2021.07.21 Hija ya kitume ya Papa Francesco huko  Budapest kwa ajili ya Kongamo la Ekaristi Kimataifa. 2021.07.21 Hija ya kitume ya Papa Francesco huko Budapest kwa ajili ya Kongamo la Ekaristi Kimataifa. 

Hija ya Papa Francisko Budapest na Slovakia:sala katika moyo wa Ulaya

Papa Francisko atafanya ziara yake ya kitume nchini Hungaria na Slovakia itakayoanza tarehe 11-17 Septemba 2021.Katika fursa hiyo baada ya sala ya Malaika wa Bwana Dominika amekumbusha siku ambayo umefunguliwa Komangamo la Ekaristi jijini Budapest.Amekumbuka pia Mama Theresa wa Kalkuta,katika siku ambayo Mama Kanisa anafanya kumbukizi la Mtakatifu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Imebaki wiki moja kabla ya  Papa Francisko kwenda huko Budapest, lakini moyo wake uko tayari nchini Hungaria, ambapo atawasili siku ya Jumapili ijayo kwa ajili ya kufunga Kongamano la Ekaristi Kimataifa na ambapo mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana amekumbusha jini ambavyp atahitimisha tukio hilo muhimu la Kanisa na kwamba baadaye ataendelea naziara yake nchini  Slovakia. Hija yake itaisha siku ya Jumatano itakayofuata huko katika sherehe kubwa maarufu ya Bikira wa Mateso na Msimamizi wa Nchi hiyo. Papa Francisko akisalimiaa waandaaji wa safari hiyo, anawashukuru wote wanaomngojea na ambao wanataka kwa dhati kukutana naye. “Ninawaomba kila mtu anisindikize kwa sala na ninaiweka ziara nitakazofanya kwa maombezi mashujaa wengi wa imani ambao walishuhudia Injili katika maeneo hayo katikati ya uhasama na mateso. Wao wasaidia Ulaya kutoa ushuhuda, hata leo hii na sio kwa maneno bali juu ya yote kwa matendo na  shughuli za huruma na kukarimu, kwa tangazo la Bwana ambaye anatupenda na anatuokoa”.

Kumbukizi la Mama wa Upendo Mama Theresa

Papa Francisko amekumbuka siku kuu ya Mtakatifu Teresa wa Calcutta na kusema: “kwa wote wanamwita Mama Teresa". "Ninatoa salamu yangu kwa wamisionari wote wa Upendo, wanaojitoa ulimwenguni kote, mara nyingi katika huduma ya kishujaa na ninafikiria kwa namna fulani Masista wa Zawadi ya Maria, waliopo jijini hapa Vatican”.

Mwenye heri mpya nchini Argentina Ndugu mdogo, Mamerto Esquiú

Hata hivyo kabla  Papa alikuwa amezungumza juu aliyetangazwa mwenye heri Jumamosi, tarehe 4 Septemba 2021 huko  Catamarca, nchini Argentina, Mamerto Esquiú, ndugu mdogo mfransiskani na askofu wa Córdoba, ambaye alitangaza kwa bidii yote Neno la Mungu kwa ajili ya kujenga jumuiya ya Kanisa pia ya serikali. Papa Francisko ameongeza kusema: “ Mfano wake na utusaidie kuunganisha kila wakati sala na utume na kutumikia amani na udugu". Hatimaye  Papa amekumbuka kuwa katika siku chache zijazo, utakuwa ni Mwaka Mpya wa Kiyahudi “Rosh Ha-Shanah” na baadaye siku kuu mbili za: “Yom Kippur” na “Sukkot”. Kwa maana hiyo ametoa salamu zake kwa moyo na matashi mema kwa kaka na dada wote wa dini ya Kiyahudi. Mwaka mpya uwe na matunda mengi, amani na mema, kwa wale wote wanaotembea kwa uaminifu katika Sheria ya Bwana".

TAFAKARI YA PAPA DOMINIKA
05 September 2021, 13:48