Mama Yetu wa Fatima Mama Yetu wa Fatima 

Papa:Msiwe nakala bali wa kweli kama watakatifu

Katika fursa ya Hija ya 25 ya kitaifa ya wahudumu wa altareni huko Fatima,Papa ametuma ujumbe kwa,rais wa Tume ya Maaskofu wa Ureno kwa ajili ya Liturujia na Kiroho.Amemtaja mwenyeheri Carlo Acutis katika Ekaristi alikuwa amepata njia kuu ya kwenda Mbinguni.Anawakumbusha maisha yao sio kijivu na kazi ambayo wanaalikwa ni ile ya kuangaza nuru inayotoka kwa Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ni kutazama Mtakatifu Yosefu Mlinzi wa Yesu na Familia Takatifu pia kwa watakatifu ambao wameshuhudia kwa njia ya  maisha namna asili ili kumfikia Bwana. Ndivyo Papa Fracisko anaelekeza njia kwa wahudumu wa altareni nchini Ureno katika ujumbe alioutuma  kwa Askofu José Manuel Garcia Cordeiro, wa  Bragança-Miranda  na rais wa Tume ya Maaskofu wa Ureno kwa ajili ya Liturujia na Kiroho. Ni katika fursa ya Hija ya 25 ya kitaifa kwa wahudumu wa altareni iliyofanyika huko Fatima siku ya Mei Mosi 2021. Papa Francisko katika ujumbe huo anaandikiìa kwamba wawe watakatifu kwa sababu awali ya yote wao ni wahudumu wa fumbo ambalo linajikita kwa tabia kushiriki kwa  undani na nje na kusali.

Vijana wawe na shauku kubwa ya kukutana na Yesu

Huduma yao kama wahudumu inakuwa ya utaalamu wa imani kwa ajili ya jumuiya. Ili kufanya hivyo, Papa amewashauri wawe na shauku kubwa kwa umri wao wa kukutana na Yesu, kujikabidhi mikononi mwa  Yesu, mawazo yao mudaa wao na yeye hatakosa kuwakirimia, na kuwapatia furaha na kuwafanya wahisi ni wapi wanapata furaha ya kweli. Papa Francisko ametaja baadhi ya watakatifu ambao katika Ekaristi waliweze kumwilishwa safari yao ya ukamilifu, kwa mfano Mwenyeheri Alexandrina Maria wa Costa ambaye kwa maka 14 alimwilishwa kwa ekaristi peke yake, au Mtakatifu Francis Marto, mmoja wa wachugaji wadogo wa Fatima waliotokewa na Mama Maria.

Watakatifu na asili

“Tunapozungumza juu ya kuiga mifano ya watakatifu, haimaanishi kuiga nakala ya njia yao ya kuishi na kuishi utakatifu, kwani kuna ushuhuda ambao ni muhimu sana ambao ni kutuchochea na kutuhamasisha” Papa amefafanua na kuongeza kuwa, “lakini sio kujaribu kuiga kwa sababu hii inaweza pia kutupeleka mbali kipekee njia maalum ambayo Bwana ametuandalia”. Mwaliko wake ni kwamba wawe  mwenyewe  na sio kuwa nakala,  lakini kuwa na msukumo kwa wengine, ukiacha alama yako kibinafsi. Papa Francisko amemtaja Mwenye Heri Carlo Acutis na sentensi yake: “Wote wanazaliwa wakiwa asili, lakini wengi wanakufa kama nakala”.

Matumaini yasiyo katisha tamaa

 “Usijiruhusu uangukie kwenye ulaghai, ambao utadhalilisha na kukufanya tuwe kijivu. Maisha sio kijivu, maisha yanapaswa kuzingatia maoni mazuri. Usifuate watu hasi, lakini muendele kuangaza karibu na ninyi nuru na matumaini ambayo hutoka kwa Mungu! Kama mnavyojua, tumaini hili halivunji moyo; kamwe hakuna kukata tamaa!  Papa amesisitiza. “Pamoja na Mungu hakuna kinachopotea, lakini bila yeye yote yanapotea. Msiogope, kwa maana hiyo mjitume  na kujiweka mikononi mwa Baba yetu wa mbinguni na kumtumainia ”.

Makuhani wawe baba, walimu na mashuhuda

Hatimaye Papa Francisko ametoa, mwaliko kwa wahudumu wa Altareni kumwomba Mtakatifu Joseph kwa uaminifu na bidii na kwa makuhani wa parokia, huku akinukuu Mtakatifu Yohane Paul II, anakumbusha  kwamba mikononi mwao wanaona Ekaristi ikifanyika na kwa sababu hiyo anawashauri  kuwa baba, waalimu na mashuhuda wa uchaji wa Ekaristi na utakatifu wa maisha.

03 May 2021, 16:33