Tetemeko kubwa huko Haiti tarehe 14.08.2021 Tetemeko kubwa huko Haiti tarehe 14.08.2021 

Papa Francisko yuko karibu na waathirika wa tetemeko huko Haiti

Papa Francisko amesali salamu Maria katika Uwanja wa Mtakatifu Petro na mahujaji wote mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana,kuwaombea mamia ya vifo vya watu na maelfu ya majeruhi kwa sababu ya tetemeko kali la ardhi ambalo limeleta uharibifu mkubwa,Jumamosi Agosti 14 huko Kusini mwa Kisiwa cha Haiti.Papa ametoa wito wa nguvu katika ushiriki hai wa jumuiya ya kimataifa ili wapate msaada.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Katika Siku kuu ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni, Jumapili 15 Agosti 2021, Papa Francisko mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana amesema kuwa: “Katika masaa machache yaliyopita, tetemeko kubwa la ardhi limetokea huko Haiti na kusababisha vifo vingi, majeruhi na uharibifu mkubwa wa mali. Ninaonesha ukaribu wangu na wale watu wapendwa waliokumbwa sana na tetemeko la ardhi. Ninapoinua maombi yangu kwa waathiriwa kwa Bwana, ninawasilisha neno langu la kutia moyo kwa walionusurika, nikitumaini kuwa mwitikio wa ushiriki wa msaada kutoka kwa jumuiya ya  kimataifa. Na mshikamano kutoka kwa wote ili upunguze matokeo ya janga hilo". Baadaye Papa ameongeza kuwaomba waamini wasali wote kwa Mama wa Yesu sala ya salamu Maria...

Papa akiendelea amewasalimia mahujaji wote waliofika kutoka pande zote za ndani na nje ya nchi. Hata hivyo pia amewakumbuka wale wote ambao wanapunzika katika maeneo mbali mbali  wawe na amani. Amewakumbuka ambao hawezi kwenda, wale ambao wanahudumia, na wale ambao wako katika hali ngumu, anawakumbuka wagonjwa, wazee wafungwa wasio na kazi, wakimbizi na wale wote wenye shida, ili Mama Maria awalinde. Papa ameshauri kwenda kwenye madhabahu ya Mama Maria kwa mfano watu wa Roma kwenda Kwa Maria  Salus Popoli Romani katika madhabahu ya Mama Maria Mkuu.

Tetemeko la Ardhi Huko Haiti, zaidi ya vifo 300 na maelfu ya majeruhi

Hili ni tetemeko kubwa la ardhi ambalo limekumba Haiti, na kuua karibu watu 304 na kuwajeruhi zaidi ya 1,800. Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 7.2 katika vipimo vya Ritcher, liligonga magharibi mwa nchi hiyo Jumamosi asubuhi tarehe 14 Agosti 2021, likavunja na kuharibu majengo yakiwemo makanisa na hoteli. Waziri mkuu amethibtisha  uharibifu mkubwa na kutangaza mwezi mmoja wa hali ya hatari. Haiti hadi sasa ilikuwa bado inajikwamua kutokana na athari za tetemeko baya la ardhi la mwaka 2010. Kina cha tetemeko hilo la Jumamosi kilikuwa karibu kilo mita 12, (maili 7.5) kutoka mji wa Saint-Louis ya Kusini, kwa mujibu wa uchunguzi wa wanajiolojia wa Marekani (USGs). Mtetemeko huo ulisikika katika mji mkuu wa Port-au-Prince uliyo na wakazi wengi, umbali wa kilomita 125, na mataifa jirani.  

