Viongozi watatu wa kikristo wanatoa wito kwa kila mtu,kwa kila imani au mtazamo wao wa ulimwengu,ajitahidi kusikiliza kilio cha dunia na cha watu maskini. Viongozi watatu wa kikristo wanatoa wito kwa kila mtu,kwa kila imani au mtazamo wao wa ulimwengu,ajitahidi kusikiliza kilio cha dunia na cha watu maskini. 

Papa,Bartholomew,Welby:kila mtu asikilize kilio cha dunia na maskini

Papa Francisko,Patriaki wa kiekumene Bartholomew na Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby kwa pamoja wameandika ujumbe wao wito wa dharura kwa ajili ya wakati ujao wa sayari.Ujumbe hunabeba wito kwa ajili ya COP26,jukumu la kila mmoja kutoa sadaka kwa ajili ya sayari na wito kwa viongozi wenye madaraka kutafuta faida ya watu ili kuongoza mpito katika uchumi wa haki na endelevu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kwa mara ya kwanza, viongozi Katoliki, WakioRthodox na Kanisa la kianglikani kwa pamoja wameandika ujumbe wao wakiangazia hatari ya dharura ya kutunza mazingira katika muktadha wa umaskini na umuhimu wa ushirikiano ulimwenguni.  Ni katika fursa ya kipindi hiki cha kuombea Kazi ya uumbaji kilicho anza tangu tarehe Mosi Septemba na kitahitimishwa tarehe 4 Oktoba sambamba na siku kuu ya Mtakatifu Francis wa Asisi. Viongozi wa kidini ni Papa Francisko, Patriaki wa kiekumene Bartholomew na Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby wanashauri kila mmoja kuchukua nafasi yake ili kuchagua kwa dhati maisha kwa ajili ya wakati ujao wa sayari hii.

Wito wa kuombea mkutano wa viongozi wa COP26 na kuombea kazi ya uumbaji

Katika Hati yao ya pamoja, viongozi hawa wa kikristo wamewaalika watu kusali, katika kipindi hiki cha kuombea kazi ya uumbaji, na kwa ajili ya mkutano ujao wa viongozi wa COP26 unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba wa kutafuta suluhisho la masuala ya mabadiliko ya tabianchi. Katika ujumbe wao  viongzoi hawa wanasema kuwa: “Tunatoa wito kwa kila mtu, kwa kila imani yake au mtazamo wao wa ulimwengu, ajitahidi kusikiliza kilio cha dunia na cha watu ambao ni maskini, akichunguza tabia zao na kuahidi kutoa sadaka za maana kwa ajili ya dunia ambayo Mungu ametupatia”.  Hata hivyo katika azimio la pamoja linatoa onyo wazi kwamba: “Leo, tunalipa bei ... Kesho inaweza kuwa mbaya” na hivyo huu ni wakati muhimu, kwani ni kwa ajili ya watoto wetu na siku zijazo za nyumba yetu ya pamoja ambayo hutegemea.

Dhuluma na ukosefu wa usawa,uharibifu wa mazingira

Viongozi watatu wa Kikristo wamezungumzia pia dhidi ya dhuluma na ukosefu wa usawa, wanasema: “Tunasimama mbele ya haki: upotezaji wa bioanuai, uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi ni matokeo yasiyoweza kuepukika ya matendo yetu, kwani tumetumia rasilimali dunia kwa pupa kuliko sayari inavyoweza kuvumilia. Lakini pia tunakabiliwa na udhalimu mkubwa kwa sababu watu wanaobeba matokeo mabaya zaidi ya dhuluma hizi ni maskini zaidi katika sayari na wa wamechukua jukumu ambalo hawakulisababisha au kidogo”.  Kwa maana hiyo katika ujumbe wao wa pamoja unawaalika watu kwa mambo muhimu: kusali kwa ajili ya mkutano wa viongozi wa COP26; kila mmoja kutoa sadaka ya maana kwa ajili ya sayari, kufanya kazi pamoja na kuchukua jukumu la jinsi tunavyotumia rasilimali zetu, na kwa wale walio na majukumu makubwa waweze kuchagua faida inayozingatia watu na kuongoza mpito kwa uchumi wa haki na endelevu.

07 September 2021, 15:48