Papa amekutana na Rais wa Chile:Mazungumzo kwa ajili ya wema wa nchi
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Alhamisi tarehe 9 Septemba 2021, Papa Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya Chile, Bwana Sebastián Piñera Echenique, jijini Vatican, ambaye mara baada ya mkutano huo amekutana pia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican kwa ajili ya Mahusiano na ushirikiano na Nchi.
Katika mazungumzo yao, yameonesha kuwa na uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizi mbili, pamoja na jitihada za pamoja kwa ajili ya amani, haki kijamii, ulinzi wa maskini, wahamiaji na watu walio katika mazingira magumu. Wakiendelea na mazungumzo hayo, wametazama hali halisi ya masuala ya ndani ya Nchi huku wakitoa umakini kwa namna ya pakee ya maendeleo, kijamii na kiuchumi, mchakato wa mageuzi ya Katiba na uhusiano na Kanisa katoliki.
Kwa mtazamo huo wa sjitahada za Kanisa, ni matarajio ya vionozi hao kuwepo ushirikiano wa utulivu kwa kuzingatia mchango unaotolewa na Kanisa katoliki kwa ajili ya wema wa watu katika muktadha wa upendo, elimu na maisha ya kijamii hasa katika kipindi hiki kigumu cha janga. Mazungumzo yao pia yameruhusu kubadilisha mawazo na mitazamo ya baadhi ya mada zilizopo za sasa kimataifa na kikanda, uhamasishaji wa amani na haki za kibinadamu ulimwenguni.