Bahari Bahari  

Barua ya Papa kwa Kard.Turkson:hitaji la ekolojia fungamani baada ya janga

Papa Francisko ametuma barua kwa Kardinali PeterTurkson katika fursa ya Mkutano kuhusu' kujenga udugu na kulinda haki.Changamoto na fursa kwa watu wa visiwani'.Ni katika fursa ya mkutano uliofanyika katika ‘Juma la Laudato sì’ ambapo Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu pamoja na Kituo cha kianglikani Roma wameandaa pamoja mkutano huo kama mpango wa kekumene.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ijumaa tarehe 21 Machi 2021 katika Juma la Laudato si, Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binadamu na Kituo cha Kianglikani Roma wameandaa mkutano wa kiekumene pamoja kwa kujikita na mada kuhusu “Kujenga udugu,na  kulinda haki. Changamoto na fursa kwa ajili ya watu wa visiwani”.  Mkutano huo umependekeza kuchunguza wasi wasi unaohusu hali halisi ya haki za mtu na haki za watu katika mantiki maalum ya Nchi zinazoishi kwenye visiwa, pamoja na changamoto za kijamii na maazingira katika mwanga wa Waraka wa Laudato Si’ na Fratelli tutti nyaraka zote zikiwa za Papa Francisko. Mkutano huo umefanyika kwa njia ya mtandao.

Katika fursa hiyo ya Mkutano Papa Francisko ameomba kufikisha salamu zake pia kwa matashi mema kwa waandaaji na wote ambao wameshikriki mkutano huo. Amemsalimia Wavel Ramkalawan, rais wa Jumhuri ya Seychellesna, Askofu Mkuu Justin Welby, wa Canterbury Uingereza, kwa shukrani ya kishiriki kwao. Mkutano huo ni muhimu wa kiekumene ambao wanaendelea na mazungumzo yaliyozaliwa kwa hekima na uzoefu tofauti wa tamaduni za kikristo na ambao unatoa kwa waamini, viongozi wa serikali na wajumbe wa jamii ya raia na zaidi kwa vijana fursa kwa ajili ya kukabiliana na changamoto maalum ambazo zinawakumba watu wanaoishi visiwani, Papa amebainisha.

Papa Francisko ametaja kuwa kati ya changamoto hizi kuna vurugu, ugaidi, umaskini, njaa na aina mbali mbali za ukosefu wa haki na usawa wa kijamii pamoja na uchumi ambao leo hii unawakumba wote hasa wanawake na watoto. Wasiwasi hata ni juu ya watu wanaoishi visiwani ambao wako wazi katika mabadiliko ya tabianchi uharibufu wa kutisha, baadhi ni matokeo ya unyonyaji usiothibitiwa wa rasilimali asili na za binadamu. Kutokana na matokeo hayo amesema hatuoni  uzoefu wa uharibifu wa mazingra tu, lakini hata uharibifu wa binadamu na jamiii ambayo iko hatari zaidi ya maisha ya wakazi wa visiwa na maeeno ya bahari. Ni mategemeo ya Papa kuwa mkutano huo unaweza kutoa mchango wa maendeleo ya kisiasa kimataifa na kikanda kwa  ili kukabiliana na changamoto kwa namna ya kweli na kuongeza uelewa wa uwajibikaji wa kila mmoja katika kutunza nyumba yetu ya pamoja.

Hata hivyo ikumbukwe kwamba mkutano huu umekusudia kutoa mwonekano na kuelezea mshikamano kwa watu wanaohusika na pia kujenga mitandao ya mshikamano kwa lengo la kutembea hatua ya pamoja. Miongoni mwa mada ambazo zimechunguzwa ni haki za watu wa kiasili, haki ya kujitawala na uhuru wa watu juu ya maliasili zao. Wakati huo huo, tukio hilo limechunguza mchango wa watu wa visiwa katika ujenzi wa ulimwengu unaojumuisha na wenye haki, hasa kupitia tafakari inayotokana na msingi wa kidini ambao unakusanya uzoefu wa karne nyingi na hekima" (Fratelli tutti, 275). Mpango huo unawahusu watu wote wanaoishi katika visiwa vya Bahari la Atlantiki, Hindi na Pasifiki na unahusisha watendaji wa ndani, kama vile mamlaka ya serikali na mashirika ya kijamii, kufuatia njia ya kiekumene na ya kidini. Mkutano huo pia umekuwa na vijana kutoka kanda zinazohusika kama wahusika wakuu.

21 May 2021, 16:09