuka hija ya kiekumene kutoka Poland kwenda mkutano wa Cop26.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu mara baada ya sala ya malaiaka wa Bwana amekumbusha juu ya  Kampeni ya watoto milioni moja kusali Rosari iliyoandaliwa na  Chama cha Kipapa cha Kanisa   hitaji kwa kuhamasisha taasisi za kielimu, familia  na parokia zote kusali kwa ajili ya  umoja na amani. Amewatia moyo katika kampeni hiyo ambayo kwa mwaka huu inaongozwa kwa namna ya pekee kwa  Maombezi ya Mtakatifu Yosefu katika fursa ya maadhimisho ya miaka 150 tangu kutangaza kuwa msimamizi wa Kanisa la Ulimwengu. Amewashukuru watoto wote kwa ushiriki wao.

Papa Francisko Aidha amekumbusha kuwa huko Cordova nchini Hispania Jumamosi tarehe 16 Oktoba wametangazwa wenyeheri wapya Padre, Juan Elías Medina  wa wenzake  126 wafiadini, mapadre, watawa, waseminari na walei, ambao waliuawa kwa kutetea imani yao wakati wa mateso ya kidini kwenye miaka ya 30 nchini Hispania. Imani yao iweze kuwa nguvu kwa wote hasa wakristo wanaoteseka katika sehemu mbali mbali za dunia, nguvu ya kushuhudia kwa ujasiri wa Injili. Ameomba wapigiwe makofi…

Wiki iliyopita, yametokeo matukio tofauti ya mashambulizi ya kigaidi  kwa mfano huko Norway, Afghanistan, Uingereza na kusababisha idadi kubwa ya vifo na majeruhi. Baba Mtakatifu ameelezea ukaribu wake kwa familia za waathiriwa wote. Ameomba waachilie mbali na njia hizi za vurugu ambazo daima ni upotofu wa kushindwa kwa wote. Kwa kukumbusha kwamba vurugu daima zinazalisha vurugu.

Papa Frabcisko amewasalimia na kuwabariki wanahija ya kiekumeni na kwa ajili ya haki ya ikoloja,walioundwa  na wakristo wa madhehebu mbali mbali ambao wameondoka kutoka Poland kuelekea Scotland katika fursa ya mkutano mkuu kuhusu tabianchi wa Cop26 unaokaribia. Na kwa wote amewatakia dominika njema na wasisahau kusali kwa ajili yake.

Umati wa wanahijia na waamini wakisali sala ya malaika wa Bwana na Papa
Umati wa wanahijia na waamini wakisali sala ya malaika wa Bwana na Papa
17 October 2021, 13:24