Papa Francisko amewatumia ujume washiriki wa Kongamano la Watawa wa Amerika ya Kusini Papa Francisko amewatumia ujume washiriki wa Kongamano la Watawa wa Amerika ya Kusini 

Papa Francisko:Furaha ni kielelezo cha Kikristo na shuhuda kwa waamini

Watawa wameombwa kuingia katika watu watakatifu waamini wa Mungu,kuwaheshimu,kuinjilisha na kumwachia yanayobaki Roho Mtakatifu.Amesema hayo Papa katika ujumbe wake kwa njia ya video kwa washiriki wa kongamano la Maisha ya kitawa barani Amerika ya kusinia lilianza tarehe 13litaisha tarehe 15 Agosti.Watawa wasisahau furaha ambayo ni kielelezo cha maisha ya kikristo na kuwa shuhuda bora kwa waamini.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko, Ijumaa tarehe 13 Agosti 2021, ametuma ujumbe wake kwa njia ya video kwa washiriki wa kongamano la Maisha ya Kitawa wa Bara la Amerika ya Kusini na Visiwa vya Carribien, ambalo litafungwa Jumapili tarehe 15 Agosti. Katika ujumbe huo Papa anawasalimu kwanza wote wanaofanya kwa njia ya mtandao kwa bara zima, ulioandaaliwa na Muungano wa Mashirika ya Kitawa barani humo( CLAR) kwa kuongozwa na kauli mbiu “Kuelekea maisha ya kitawa kwa njia ya muungano wa mashirika, utumadunisho na kutembea pamoja”. Papa Francisko amewashukuru kwa ushiriki huo. Anawakumbusha ni kwa jinsi gani ilivyo muhimu katika maisha ya kitawa hasa katika changamoto ya kutamadunisha imani. Na jinsi gani inaweza kuwa nzuri kwao pia kugundua kuwa umoja siyo mfanano, bali ni maelewano ya mitindo mingi. (taz Woswa wa Kitume wa Evangelii Gaudium 220), na anawaomba wasisahau kuwa Roho Mtakatifu ndiye mhusika mkuu ambaye anaunda maelewano hayo. Ni katika maelewano ya kuwa na mitindo mingi ili kuchukuliana vema tofauti na kuthamanisha zile muhimu katika roho safi na iliyo wazi ya tamaduni nyingi.

Papa Francisko amesema “uwepo wenu ni wa lazima kwa sababu unaweza kutoa na kukuza, kwa hakika taalimungu iliyotamadunishwa, ambayo inakubali hali halisi mahalia, na ikawa ndiyo injini ya uinjilishaji. Msisahau kuwa imani ambayohaitamadunishwi siyo ya kweli. Kwa maana hiyo ninawaalika kuingia katika kile ambacho kitatupatia uhalisia, kile ambacho kitatupatia maana ya kweli ya utumaduni ambao upo katika roho za watu. Ingieni katika maisha ya watu waaminifu, ingieni na heshima mila zao, tamaduni zao na kwa kutafuta kupeleka mbele utume wa utamadunisho wa imani na uinjilishaji wa utamaduni. Ni mambo mawili yanayofanana, utamadunisho wa imani na uinjilishaji wa utamaduni”, amesisitiza Papa.

Kuthamanisha kile ambacho Roho Mtakatifu alipanda kwa watu hata hiyo ni  zawadi kwetu sisi (Ibid. 246)”. Papa Francisko akiendelea amesema "utamadunisho huu ukipotea, maisha ya kikristo na kabla ya maisha ya kuwa utawa, inaishia katika nafasi za nadharia na za vichekesho kwa wasiomjua Mungu. Hii imeonekana, kwa mfano katika utumiaji mbaya wa liturujia. Kile ambacho hakihesabiwi ni itikadi na siyo hali halisi ya watu na hiyo sio Injili.  Papa amehimiza watawa hao wasisahau mambo mawili yanayofanana: kutamadunisha imani na kuinjilisha utamaduni. " Maisha ya kitawa ni mtaalamu wa muungano: maisha ya kitawa ni ya kutembea pamoja, ni mhamasishaji wa udugu. Pamoja na hayo katika nyakati zetu ni lazima kukabiliana na vishawishi vya namna ya kuishi".

Katika kufafanua suala hili  ametoa mfano kwamba “Ni mara ngapi wanahesabu kwamba ni watawa wa kiume  wangapi au ni masisita wangapi walioko kwenye shirika au kutathimimi ufungufu wake. Ni kishawishi cha kuishi. Ni vema kukataa mantiki za kuhesabu idadi, mantiki za kutojitosheleza ambazo zinaweza kuwabadili kuwa mitume wenye hofu, waliofungwa katika wakati uliopita na kulilia yaliyopita. Maombolezo hayo ndiyo wimbo wa maisha ya watawa”,  amesistiza Papa. Mbele ya hayo, mkakati na maamuzi ya busara zaidi yangekuwa ni kupokea fursa ya kutembela na Bwana katika njia za matumaini, kumtambua kuwa chini ya mwongozo kabisa wa Roho Mtakatifu ni tunda.

Kwa maana hii tufanye nini basi? Papa amuliza swali na kulijibu akisema: "ni kuingia katika watu watakatifu waamini wa Mungu, kuwaheshimi watu watakatifu waamini wa Mungu, kuinjilisha na kumwachia yanayobaki Roho Mtakatifu. (Yeye anajua yote na anasema katika nafasi yake ya pili: ingia katika watu wa takatifu wa Mungu, waheshimu watu waaminifu wa Mungu injilisha, wafanye wawe mashuhuda na yanayobaki mwachie Roho Mtakatifu). Kwa kuwasaidia, ili wafikie lengo ambalo wamekusudia, Papa Francisko amependa kuwakumbusha kuwa furaha na kielelezo cha hali ya juu cha maisha ya Kikristo,  ni kuwa shuhuda bora ambapo tunaweza kutoa kwa watu watakatifu waamini wa Mungu, ambao tunaitwa kuhudumia na kuwasindikiza katika hija yao ya kukutana na Baba".

Furaha,  zaidi ya mtindo. Amani, furaha, maana ya kuchangamka. Papa ameshauri waombe neema hii. Katika Wosia wake juu ya utakatifu, Papa mesema kuwa alipendelea kuweka sura mmoja kutokana na kwa maana ya kuchangamka. Ni jambo la huzuni anaema kuona wanaume na wanawake watawa ambao hawana maana ya kuchangamka, ambao  mara nyingi wamenuna. “Kukaa na Yesu ni kuwa na furaha, hata kuwa na uwezo huo kwa maana ya kuchangamka kutatoa utakatifu. Someni sura za Wosia wangu kuhusu utakatifu”, Papa ameshauri!

Kwa kuhitimisha: "Ninawatakia mkutano mwema kwa njia ya mtandao. Mungu awabariki na Roho Mtakatifu awajalie mwanga wa neema yake ili muweza kuwa daima wanaume na wanawake wa kukuta na kidugu. Bikira Maria awalinde. Yeye anajua nini maana ya kukutana, udugu, uvumilivi, na utamadunisho. Yeye anajua yote hayo. Aweze kuwalinda. Na saa kama ilivyo kawaida ninawaomba mimi kitu: msisahau kusali kwa ajili yangu, ninahitaji sana. Mkutano mwema” 

13 August 2021, 16:00