Nyumba nyingi ziliharibiwa, watu wamefariki na wengine wako hospitalini. Waziri Mkuu Ariel Henry alisema jinis ambavyo ameandaa timu ya kufanya kazi ya kutoa misaada. "Kitu cha muhimu ni kuokoa manusura wengi iwezekanavyo waliokwama kwenye vifusi. Tumefahamishwa kuwa hospitali zimelemewa na kazi hasa ile ya Les Cayes inayowahudumia wale waliojeruhiwa na watu waliovunjika” amesema na baadaye, Waziri Henry alifichua kwamba alisafiri kwa ndege juu ya mji wa Cayes. Kwa mujibu wa Waandishi wa habari huko Le Nouvelliste walisema makanisa mengi na hoteli katika pwani ya kusini zimeporomoka au kuharibiwa vibaya.

Ushuhuda wa wamisionari

Nchi hii imechoka, amesema Maddalena Boschetti, mmisionari wa fidei donum kutoka Genova Italia ambaye amekuwa nchini humo kwa miaka 18 sasa na mahali alipo amesema kuwa walihisi tetemeko la ardhi lakini hakukuwa na uharibifu. Kila kitu kimejilimbikizia kusini mwa nchi wakati akizungumzia juu ya mateso mengi kwa watu. “Masikini ndio walio wazi zaidi na watajitahidi kujaribu kuendelea zaidi. Ni Mungu ambaye hutusukuma kwa sababu nguvu za wanadamu sasa ziko  katika ukomo".

Maombi na msaa wa maaskofu wa Marekani (USCCB) kwa Haiti

Msaada wa kiroho na zana, vimetolewa na Baraza la Maaskofu wa Marekani (Usccb). Kwa ajili ya Haiti, kisiwa ambacho kimepata mapngu mawili makubwa ya tetemekoKwa mujibu wa Askofu Mkuu José H. Gomez, wa Los Angeles na Rais wa Baraza la Maaskofu Marekani, anaelezea kwa kina sala zao kwa watu wa Hati ambao wanaomboleza kufuatia na kupotea kwa wapendwa wao na wanateseka na uhalribifu uliosababishwa na tetemeko. Kwa namna ya pekee katika Siku Kuu ya Kupalizwa mbinguni Bikra Maria, Bara azima linawaakikishia maombi kwa Askofu Mkuu Launay Saturné, na rais wa Baraza la maaskofu wa Haiti na waleo wote ambao bila kuchoka wanatoa huduma kwa jumuiya za waamini katika kisiwa. “tuna mshimano na Kanisa la Haiti. Katika wakati huu wa majaribi ili waweze kuhidi faraja, huruma na mkubatio wa Mama yetu wa Msaada, Msimamizi wa Kisiwa”. Na wakati huo huo Askofu Mkuu Gomez amewaalikwa wakatoliki wote na watu wenye mapenzi mema kusaidia shughuli ya waokoaji kwa kutegemea “Huduma Katoliki ya Msaada, yaani Shirika la katoliki la msaada wa kibinadamu la Baraza la Maaskofu Marekani. Anatanguliza shukrani kwa wote ambao wataweza kutoa msaada wao kwa ajili ya kaka na dawa wa Haiti.”

Kituo cha Caritas Italia huko Haiti

Mkakati wam shikamano zaidi wa ule wa kimataifa katika Kanisa na Caritas unahitajika. Mshtuko wa kutisha amesema Caritas ya Les Cayes iliyofikiwa kwa njia ya simu. Ofisi ya jimbo iliyobaki bila kuguswa kama muujiza, askofu na watawa uaskofuni wako salama, lakini inasadikika watu wengine inawezekanao wamebaki kwenye kifusi.  Jiji lilipigwa vibaya, majengo mengi yamebomolewa na kulala chini, barabara zime jaa maji. Onyo la Tsunami kando ya pwani zilizoathiriwa sana bado inaendelea kutishia na kuwa dharura. “Mawasiliano, hasa na maeneo ya vijijini, ni ngumu. Hata jimbo la Jeremie bado imetengwa kwa sasa kwa mujibu wa Caritas Italiana kwa maandishi.  Familia nyingi zimepoteza nyumba zao na wathiriwa ni wengi.

Makanisa na nyumba nyingi vimeanguka
Makanisa na nyumba nyingi vimeanguka
15 August 2021, 15:32