Papa:Unafiki unahatarisha umoja wa Kanisa!

Katika katekesi ya Papa Francisko Jumatano tarehe 25 Agosti 2021,ametoa onyo juu ya tabia ambazo zinaweza kusababisha unafiki kwa watu na ambazo ni hatari katika umoja wa Kanisa.Na tusiogope kuwa wakweli na kusema ukweli,kusikia ukweli,na kuendana na ukweli.Kwa njia hii tunaweza kupenda."Mnafiki hajui kupenda.Kutenda vinginevyo na ukweli inamaanisha kuhatarisha umoja katika Kanisa,ambalo Bwana aliiombea”.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Barua ya Wagalatia inashangaza sana. Kama ilivyosikika Paulo anasema alivyo mkaripia Kefa yaani Petro, mbele ya jumuiya ya Antiokia, kwa sababu ya mwenendo wake haukuwa mzuri. Je ni kitu gani kilikuwa kimetokea hadi kulazimisha Paulo kutumia maneno magumu kumkaripia Petro? Labda Paulo alizidi kiasi na kuacha nafasi sana ya kuonesha tabia yake bila kunyamaza? Lakini tutaona kuwa si hivyo, japokuwa mara nyingine inatuweka katika mchezo wa uhusiano kati ya Sheria na uhuru. Lazima kurudi katika hilo mara nyingi. Ndivyo Baba Mtakatifu Francisko ameanza katekesi yake Jumatano tarehe 25 Agosti 2021, katika ukumbi wa Paulo VI jijini Vatican. Papa Francisko akiendelea na tafakari amesema kuwa “Akiwaandikia Wagalatia, Paulo anataja kwa makusudi tukio hili ambalo lilitokea huko Antiokia miaka ya kwanza. Alitaka kuwakumbusha wakristo wa jumuiya hiyo kuwa wasisikiliza kabisa wale ambao wanahubiri ulazima wa kufanya watairiwe na hivyo kuangukia chini ya sheria na maelekezo yake yote”.

Papa amesema kuwamba "Tukumbue kuwa ni hawa wahubiri wa kihitikadi ambao walifika hapo na walileta mkanganiko na wakondoa amani katika jumuiya hiyo. Kitu cha kukosolewa dhidi ya Pietro ilikuwa tabia yake katika kushiriki kwenye meza. Kwa Myahudi, Sheria ilikatazwa kula chakula na wasio Wayahudi. Lakini Petro mwenyewe, wakati mwingine, alikuwa ameenda Kaisaria katika nyumba ya akida Kornelio, ingawa alijua alikuwa akivunja Sheria. Ndipo akasisitiza: “Mungu amenionesha kwamba hakuna mtu awezaye kuitwa mchafu au najisi (Mdo 10:28). Mara tu waliporudi Yerusalemu, Wakristo waliotahiriwa ambao walikuwa waaminifu katika Sheria ya Musa walimlaumu Petro kwa tabia hiyo, lakini alijihesabia haki kwa kusema: “Nilikumbuka neno la Bwana alilosema: “Yohana alibatiza kwa maji, lakini wewe utabatizwa katika Roho Mtakatifu”. Kwa hivyo ikiwa Mungu aliwapa zawadi ile ile aliyotupatia sisi, kwa kumwamini Bwana Yesu Kristo, mimi nilikuwa nani kumzuia Mungu?” (Mdo11,16-17).

Papa Francisko amesisitiza kuwa “tukumbuke kuwa Roho Mtakatifu alikuwa katika muda huo katika nyumba ya Kornelio wakati Petro alikwenda hapo”. Tukio kama hilo pia lilitokea huko Antiokia mbele ya Paulo. Kabla, Petri alikuwa mezani bila shida yoyote na Wakristo ambao walitoka kwa wapagani; Walakini, wakati Wakristo wengine waliotahiriwa kutoka Yerusalemu, wale waliotoka Uyahudi, walipofika jijini, basi hawakufanya hivyo tena, ili wasilete ukosoaji wao. Na hii, Papa ameongeza kusema kuwa lazima kuwa mwangalifu, kosa lilikuwa kwamba [alikuwa] makini zaidi kwa kukosolewa, kwa kutoa maoni mazuri, kuliko ukweli, wa wengine? Na hii ni mbaya machoni pa Paulo, pia kwa sababu Petro alikuwa anaiigwa mfano na wanafunzi wengine, wa kwanza kabisa  kati ya wote ni Barnaba, ambaye pamoja na Paulo alikuwa akiinjilisha kwa Wagalatia (taz. Gal 2:13). Papa kwa kutoa mfano amesema “Bila kujua, Pietro, na njia hiyo ya kufanya kidogo kama hii, kidogo kama huko yaani kutokuwa wazi, kiukweli ilikuwa anaunda mgawanyiko usiofaa katika jumuiya: “Mimi ni safi ... mimi ninakwenda kwenye mstari huu, mimi lazima niende hivi, hii haiwezi kufanywa ...”

