Watu wa Afghanistan wakiwa mpakani wanakimbilia nchi ya karibu Pakistan Watu wa Afghanistan wakiwa mpakani wanakimbilia nchi ya karibu Pakistan 

Papa kwa Afghanistan:suluhisho ni katika meza ya mazungumzo

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwanatarehe 15 Agosti 2021,Papa Francisko ameungana kwa roho moja na wasiwasi kwa hali ya nchi akiomba ili milio ya silaha zisitishwe.

Mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, Papa Francisko ameungana kwa roho moja na  wasi wasi kuhusiana na hali halisi nchini Afghanistan.  “ ninawaomba kusali na mimi kwa Mungu kwa ajili ya amani ili milio za silaha ndipo idadi ya watu waliopigwa wa nchi hiyo  wanaume, wanawake, wazee na watoto wataweza kurudi nyumbani kwao, kuishi kwa amani na usalama kwa kuheshimiana kwa dhati”.

Kila mmoja antafuta namna ya kukimbia kutoka Afghanistan
Kila mmoja antafuta namna ya kukimbia kutoka Afghanistan

Wapiganaji wa Taliban wametwaa udhibiti wa mji mkubwa wa kaskazini mwa Afghanistan, Mazar-i-Sharif, wakiukaribia mji mkuu, Kabul, na huku vikosi vya serikali vikikimbia na mataifa ya Magharibi yakiwania kuwaokowa raia wao waliopo Kabul. Maafisa wa jimbo la Balkh wanasema wanamgambo wa Taliban waliingia Mazar-i-Sharif bila upinzani wowote, ambapo wanajeshi wa serikali waliamua kukimbilia kwenye mpaka ya nchi na Uzbekistan.

Wasiwasi ni mkubwa kwa watu nchini Afghanistan
Wasiwasi ni mkubwa kwa watu nchini Afghanistan

Picha za video kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha magari ya kijeshi na wanajeshi wakijazana kwenye daraja la chuma baina ya mji wa Hairatan ulio Afghanistan na Uzbekistan. Viongozi wawili wa kivita wanaoongoza makundi ya wanamgambo yanayounga mkono serikali, Atta Mohammad Noor na Abdul Rashid Dostum, nao pia wamekimbia, huku Noor akiandika kwenye mitandao ya kijamii kwamba Taliban wamekabidhiwa udhibiti wa jimbo zima la Balkh. Kutwaliwa kwa mji huo ni ushindi muhimu kwa kundi hilo la siasa kali, ambalo ndani ya wiki chache limeshachukuwa takribani miji yote mikubwa. Miji miwili ya Kabul na Jalalabad iliyo mashariki mwa Afghanistan ndiyo pekee iliyoko mikononi mwa serikali hadi sasa

 

15 August 2021, 15:16