Tafuta

Papa Francisko ameonesha mshikamano wake wa udugu na upendo kwa waathirika wa Volkano kwenye Kisiwa cha La Palma nchini Hispania. Papa Francisko ameonesha mshikamano wake wa udugu na upendo kwa waathirika wa Volkano kwenye Kisiwa cha La Palma nchini Hispania. 

Mshikamano wa Papa Francisko na Waathirika wa Volkano La Palma!

Baba Mtakatifu Francisko alipenda kuonesha uwepo wake wa karibu, upendo na mshikamano wa kidugu kwa watu wote walioathirika na mlipuko huo. Baba Mtakatifu amewaombea pia wale wote wanaoendelea kutoa msaada kwa waathirika hawa, ili Bikira Maria, Mama Yetu wa Las Nieves, aweze kuwalinda. Volkano kulipuka kisiwani hapo mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 1971.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. –Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili tarehe 26 Septemba 2021 kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican aliwakumbuka na kuwaombea watu walioathirika kutokana na mlipuko wa Volkano ya Teneguía iliyoko kwenye kisiwa cha La Palma katika Visiwa vya Canary,  nchini Hispania  janga lililotokea tarehe 19 Septemba 2021. Watu zaidi ya 500 walihamishwa kutoka Kisiwani hapo kama sehemu ya hatua za usalama wa maisha yao. Viongozi wa Serikali ya Hispania wametembelea eneo hili ili kujionea maafa yaliyojitokeza.

Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Francisko alipenda kuonesha uwepo wake wa karibu, upendo na mshikamano wa kidugu kwa watu wote walioathirika na mlipuko huo. Baba Mtakatifu amewaombea pia wale wote wanaoendelea kutoa msaada kwa waathirika hawa, ili Bikira Maria, Mama Yetu wa Las Nieves, aweze kuwalinda na kuwapatia tunza yake ya Kimama.  Kwa mara ya mwisho, Volkano ya Teneguía iliyoko kwenye kisiwa cha La Palma katika Visiwa vya Canary ililipuka kunako mwaka 1971. Na takwimu zinaonesha kwamba, kabla ya hapo, mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 1430, kadiri ya Takwimu zilizotolewa na Taasisi ya “National Geographical Institute, ING, nchini Hispania.

Volkano

 

27 September 2021, 14:14