Mgogoro mzito nchini Colombia Mgogoro mzito nchini Colombia 

Wito wa Papa wa kuombea Nchi ya Colombia

Papa Francisko ameomba waamini wote kusali kwa ajili ya hali nchini Colombia ambayo inaendelea kuwa ya wasi wasi.Katika Siku Kuu ya Penkoste anasali ili watu wapendwa wa Colombia watambue kupokea zawadi ya Roho Mtakatifu na ili waweze kupata suluhisho la haki katika matatizo mengi ambayo wanateseka hasa zaidi maskini.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mara baada ya sala ya Malkia wa Mbingu Jumapili tarehe 23 Mei, ambapo Mama Kanisa ameadhisha siku kuu ya Pentekoste, Papa Francisko ameomba waamini wote kusali kwa ajili ya hali nchini Colombia ambayo inaendelea kuwa ya wasi wasi. Katika Siku Kuu ya Penkoste anasali ili watu wapendwa wa Colombia watambue kupokea zawadi ya Roho Mtakatifu na ili waweze kupata suluhisho la haki katika matatizo mengi ambayo wanateseka hasa zaidi maskini, kwa sababu ya janga la virusi. Ameshauri wote kuzuia kwa sababu za kibinadamu zinzaoleta madhara kwa watu katika zoezi la haki wakati wa maandamano ya haki.

Laudato si

Papa Francisko, amekumbusha kwa Jumatatu inahitimishwa Mwaka wa Laudato si. Amewashukuru wote ambao wamishiriki kwa wingi katika mipango mingi ulimwengu wote. Ni safari ambayo lazima kuendelea pamoja  kwa kusikiliza kilio cha dunia na maskini. Kufutana na hilo,  amebainisha jinsi ambavyo watazindua juwkaa la Laudato si, ambao ni hatua ya machakato wa safari ya  miaka saba ambayo itaongozwa familia, jumuiya za parokia  na majimbo, shule na vyuo vikuu, hospitali na makampuni, makundi, harakat, mashirika ya kiraia, taasisi za kitawa ili kuchukua wajibu wa kuwa na mtindo wa maisha endelevu. Amewatakia matashi mema wahudumu wengi ambao wametumwa kueneza Injili ya kazi ya uumbaji na kuchukua wajibu wa kutunza nyumba yetu ya pamoja.

Maombi kwa watu wa Goma DRC

Papa Francisko ameomba wasali kwa ajili ya watu wa mji wa Goma, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC ambao wamelazimika kukimbia kwa sababu ya mlipuko mkubwa wa Volkeno huko Nyiragongo. Amewasalimiwa wote wanatoka Roma na Italia lwa ujumla na nchi nyingine  akiwatakia kila jema ya sikukuu.

23 May 2021, 16:19