Je inastahili thamani ya kuzalisha kazi nzuri na za busara ikiwa tunahitaji kazi ya watumwa kufanya hivyo? Je inastahili thamani ya kuzalisha kazi nzuri na za busara ikiwa tunahitaji kazi ya watumwa kufanya hivyo? 

Papa Francisko:sio utamaduni wala uzuri ikiwa unatumia kazi ya watumwa!

Papa anamjibu Maurizio Maggiani,ambaye alikuwa amemwandikia barua ya wazi siku chache zilizopita kuhusu Karne ya XIX,akisimulia aibu ya kugundua njia za uhalifu kwa madhara ya wahamiaji ambapo vitabu vyake na vya waandishi wengine vilivyo chapishwa.Leo katika gazeti la Genova,La Stampa na magazeti mengine ya vikundi,vimechapisha jibu la Papa kwa kujibu mwandishi wa Italia kwamba“tunahitaji ujasiri wa kukataa faida zinazozalishwa kwa mifumo ya kifo”.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kichwa “Ujasiri wa Petttiroso”, moja ya vitabu vyake vinavyojulikana zaidi, kwa mara hii ilikuwa wakati wake. Mtunzi wa riwaya-David ambaye anajiuliza juu ya maadili ya tasnia ya kiwanda cha Goliathi, ambacho yeye mwenyewe ni mwanachama mwenye mamlaka, katika kesi hii ya uhariri, kwa sababu anachukizwa na uzembe fulani ambao wakati mwingine huepuka kuhakikisha ikiwa sehemu ya faida yake inaficha hali zisizo za kibinadamu, ikiwa chini ya uboreshaji wa bidhaa zake kuna mlolongo wa vurugu dhidi ya wale wanaozizalisha, ikiwa nyuma ya pambo la kiota cha hadithi zisizoonekana za mawindo yasiyoweza kujilinda na wawindaji wenye ukatili. Na kwenye kioo, upande wa pili, imani inayoju likana ya Papa, kwa njia fulani “mwenzake” wa kalamu na juu ya yote “sauti ya juu” kuuliza swali ambalo linasaliti shida ya msingi: Je inastahili thamani ya kuzalisha kazi nzuri na za busara ikiwa tunahitaji kazi ya watumwa kufanya hivyo?”

Kwa kulinganisha na Papa Francisko

Ni mazungumzo ya asili ya kina  ambayo yameibuka katika siku za hivi karibuni kati ya Maurizio Maggiani, mwandishi wa Vitabu na mwana habari wa Liguria nchini Italia na Papa  Francisko, ambaye aliyetaka kumjibu mwandishi wa riwaya kwa barua  ya tarehe 9 Agosti 2021, siku ambayo Kanisa lilikuwa linaadhimisha Kumbukizi la Mtakatifu Teresa Benedetta wa Msalaba (Edith Stein), Msimamizi  mwenza wa Ulaya kwa swali lililoulizwa hadharani na mwandishi katika barua wazi, iliyochapishwa tarehe Mosi Agosti iliyopita katika safu za karne ya 19, ambayo leo hii, pamoja na gazeti la Stampa na magazeti mengine, yamechapisha tena jibu la la Papa. Maggiani alitaka kushirikisha moja kwa moja na Papa Francisko kuhusu “aibu” aliyohisi katika kujifunza kutokana na habari za uhalifu kwamba hata katika uundaji wa vitabu vyake na vya waandishi wengine walipitia kampuni ya Veneto na kiwanda cha wakandarasi wadogo huko Trentino, wote wakituhumiwa na mahakama kuwa wametumia njia za uhalifu, zisizoweza kuelezeka”, anaandika Maggiani, kuwa  kazi ya wafanyakazi wa Pakistani, walivyofanywa vibaya”.

Nilijionea haya

Maggiani, ambaye anajiifafanua mwenyewe kama asiyeamini anasema kuwa "ninajua nguvu ya kinabii inayopasuka” ya Kristo lakini sikuwahi kupata zawadi, neema, kuwa mvumilivu kwa siku tatu kwenye kaburi lake, kusubiri na Maria Magdalena na kuona ufufuko wa mwana wa Mungu”, na kwa maana hiyo  anathibitisha kwamba alimgeukia Papa Francisko kwa sababu kadhaa, na sio tu  ile ya unyeti wa kushirikishana. “Historia ambazo ninapenda kusimulia na ambazo ninahisi ni jukumu la kufanya hivyo, ni historia za wanyamazaji, watu wa mwisho na wanyenyekevu",  lakini pia kutokujali kwake kwa sababu ilipatikana kwa wenzake katika sekta hiyo, na ni kana kwamba ni suala lisilofaa hivyo ilimfanya amgeukie Baba Mtakatifu kwa sabab,u anakiri  kuwa ni " katika kutafuta kwangu, siwezi kuona mamlaka mengine yoyote ya maadili ambayo, yanaweza kuwa na sauti kubwa, kwani anapatikana , anasikiza anajiuliza kabla ya kuhukumu”.

