Viongozi wakuu wa Vatican Jumatatu tarehe 13 Septemba 2021 wamekutana na kuzungumza na viongozi wa Serikali ya Slovakia. Viongozi wakuu wa Vatican Jumatatu tarehe 13 Septemba 2021 wamekutana na kuzungumza na viongozi wa Serikali ya Slovakia.  

Viongozi Wakuu wa Slovakia Wakutana na Papa Francisko!

Baba Mtakatifu, Jumatatu tarehe 13 Septemba 2021 majira ya jioni, alikutana na kuzungumza kwa faragha na Bwana Boris Kollár, Rais wa Bunge la Slovakia pamoja na Bwana Eduard Heger, Waziri mkuu wa Slovakia waliokuwa wameandamana na familia zao. Viongozi hawa walipata nafasi ya kuzungumza pia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican na ujumbe wake mzito!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. –Vatican.

Hija ya Kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Slovakia kuanzia tarehe 12 hadi tarehe 15 Septemba 2021 inanogeshwa na kauli mbiu “Pamoja na Bikira Maria na Mtakatifu Yosefu Njia ya Kwenda kwa Yesu”. Baba Mtakatifu, Jumatatu tarehe 13 Septemba 2021 majira ya jioni, alikutana na kuzungumza kwa faragha na Bwana Boris Kollár, Rais wa Bunge la Slovakia pamoja na Bwana Eduard Heger, Waziri mkuu wa Slovakia waliokuwa wameandamana na familia zao.

Viongozi hawa wa kitaifa walipata pia nafasi ya kukutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican akiwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican pamoja na Askofu mkuu Edgar Peña Parra, Katibu mkuu Msaidizi wa Vatican. Mazungumzo kati ya viongozi hawa yamedumu kwa takribani dakika 45 na wamejadili tema mbalimbali kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu ndani na nje ya Slovakia.

Parolin Viongozi
14 September 2021, 12:32