Papa:Waraka wa Laudato sì sio waraka wa 'kijani' ni waraka wa 'kijamii'!

Katika fursa ya ufunguzi wa kongamano la umoja wa vyuo vikuu wa Laudato si utakaofanyika 1-4 Septemba ijayo,Papa ametuma ujumbe kwa njia ya video:Waraka wa Laudato sio waaka wa "kijani", ni waraka wa "kijamii”.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Papa Francisko Jumanne tarehe 24 Agosti 2021 ametuma ujumbe mfupi kwa njia ya video kwa washiriki wa kongamano la umoja wa vyuo vikuu kwa ajili ya Laudato sì ambalo litafanyika kuanzia tarehe Mosi hadi  4 Septemba 2021.

Papa katika ujumbe huo kwa njia ya video anapenda kuwatia moyo juu ya juhudi hizi walizozianzisha na ili ziweze kuendeleza dhamiri kijamii na dhamiri kwa ajili ya utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja. Papa amesema kuwa: “Waraka wa Laudato sì, siyo  tu Waraka wa "kijani", badala yake ni Waraka wa "kijamii”. Kwa kuhitimisha ni matumaini ya Papa kuwa kongamano hilo litaweza kuwasaidia kuona uungwaji mkono na matokeo yake yote. Anawatakia mema na Mungu awabariki, lakini wasisahau kusali kwa ajili yake.

24 August 2021, 15:23