Tafuta

Upole wa Papa na huruma. Upole wa Papa na huruma. 

Papa akutana na wafungwa katika nyumba ya Mtakatifu Marta

Ijumaa 22 Oktoba 2021,Papa Francisko alikutana katika nyumba ya Mtakatifu Marta Vatican na kundi la wafungwa,walioishi uzoefu wa magereza.Amewatakia mwanzo mzuri wa kuzaliwa upya hata wa kujikomboa hasa hata masaada kwa watu wengine waweze kufanya safari hiyo.Aliyewasaidia ni Padre Benito Gioretta ambaye aliwasikiliza kwa makini na kushirikishana nao maisha yao magumu.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko anayesikiliza na kusindikiza kwa tabasamu na maneno ambayo yasikika yenye huruma ya Mungu kwa ajili ya msaada wa wengine ili wasihukumu makosa yaliyotendekea. Ni uzoefu wa wale ambao walikutana katika nyumba ya Mtakatifu Marta, Vatican, wafungwa ambao walikwisha maliza kifungo au wale ambao bado wanaendelea na adhabu ndani ya miundo ya nyumba za Jumuiya ya Don Benzi huko Vasto Italia, katika Wilaya ya Chieti na Termoli karibu na Campobasso Italia. Papa Francisko alichagua kuwasikiliza sauti zao na kushukuru ushuhuda wao walioutoa na ambao mara nyingi ni mgumu sana. Amekumbusha video moja aliyokuwa anawelea wafungwa ambao hawakuwapo ambao alikuwa anawauliza kama ni muhimu kutembea peke yao au kuomba msaada, kwa kubisha hodi mlango kwa maana ikiwa unaishi lakini hujui mahali pa kwenda. “Bwana ndiye anatoa fursa na atakufanya upige hatua”.

Jambo muhimu katika maisha ni kutembea, ni kuwa katika njia, Papa amebainisha. Na kongeza kusema kwamba “kuna ambaye haoni mwelekeo na wala njia, kuna watu wengi wameegeshwa wa kusaidiwa, kuna moyo uliogeshwa na ambao unaingia katika wasiwasi na kukufanya uanze kuondoka. Tunazunguka lakini tunakuwa katika njia hisio na mlango wa kutokea, hatupati mlango, katika njia hiyo ndiyo tunatembe na kuzungukia ndani mwake bila kutoka nje”. Sisi sote tunakosea katika maisha, lakini jambo la muhimu ni kutobaki katika makosa, Papa amesema na kunukuu wimbo wapanda milima unaoalika kutobaki ardhini hasa unapoanguka.

“Kuamka hata kwa sababu shukrani kwa neema ya yule ambaye anafanya kuamka bila kuhukumu aliyeanguka kwa sababu anastahili. Mara nyingi katika maisha tunakutana msaaada wa wale ambao wanataka kutusaidia na hivyo hata sisi lazima kufanya hivyo kwa wengine. Kwa uzoefu tulio nao basi tuwafanyie wengine”. Kabla ya kuwaaga, awaliwaomba waweke matunda ya kile ambacho waliishi ili kuweza kuzalisha wema wa kweli “ ni matashi yangu kuwa uzoefu uwe na matunda na uwe kama mbeu ambayo ikipandwa, inakua …Iwe kama ugonjwa mwema, ambao unaambukiza, Uzoefu wa kuambukiza. Uwe wa ukombozi , ambao unafungya milangi kwa ajili ya watu wengi wenye kuhitaji kuishi uzoefu ambao wao wameuishi.

Aliyesindikiza kikundi hicho ni Padre Benito Giorgetta, Paroko wa Kanisa la Mtakatifu Timoteo huko Termoli, ambaye mara baada ya mkutano huo ameelezea hisia nzuri sana iliyokuwapo katika nyumba ya Mtakatifu Marta na sahii katika kitabu cha Sandra Sabattini katika mkesha wa Kutangazwa kwake mwenyeheri. Hii ni safari ambayo imezaliwa katika moyo wa Papa ambaye kama inavyojulikana, yuko makini sana na ukaribu kwa walio dhaifu, watu duni kwa namna ya pekee wafungwa magerezani. Inatosha kufikiria alivyochagua jiji la Roma wakati wa Siku ya Karamu kuu akawaosha miguu wafungwa katika Gereza la Casal del Marmo gereza ambalo ni  la vijana. Kwa maana hiyo Padre Benito ametumia fursa hiyo kumwomba Papa awapokee hatimaye wafungwa hawa na ndoto hiyo ilikamilika.

23 October 2021, 17:16