Papa:Mapinduzi ya usawa kijamii yanaanzia ndani ya Kristo

Papa Fancisko akiwa katika ukumbi wa Papa Paulo VI,jijini Vatican ameendeleza katekesi yake ambayo amewaalika wakristo kuwa na umoja na siyo kuunda utengano na sitofahamu za kijamii kati ya jinsia mbili.Papa amekumbusha hata utumwa mpya mamboleo na jinsi ambavyo wanawake wana fursa zinazofanana na wanaume.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Papa Francisko Jumatano tarehe 8 Septemba 2021 ameendelea kama kawaida na Katekesi yake kwa waamini na mahujaji wote katika ukumbi wa Paulo VI, jijini Vatican. Kwa kuongozwa na Waraka wa Mtakatifu Paulo kwa Wagalatia. Akianza tafakari hiyo Papa amesema “Tuendelee na safari yetu ya tafakari ya imani katika mwanga wa Barua ya Mtakatifu Paulo kwa Wagalatia. Mtume anasisitiza kwa wakristo hao ili wasisasahu mapya ya maonesho ya Mungu ambaye walitangaziwa. Kwa kukubaliana kabisa na mwinjili Yohane (Yh 3,1-2), Paulo anasisitiza kuwa imani katika Yesu Kristo imeruhusu kugeuka kiukweli wana wa Mungu na warithi wake. Sisi mara nyingi hatutambui sana hali halisi ya kuwa wana wa Mungu. Ni vizuri kufanya kumbu kumbu daima ya shukrani kwa wakati ambao tumepata  ubatizo wetu ili kuishi kwa utambuzi wa zawadi kubwa tuliyoipokea.

“Ikiwa mimi leo nitauliza, ni nani kati yenu anayejua tarehe ya ubatizo wake? Ninafikiri wa kuamsha mikono wanaweza kuwa wachache… Na kinyume chake ni tarehe ambayo sisi tulikombolewa, ni tarehe ambayo sisi sote tumegeuka kuwa wana wa Mungu.  Na sasa ambao hawajuhi siku hiyo basi wawaombe wasimamizi wa ubatizo, baba na mama wazazi, wajomba na shangazi kwamba: mimi nilibatizwa lini? Ni vema kuikumbuka kila mwaka tarehe hiyo; ni tarehe ambayo tulifanywa kuwa wana wa Mungu. Papa ameongeza kuuliza “ni sawa? Mtafanya hivyo? (Wamejibu ndiyo) Papa akasema ni jibu la hivi hizi … lakini basi tuendelee mbele….

Papa akiendelea amesema kuwa kwa hakika mara tu unapofikia imani katika Yesu Kristo, ambayo ni ya kina inakufanya kuwa mwana wa Mungu. Kuwa mwana anayozungumzia Paulo si ile ya ujumla ambayo unawahusisha wanaume na wanawake, bali ni ya kuwa kama watoto Mungu mmoja. Katika somo ambalo limesikika yeye anathibitisha wazi kwamba: kwa njia ya imani inaruhusu kuwa wana wa Mungu katika Kristo (Waga 3,26). Hili ndilo jambo jipya. Ni hiyo ya kuwa katika Kristo ambayo inafanya utofauti. “Si wana wa Mungu tu, bali wote kwa maana ya  wanaume na wanawake wote ni wana wa Mungu, kila dini yoyote tuliyo nayo”, Papa ameongeza. Lakini yote hayo ni katika Kristo ambayo inaleta utofati kati ya wakristo na hiyo inakuja peke yake kwa ushiriki katika ukombozi wa Kristo na ndani yetu katika Sakramentii ya ubatizo, Papa amefafanua. Kwa kufanyika mwili Yeye amekuwa kaka yetu, na kwa kifo chake na ufufuko ametupatanisha na Baba. Maana anayempokea katika imani kwa ubatizo katika Kristo anamvaa Yeye na katika hadhi ya kuwa mwana, haya ya 27, inasema.

Mtakatifu Paulo katika barua zake anarejea mara nyingi ubatizo. Kwake yeye, tendo la  kuwa mbatizwa ndilo  sehemu halisi ya fumbo la Yesu.  Kwa mfano katika barua yake kwa Warumi atafikia kusema kuwa katika ubatizo sisi tumekufa na Kristo na kuzikwa na Yeye ili kuweza kuishi na Yeye (Rm 6,3-14). Kufa na Kristo kuzikwa na Yeye ili kuweza kuishi na Yeye. Na hii ni neema ya ubatizo yaani kwa kushiriki kifo na ufufuko wa Yesu.  Katika ubatizo kwa maana hiyo sio jambo la ibada ya nje. Kwa wale wanaopokea ubatizo wanabadilishwa kwa ndani  na wanakuwa na maisha mapya, kwa hakika yeyote  anayeruhusu kumgeukia Mungu na kumwomba kwa jina la Aba yaani baba (rej. Gal 4,6). Mtume anathibitisha kwa shauku kubwa kuwa kile alichopokea kwa ubatizo ni utambulisho wote  mpya  ambao unastahili heshima zaidi ya tofauti ambazo zipo katika mpango wa dini za kikabila.

Paulo anaeleza:“Hapana Myahudi wala Myunani; na hata yule wa kijamii: Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke (Gal 3,28). Mara nyingi vielelezo hivi vinasomwa kwa haraka, bila kuelewa thamani ya mapinduzi yaliyomo  ndani mwake. Kwa upande wa Paulo anawaandikia Wagalatia  kwamba katika Kristo hakuna Mhahudi wala Myunani , ambayo ni sawa na utambulisho wa kupinda katika muktadha wa kabila la kidini wa wakati ule. Kwanu Myahudi kwa dhati alikuwa  katika nafasi ya watu waliochaguliwa, na alikuwa na fursa zaidi ya mpagani ( Rm 2,17-20) , kama asemavyo katika Barua kwa Warumi sura ya pili haya ya 20 na Paulo mwenyewe anasisitiza hilo (Rm 9,4-5). Hata leo hii yanatokea, watu wengi ulimwenguni, mamilioni hawana haki ya kula, hawana haki ya elimu, hawana haki ya ajira. Ni utumwa mpya, ni wale ambao wanaishi pembezoni, na ambao wananyonywa na wote. Hata leo hii kuna utumwa, tufikirie kidogo hilo. Sisi tunakataa hadhi ya watu wa kibinadamu. Lakini kuna watumwa Papa amesisitiza.

 

08 September 2021, 17:00