Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI tarehe 29 Juni 2021 amefanya kumbukizi la miaka 70 tangu alipopewa Daraja Takatifu ya Upadre. Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI tarehe 29 Juni 2021 amefanya kumbukizi la miaka 70 tangu alipopewa Daraja Takatifu ya Upadre. 

Papa Mstaafu Benedikto XVI Miaka 70 ya Daraja Takatifu 29 Juni 2021

Jumanne tarehe 29 Juni 2021, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI ameadhimisha kumbukizi la miaka 70 tangu alipopewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ushiriki wa Ibada ya Misa Takatifu iliyonogeshwa na Kwaya iliyokuwa ikiongozwa na Kaka yake Monsinyo Georg aliyefariki dunia hivi karibuni. Papa Francisko amempongeza kwa ushuhuda wake wa sala wenye mvuto mkubwa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI tarehe 29 Juni 1951 alipewa Daraja Takatifu ya Upadre akiwa na umri wa miaka 24, huku akiambatana na Kaka yake Georg kwenye Kanisa kuu la Jimbo kuu la Freising nchini Ujerumani. Jumanne tarehe 29 Juni 2021, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI ameadhimisha kumbukizi la miaka 70 tangu alipopewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ushiriki wa Ibada ya Misa Takatifu iliyonogeshwa na Kwaya iliyokuwa ikiongozwa na Kaka yake Monsinyo Georg aliyefariki dunia hivi karibuni. Wanakwaya wa Regensburg wengi wao wana umri kati ya miaka 40 hadi 60 walifunga safari kutoka ujerumani ili kushiriki katika kumbukizi hii ya miaka 70 tangu alipopewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya Sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo miamba wa imani, tarehe 29 Juni 2021 kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican amemshukuru na kumpongeza Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI.  Papa Francisko anasema maisha na utume wa Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI unagusa maisha ya watu wengi duniani. Amemshukuru kwa kuendelea kusali na kuliombea Kanisa katika maisha na utume wake akiwa kwenye Monasteri ya “Mater Ecclesiae” iliyoko kwenye viunga vya mji wa Vatican tangu mwaka 2013 alipong’atuka kutoka madarakani. Ni kiongozi ambaye amejisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya maisha na utume wa Kanisa. Mama Kanisa anamshukuru Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kwa ushuhuda wake wenye mvuto na mashiko!

Miaka 70 ya Daraja
30 June 2021, 16:31