2021.09.11 Papa amekutana na Wakalmeli Vaatican katika mchakato wa Mkutano wao mkuu. 2021.09.11 Papa amekutana na Wakalmeli Vaatican katika mchakato wa Mkutano wao mkuu.  

Papa kwa Wakarmeli:tunzeni moto wa urafiki na Mungu

Papa Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Ndugu Wakarmeli:Ushauri wa Papa anawaomba wasimike mizizi ya uhusiano wao na Mungu,Utatu wa upendo na wameitwa kukuza uhusiano katika Roho katika mvutano mzuri kati ya kuwa peke yako na kuwa na wengine.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kusikiliza, kutambua, na kuwa mashahuda. Ndiyo mambo makuu yaliyosikika katika hotuba iliyotolewa na Baba Mtakatifu Francisko kwa washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Wakarmeli peku. Kusikiza ni mtazamo kimsingi wa mwanafunzi, wa mtu ambaye anajiweka katika shule ya Yesu na anataka kujibu kile anachoomba katika wakati huu mgumu lakini mzuri kila wakati, kwa sababu ni wakati wa Mungu, amesema hayp Papa Francisko. Kwa wakati huu, ambapo janga hili limetuweka sisi wote mbele ya maswali mengi na ambayo imeona kuanguka kwa dhamana nyingi, amesema watawa hao wanaiitwa, kama watoto wa Mtakatifu Teresa, kutunza kwa uaminifu wao vitu vya kudumu vya karama zao. Ikiwa mgogoro huu una kitu kizuri na hakika kipo ni hasa kuturudisha kwa vile vitu muhimu, sio kuishi tukiwa tumevurugwa na uhakika wa uwongo.

Makofi kwa Wakarmeli
Makofi kwa Wakarmeli

Papa kwa maama hiyo amesisitiza kwamba wakati mwingine mtu hujiuliza ni nini mustakabali wa maisha ya wakfu. Hayo ni maono ya kukata tamaa ambayo yamekusudiwa na yanayopaswa kukataliwa kama yale ya kuhusu Kanisa lenyewe: Maisha yaliyowekwa wakfu ni sehemu ya Kanisa kama vile Yesu alivyokusudia na kama Roho anavyozidi kila wakati kuzaa.  Kwa maana hiyo kila jaribu la kuwa na wasiwasi juu ya kuishi, lazima ziondolewe, kinyume chake ni kuishi kwa ukamilifu, kukubali neema ya sasa, hata na hatari zinazojumuisha, Maisha ya Wakarmeli, Papa Francisko amewakumbusha, kuwa ni maisha ya kutafakari. Hii ndio zawadi ambayo Roho ametoa kwa Kanisa na Mtakatifu Teresa wa Yesu na Mtakatifu Yohane wa Msalaba, na baadaye na watakatifu wa Wakarmeli. Kwa uaminifu wa zawadi hii, Papa anaongeza, “Maisha ya Wakarmeli ni jibu kwa kiu cha mwanadamu wa siku hizi, ambaye ana kiu kubwa kwa Mungu, kiu cha umilele. Na inalindwa kutokana na saikolojia, kiroho, au kutoka kwa visasisho vya uwongo ambavyo huficha roho ya ulimwengu”.

Picha ya pamoja ya Wakarmeli
Picha ya pamoja ya Wakarmeli

Papa amekitaja kitabu cha Padri de Lubac juu ya ulimwengu wa kiroho ambacho kinasema kwamba “maovu mabaya zaidi ambayo yanaweza kutokea kwa Kanisa, kuliko wakati ule ni roho ya ulimwengu”. Ulimwengu wa kiroho ni utamaduni wa muda mfupi na wa kuonekana juu juu Papa, Francisko amesema, ambao ni hila kubwa inaingia na hatuoni. Papa ameongeza kusema “mnajua vizuri jaribu la kisaikolojia, kiroho na sasisho za ulimwengu: roho ya ulimwengu. Na juu ya hili ninawaomba tafadhali: jihadharini na ulimwengu wa kiroho, ambao ndio uovu mbaya zaidi ambao unaweza kutokea kwa Kanisa”. Uaminifu wa Kiinjili, sio utulivu wa mahali, lakini ni utulivu wa moyo; ambao haujuhi kukataa mabadiliko, lakini katika kufanya mabadiliko muhimu ili kukidhi kile ambachp Bwana anatuomba, hapa na sasa. Na kwa hivyo uaminifu unahitaji kujitolea thabiti kwa maadili ya Injili na karama ya mtu mwenyewe na kukataa kile kinachotuzuia kutoa kikamilifu  kwa Bwana na kwa wengine. Papa pia  amekumbusha kwamba furaha na ucheshi lazima ziwe sifa tofauti za maisha ya kitawa. Na amewatia moyo Wakarmeli kuweka urafiki na Mungu, maisha ya kidugu katika jumuiya na utume wao.

Papa akisalimiana na Mkuu wa Shirika la Wakarmeli
Papa akisalimiana na Mkuu wa Shirika la Wakarmeli

Papa Francisko amewawasihi, akianzia na urafiki na Mungu na mtindo wa udugu kwa kufikiria tena utume, ubunifu na msukumo wa kitume wa kufanya uamuzi, ukizingatia ulimwengu wa leo. Urafiki na Mungu hukomaa katika ukimya, katika kumbukumbu, na katika kusikiliza Neno la Mungu. Hata hivyo amesema urafiki ni kama moto ambao lazima utunzwe na kulindwa. Joto la moto huo wa ndani pia husaidia kufanya mazoezi ya maisha ya kidugu katika jumuiya. Sio la kipengee la kuongeza, lakini ni kubwa sana na muhimu. “ninyi mnakumbuka vema majina yenye wenyewe: “ Ndugu peku”. Mliosimimia mizizi katika uhusiano na Mungu, Utatu wa Upendo, na ambapo mnaitwa kukuza uhusiano katika Roho, katika mvutano mzuri kati ya kuwa peke yako na kuwa na wengine, kinyume na kuwa na ubinafsi na usanifishaji wa ulimwengu” , Papa amebainisha.

Mkutano Mkuu wa Wakarmeli ambao umefanyika  Roma tangu tarehe  30 Agosti hadi 14 Septemba ni wa 92 katika historia ya Shirika hilo. Kazi ya mkutano huo inajikia na kufanyia kazi ya kusasisha  maandishi yaliyoundwa katika miaka sita iliyopita na imejikita katika karama ya Wakarmeli na Wateresia. Miongoni mwa madhumuni, yake ni yale ya kujibu kwa njia iliyosasishwa maswali: inamaanisha nini ya kuwa Wakarmeli leo hii? Jinsi gani ya kuishi wito huo ili kuendana na changamoto za sasa? Washirika 95 wa Wakarmeli kutoka mabara 5 wameitwa kwenye Sura hiyo, wakiwakilisha takriban Ndugu 4,000 wa Shirika hili. Mnamo tarehe 4 Septemba mkutano Mkuu ulimchagua Padri Miguel Marquez Calle, aliyezaliwa tarehe 5 Oktoba 1965 nchini Uhispania, kama mkuu mpya wa Shirika.

11 September 2021, 14:40