Papa Francisko padre Frédéric Fornos Mkurugenzi wa Utume wa Sala Kimataifa Papa Francisko padre Frédéric Fornos Mkurugenzi wa Utume wa Sala Kimataifa 

Video ya Papa katika utume wa sala kwa mwaka 5 inatafsiriwa kwa lugha 23

Kila mwezi Papa Francisko anashirikisha nia ya sala kwa njia ya video.Ni mpango wa kimataifa mbao Jumapili tarehe 23 umefikisha miaka 5 tangu kuanza kwake na ambao tayari unatangazwa kwa lugha 23.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kila mwezi Papa Francisko anashirikisha nia za sala kuhusu changamoto za ubinadamu na utume wa Kanisa. Mtandao wa Utume wa sala ya Papa unafanya huduma ya kuelewesha nia kwa njia ya video za Papa, ambapo ni mpango wa kimataifa naambao umezidi kukua katika mitandao ya kijamii na ambao kufika mwaka 2021 tayari una matoleo 23 ya lugha mbali mbali. Video ya kwanza ya Papa ilizinduliwa mnamo 2016 kwa lugha tisa rasimi: kihisapinia, kiingereza, kireno, kiitaliano, kifaransa, kijerumani, Netherlands (Kidachi), kiarabu na kichina. Na kadiri siku ambazo zimepita mpango huo umekua na kuongezwa lugha nyingine kama vile ya kivietnam, kichina, kipoland, kiswahili, kinyarwanda, kikatalani, kirithuania, kislonenia, kihindi, kirusi kikorea na kijapani. Na katika mwaka huu wa tano katika video za Papa, wameongeza hata lugha nyingine mbili ya kifilipino na Maya-Q'eqchi.  Leo hii video za nia za sala ya Papa zimewafikia zaidi ya watu milioni 155 kupitia katika mitandao ya kijamii ya vatican, na washirika wake ambao wamefikia zaidi ya 17,000 katika makala za magazeti ya kimataifa.

Padre Frédéric Fornos S.J, Mkurugenzi wa Mtandao wa Kimataia wa Papa ameeleza jinsi ilivyo muhimu kwamba ujumbe wa Papa uweze kufikia lugha zote na tamaduni zote: “sala ni moyo wa utume wa Kanisa, anasema Papa. Anayesali anaingia katika mawasiliano ya upendo na Baba, ni uhusiano wa kina na hakuna kilicho zaidi bora cha kuweza kuzungumza katika lugha yake binafsi. Kama Lugha mama ya Yesu ya Kiaramu ambacho alikitumia kusema ‘Abba’, ‘Padre’, ‘Baba yangu’, kusali kwa ajili ya changamoto za binadamu na utume wa Kanisa na ndiyo hakuna kingene zaidi ya kueneza sala ya Papa katika lugha yake. Kila mmoja anasali kwa lugha yake, lakini wote tunaungana katika sala.

Video ya Papa inaendelea kukua kwa nammna kwamba watu wote ulimwenguni wanaweza kuungana kwa nia za Baba Mtakatifu. Kila mmoja anasali kwa lugha yake na wote wanasali kwa  ajili ya changamoto za binadamu na utume wa Kanisa. Mpango huo umeendelezwa shukrani kwa zawadi inayowezekana kupitia tuvuti yao. Mtandao wa kimataifa wa nia za sala ya Papa ni kazi  Shughuli ya Kipapa ambayo utume wake unaendeshwa na wakatoliki kupitia sala na matendo ya dhati mbele ya changamoto za binadamu na utume wa Kanisa. Changamoto hizi zinawalikisha si chini ya nia za sala ambazo zimependwa na Papa Francisko kwa ajili ya Kanisa zima. Utume wake umeandikwa katika moyo wa Yesu na utume wa huruma kwa ajili ya ulimwengu mzima. Utume wa Sala ulianzishwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1844 na upo katika nchini 89 na ambao unafikiwa na wakatoliki zaidi ya milioni 22. Unajumuisha kitengo cha vijana “harakati Ekaristi ya Vijana (MEG). Mnamo Desemba 2020, Papa Francisko aliunda Mfuko wa Kipapa wa Vatican na kuthibitisha kanuni zake mpya. Mkurugenzi wake kimataifa na Padre P. Frederic Fornos, S.J. Kwa maelezo zaidi bonyeza: www.popesprayer.va/it/.

23 May 2021, 16:31