Paulo, katika karipio lake na hapa ndio kiini cha shida, kwani Paulo, katika lawama yake, anatumia neno ambalo linaturuhusu kuingia katika sifa za majibu yake: unafiki (rej. Gal 2:13). Hili ni neno ambalo litarudi mara nyingi: unafiki. Papa ameongeza “Nadhani sote tunaelewa inamaanisha nini ... Utunzaji wa Sheria kwa upande wa Wakristo ulisababisha tabia hii ya unafiki, ambayo mtume anania ya kupambana kwa nguvu na usadikisho. Paulo alikuwa mwadilifu, na alikuwa na kasoro zake, nyingi, nyingi ... tabia yake ilikuwa mbaya, lakini alikuwa mwadilifu. Je unafiki ni nini? Tunaposema kuwa mwangalifu kwa kuwa huyo ni mnafiki, tunamaanisha nini? Unafiki ni nini? Inawezekana kusema kuwa ni hofu ya ukweli. Mnafiki anaogopa ukweli. Anapendelea kujifanya badala ya kuwa mwenyewe. Hii ni kama kujipodoa rohoni, kama vile kujipodoa katika mitazamo, na ni kama kujipodoa katika njia ya kuendelea na sio ukweli. Ni kama kusema hapana ninaogopa kuendelea kama nilivyo na kwa maana hiyo ninajipondoa na mitazamo hii”.

Na uwongo huu unazuia ujasiri wa kusema ukweli kwa uwazi na kwa hivyo mtu hukimbia kwa urahisi jukumu la kusema kila wakati, kila mahali na licha ya kila kitu. Uongo huo unakuongoza kwa hili katika nusu ukweli. Na nusu ukweli ni uwongo, kwa sababu ukweli ni ukweli au sio ukweli. Lakini nusu ukweli ni hatua hii isiyo ya kitendo cha kweli. Mtu anapendelea, kama nilivyosema, kujifanya badala ya kuwa mwenyewe, na uwongo unazuia ujasiri huo, kusema ukweli waziwazi”, Papa amesisitiza. Akiendelea “Na kwa hivyo tunakwepa wajibu kwamba hii ni amri: kuisema kila wakati; kuwa mkweli: kuisema kila mahali na kuisema licha ya kila kitu. Na katika mazingira ambayo uhusiano wa binafsi unaishi chini ya bendera ya utaratibu, virusi vya unafiki huenea kwa urahisi. Tabasamu kama hilo ... eh eh ... hilo halitoki moyoni ... hii ni kama kujaribu kukaa vema na kila mtu, lakini kumbe bila kuwa na mtu yeyote …”, Papa amefafanua.

Katika Biblia, kuna mifano kadhaa ya kupambana na unafiki. Ushuhuda mzuri wa kupambana na unafiki ni ule wa mzee Eleazaro, ambaye alikuwa anaombwa kujifanya kula nyama iliyotolewa kafara kwa miungu ya kipagani ili kuokoa maisha yake: kujifanya kwamba amekula na hakuila. Au kujifanya kwamba alikula nyama ya nguruwe lakini marafiki zake walikuwa wamemuandalia nyingine. Lakini mtu huyo na ambaye hakuwa na umri wa miaka ishirini amesema Papa, alikuwa mcha Mungu na alijibu: “Haifai kabisa katika umri wetu kujifanya, na hatari kwamba vijana wengi, wakidhani kuwa miaka tisini Eleazaro amegeukia tamaduni za kigeni, nao pia kwa ssababu ya kujifanya uongo wangu, unafiki wangu, kwa muda kidogo tu kuliko maisha yangu, wanapotea kwa sababu yangu na kwa hivyo nasababisha aibu na doa kwa uzee wangu” (2Mac 6,24-25). Papa ameongeza kusema kuwa “uaminifu hauingii katika njia ya unafiki. Ni ukurasa mzuri sana wa kutafakari ili kuondokana na unafiki! Hata Injili zinaripoti hali mbali mbali ambazo Yesu anawalaani sana wale wanaoonekana kuwa waadilifu nje tu, lakini ndani wamejaa uongo na uovu” (rej. Mt 23: 13-29). Papa ametoa ushauri “Ikiwa mna wakati leo hii, chukua sura ya 23 ya Injili ya Mtakatifu Mathayo na uone ni mara ngapi Yesu anasema: wanafiki, wanafiki, wanafiki, na kufunua unafiki ni nini.”

Mnafiki ni mtu anayejifanya, kubembeleza na kudanganya kwa sababu anaishi kama vile amejifunika usoni barakoa, na hana ujasiri wa kuukabili ukweli. Kwa sababu hiyo, hana uwezo wa kukabiliana na ukweli na mnafiki hajui kupenda, anaishia kuishi kwa ubinafsi na hana nguvu ya kuonesha moyo wake kwa uwazi. Kuna hali nyingi ambazo unafiki unaweza kutokea. Mara nyingi hujificha mahali pa kazi, ambapo hujaribu kuonekana marafiki na wenzake lakini wakati ushindani unamsababisha afiche kisogo. Hata hivi amebainisha kuwa katika masuala ya kisiasa sio kawaida kupata wanafiki wanaopata mgawanyiko kati ya umma na watu binafsi. Unafiki katika Kanisa ni chukizo hasa, na kwa bahati mbaya kuna unafiki katika Kanisa, na kuna Wakristo wengi na wahudumu wanafiki. Hatupaswi kusahau maneno ya Bwana: “Maneno yenu na yawe ndiyo ndiyo, hapana hapana, zaidi hutoka kwa yule mwovu” (Mt 5:37). Papa Francisko amehitimisha kwa kuwaalika ndugu kaka na dada kufikiria leo hii kile anacholaani Paulo: unafiki; na kwamba Yesu analaani: unafiki. Na tusiogope kuwa wakweli na kusema ukweli, kusikia ukweli, na kuendana na ukweli. Kwa njia hii tunaweza kupenda. Mnafiki hajui kupenda. Kutenda vinginevyo na ukweli inamaanisha kuhatarisha umoja katika Kanisa, ambalo Bwana mwenyewe aliiombea.

KATEKESI YA PAPA 25 AGOSTI
25 August 2021, 11:17