Kwa kujiuliza hasa juu ya athari zinazotokana na hofu iliyotumiwa katika kambi hiyo ya kisasa ya mateso, iliyojengwa kwenye ngozi ya wahamiaji maskini na malipo ya njaa, bila ratiba na haki, walipigwa mateke na kupigwa ngumi ikiwa walithubutu kuomba heshima: “Nilijionea haya, mimi ambaye ni mwangalifu sana kujaribu kukaa kuwa msafi wa mikono yangu na kutotumia bidhaa zinazoshukiwa kuwa za unyonyaji wa watumwa", lakini anakubali mwandishi huyo kuwa “sijawahi kutafakari juu ya ushahidi kwamba kazi yangu kama mwandishi wa riwaya, ni yenye sifa sana  na ni sehemu ya mlolongo wa mfumo wa uzalishaji, kile tunachokiita mnyororo wa ugavi, sio tofauti na nyingine yoyote, na kwa maana hiyo tunakabiliwa na upotofu huo huo”.

Kutazama visivyoonekana

Papa Francisko anajibu kwa kutuliza moja ya maoni muhimu ya mafundisho yake. Papa anakubali maneno ya Maggiani kuwa swali lake halina usumbufu, " kwa sababu mchezo ulio hatarini ni hadhi ya watu, heshima hiyo ambayo leo na mara nyingi sana inakanyagwa kwa urahisi na 'kazi ya watumwa', katika ukimya wa kushikamana na wa watu wengi. Tulikuwa tumeiona wakati wa karantini wakati wengi wetu tuligundua kwamba nyuma ya chakula kilichoendelea kufika kwenye meza zetu kulikuwa na mamia ya maelfu ya wafanyakazi bila haki: wasioonekana na wa mwisho japokuwa wao walikuwa wa kwanza! Wakiwa katika hatua za mnyororo wa usambazaji ambao, uliwanyima kupata chakula, mkate na kazi nzuri". Papa Francisko anaendelea, pia kuhusisha aina hii ya udhalilishaji na fasihi na labda ni ya kushangaza zaidi ikiwa kile ambacho Papa anafafanua kama mkate wa roho, usemi unaoinua roho ya mwanadamu, umejeruhiwa na uovu wa unyonyaji ambao hufanyika katika kivuli, inafuta nyuso na majina. "Kwa hivyo ikiwa kitu kinachochapishwa ambacho kinatokana na ukosefu wa haki ni haki yenyewe na kwa Mkristo, Papa anakumbusha "kila aina ya unyonyaji ni dhambi”.

Mambo mawili ya kufanya

Suluhisho, hata hivyo, sio kukata tamaa.  “Kukataa uzuri itakuwa ni kujirudisha nyuma pasipo haki, upungufu wa mema, anasema Papa Francisko, ambaye anapendekeza majibu kulingana na vitenzi viwili. Kwanza ni “kukataa mifumo ya kifo, miundo ya dhambi”, hadi kufikia kuandika vitu ambavyo havipendwi ili kuweza kuondoa kutokujali, kuchochea dhamiri, kuwavuruga ili wasiruhusu wenyewe kujiachia, kwa kudai hawajali, hawana uchungu, siyo kazi yao na wala biashara yao, au je tutafanya nini ikiwa ulimwengu utaenda hivi? Kitenzi cha pili ni kukataa. Kwa kumshukuru Maggiani kutokana na kuandika yale aliyoandika bila kujisumbua kuhesabu mapato, Papa Francisko anasema kuwa "pamoja na ujasiri wa kukemea tunahitaji ule wa kukataa. Ni kukataa na sio fasihi na tamaduni lakini kwa tabia na faida ambazo, leo hii kila kitu kimeunganishwa, tunagundua, kwa sababu ya mifumo potovu ya unyonyaji, inaharibu hadhi ya kaka na dada zetu. Ni ishara yenye nguvu kakataa nafasi nzuri na faraja ili kutoa nafasi kwa wale ambao hawana nafasi hiyo" anasema Papa. "Hii ni katika kutaka kufikia kusema hapana kwa ajili ya ndiyo iliyo kubwa na kufanya kupinga dhamiri ili kukuza hadhi ya binadamu”.

Utamaduni, sauti ya wanyonge, sio ya soko

Papa wa Kanisa maskini kwaajili ya maskini anarudia kusema kwamba anampenda Dostoevsky sio tu kwa kusoma vitabi vyake kwa undani roho ya mwanadamu na kwa hisia zake za kidini, lakini kwa sababu alichagua kuelezea juu ya maisha duni, ya kufedheheshwa na kukosea. Kwa kuzingatia hayo kunatoa mwaliko mkuu kwamba “mbele ya watu wengi waliodhalilishwa na kukerwa leo hii, bila mtu yeyote kuwafanya wahusika wakuu, wakati pesa na masilahi yanatawala, utamaduni ndio wito wa Papa Francisko ya kuwa “usijiruhusu kutawaliwa na soko”.

12 August 2021, 18:42