Ziara ya Kitume nchini Itaq akiwa anatembelea Jumuiya ya Qaraqosh Ziara ya Kitume nchini Itaq akiwa anatembelea Jumuiya ya Qaraqosh 

Barua ya Papa kwa Mapatriaki wa Mashariki ya Kati:Neno la Mungu ni taa inayoangaza

Ustaarabu na tawala ngapi zimetokea kushamiri na kisha kuanguka na kazi zao nzuri na ushindi ardhini lakini kila kitu kimepita.Kwa kuanza na Baba Yetu Ibrahimu Neno la Mungu kinyume chake limeendelea kubaki kama taa ambayo inaangaza hatua zetu.Ni tafakari katika barua ya Papa Francisko aliyowaandikia mapatriaki katoliki wa nchi za Mashariki ya Kati.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko Jumapili tarehe 27 Juni 2021, ametuma barua yake kwa Mapatriaki Wakatoliki wa Nchi za Mashariki ya kati. Katika barua hiyo anafurahi kupokea mwaliko wao wa kuungana nao katika siku maalum ambayo kila mmoja anaadhimisha na waamini wake katika Liturujia ili kumwomba Bwana zawadi ya amani katika Nchi za mashariki ya Kati na kuiweka wakfu Familia takatifu. Tangu mwanzo wa Upapa wake, Papa amesema kuwa amekuwa karibu na mateso yao, kwa kufanya hija kwanza katika Nchi Takatifu, baadaye Misri, Nchi za uarabuni na mwisho kwa miezi ya hivi karibuni nchini Iraq, akiwaalika Kanisa zima kusali na mshikamano wa dhati kwa ajili ya Siria na Lebanon ambayo imejaribiwa na vita na ukosefu wa msimamo kijamii, kisiasa na kiuchumi.  Papa Francisko amethibitisha jinsi anavyokumbuka vema mkutano wa tarehe 7 Julai 2018 huko Bari, Italia hivyo anwashukuru kwa sababu ya mwaliko wao wa kuungana kwao, ambapo wanaandaa mioyo yao katika sala ijayo ya tarehe Mosi Julai itakayofanyika jijini Vatican pamoja na viongozi wakuu wa Makanisa ya Nchi ya Mwerezi.

Familia Takatifu ya Yesu, Maria na Yosefu ambayo wamechagua kuiweka wakfu Nchi za Mashari ya Kati inawakilisha vema utambulisho wao na utume wao, Papa amesisitiza. Familia hii awali ya yote ilikuwa inatunza fumbo la kujfanya mwili wa Mtoto wa Mungu na ilikuwa imeunda kuzunguka Yesu na katika sababu yake. Ni kwa njia ya  Maria alipotikika tamaza mimi hapa alipotangaziwa na Malaika huko Nazareth, na Yosefu alimkaribisha kubaki hata wakati wa usingizi ili kusikiliza sauti ya Mungu na kuwa tayari kufanya mapenzi yake mara moja alipoamka. Siri ya unyenyekevu na kujifunua kila kitu, kama vile kuzaliwa huko Bethlehemu, kutambuliwa na watoto wadogo na wale walio mbali, lakini kwa kutishiwa na wale walioshikamana zaidi na nguvu za kidunia kuliko kushangazwa na kutimizwa kwa ahadi ya Mungu. Ili kulinda Neno lililofanyika mwili, Yosefu na Maria walianza safari, wakienda Misri, wakiunganisha unyenyekevu wa kuzaliwa huko Bethlehemu na uzembe wa watu waliolazimishwa kuhamia. Kwa njia hii, hata hivyo, walibaki waaminifu kwa wito wao na bila kujua kuwa walikuwa  na hatima ya kuhama na kutengwa na mateso ambayo yalikuwa yawe ya Yesu wakati angekuwa mtu mzima na ambaye, hata hivyo, alifunua jibu la Baba yake asubuhi ya Pasaka.

Kuwekwa wakfu kwa Familia Takatifu Papa mesisitiza kwamba kunamwalika kila mmoja wao kugundua tena kama watu binafsi na kama jumuiya wito wao wa kuwa Wakristo katika Mashariki ya Kati, na  sio tu kwa kuomba utambuzi sahihi wa haki zao kama raia wa asili wa nchi hizo zinazopendwa, lakini kwa kuishi utume wao kama walinzi na mashahuda wa asili wa kwanza wa kitume. Papa Francisko amesema kuwa katika ziara yake nchini Iraq alitumia fursa mbili za picha ya zulia, ambayo inaonesha mikono yenye ujuzi ya wanaume na wanawake wa nchi za Mashariki ya Kati wanaojua jinsi ya kusuka, kuunda kijiometri sahihi na picha za thamani, matokeo ya kuunganishwa kwa nyuzi nyingi ambazo huwa kito tu, kwa sababu ya kuwa pamoja bega kwa bega. Ikiwa vurugu, wivu, mgawanyiko, vinaweza kuja kubomoa hata moja ya nyuzi hizo, zulia zima linajeruhiwa na kuchafuliwa. Wakati huo, mipango na makubaliano ya kibinadamu hayawezi kufanya kidogo ikiwa hatuamini nguvu ya uponyaji ya Mungu. “Msijaribu kukata kiu yenu kwenye vyanzo vya sumu ya chuki, lakini acha mifereji ya shamba la mioyo yeni inyweshwe na umande wa Roho, kama watakatifu wakuu wa tamaduni yao husika ya Coptiki, Maronite, Melkite, Kisiria, Kiarmenia, Kikaldayo, Kilatino.

Ustaarabu na tawala ngapi zimetokea, kushamiri na kisha kuanguka na kazi zao nzuri na ushindi ardhini: kila kitu kimepita. Kwa kuanza na Baba Yetu Ibarahimu Neno la Mungu kinyume chake limeendelea kubaki kama taa ambayo inaangaza hatua zetu. Papa Francisko ameongeza kusema “Ninakachia amani, ninakupa amani yangu”, Bwana Mfufuka aliwaambia wanafunzi wakiwa bado wanaogopa katika Chumba cha Juu baada ya Pasaka. Kwa maana hiyo Papa amesema kwamba hata yeye kwa kushukuru ushuhuda wao na uvumilivu wao katika imani, anawaalika kuishi unabii wa kibinadamu wa udugu, ambao ulikuwa kiini cha mikutano yake huko Abu Dhabi na Najaf,  pia katika Barua yake  ya Fratelli Tutti yaani Wote ni ndugu. Kwa kuhitimisha Papa Francisko amewaomba wawe chumvi ya kweli ya ardhi yao, watoe ladha ya maisha ya kijamii yanayotamanisha kuchangia ujenzi wa wema wa pamoja kwa mujibu uliolekezwa katika Wosia wa Kitume wa Baada ya Sinodi ya nchi za Mashariki na kama alivyopenda kukumbusha wakati wa miaka 103 ya Barua Rerum Novarum. Amewapa baraka yake ya kitume kwa moyo wote ambapo wamefika katika maadhimisho hayo na wale wote ambao watafuatilia kwa njia ya vyombo vya habari na amewaomba wasali kwa ajili yake.

27 June 2021, 10:05