2019.05.04Kikizi cha Uliniz cha Kipapa  2019.05.04Kikizi cha Uliniz cha Kipapa  

Papa kwa kikosi cha Ulinzi Vatican:Muwe ishara ya makaribisho ya Kanisa

Papa Francisko Alhamisi tarehe 6 Mei 2021 akikutana na wahimu wa Kikosi cha Ulinzi wa Kipapa,ambao watakula kiapo mchana katika Uwanja wa Mtakatifu Damas Vatican ameangazia huduma yao maalum ambayo watatimiza hasa kuanzia na ibada na uaminifu kwa Makao ya Kitume.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Wahitimu wapya wa Kikosi cha ulinzi wa Kipapa kutoka Uswiss, kichulikanacho kama “Swissguards”, kabla ya kula kiapo cha utii kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro, siku ya Alhamisi tarehe 6 Mei 2021 wamekutana na Papa Francisko wakiwa katika mavazi yao rasmi ya kihistoria ambapo Papa Francisko katika hotuba yake amekazia uaminifu na upendo kwa Papa, katika huduma yao ambayo leo amesema ni msingi na ambayo inafanywa kwa ibada na kiroho kwa pamoja. Papa Francisko ameeleza jisi ambavyo kipinid ambacho wanakuwa hapo kinawasaidia kutambua vema wito wao wa maisha. Anawasifu kwa shughuli zao wanazojikita nazo hasa ule uwezekano wao na utayari wa kutoa msaa kwa wale wanao wakimbilia au kuuliza na hata kwa ile salamu ya heshima.

Papa amesema “Ninashukuru sana uwezo wenu wa kuchanganya nyanja za kitaalam na za  kiroho, kwa kuelezea kujitoa kwenu na uaminifu katika makao makuu ya Kitume. Kwa upande wa, mahujaji na watalii wanaokuja Roma mnayo nafasi ya kufanya uzoefu wa huduma yenu na usaidizi kama walinzi katika malango yote ya Jiji la Vatican. Kamwe msisahau sifa hizi, ambazo zinawakilisha ushuhuda mzuri na ni ishara ya kukaribisha ya Kanisa”.

Wito wa ukarimu

Akisalimiana pia na wazazi wa wahitimu hawa Papa Francisko amesema kwamba uwepo wao unathibitisha kushikamana na Wakatoliki wengi wa Uswiss kwa Kanisa, hasa katika  Makao ya Petro. Amekumbuka pia sadaka ya maisha iliyotolewa na Walinzi wa Uswiss, katika huduma ya Papa na uwezekano wa vijana kujitoa kwao kwa miaka michache  kwa ukarimu wao kwa Mrithi wa Petro na kwa jumuiya ya kikanisa.

“Bwana wakati mwingine huwaita wengine wenu kumfuata katika njia ya ukuhani au maisha  mengine ya  kujitoa wakfu, na kupokea hizo zinazo patikana ili kukuza usahihi wakati wa utoaji wa huduma ya ulinzi. Wengine, kwa upande mwingine, hufuata wito wa ndoa na kuunda familia zao. Ninakushukuru Bwana, chanzo cha mema yote, kwa zawadi tofauti  na miito mbalimbali ambayo anawakabidhi, na ninaomba kwamba wale wanaoanza huduma yao sasa pia waweze kuitikia kikamilifu wito wa Kristo, wakimfuata kwa ukarimu wa uaminifu” . Hatimaye ni matumaini kwamba" uzoefu wenye kuzaa matunda kiroho na kibinadamu jijini  Vatican na katika jiji la Roma yanaweza kuwa fursa ya kuimarisha imani na kufanya upendo wenye nguvu zaidi kwa Kanisa.

Kikosi kidogo

Kikosi kipya kimeunda na wajeshi  34 ambao  wataapishwa katika uwaja wa Mtakatifu Damas mbele ya Askofu Mkuu Edgar Peña Parra, kwa niaba ya  Papa. Katika uwanja wa Mashahidi wa Roma taji litawekwa kwanza kukumbuka kifo cha kishujaa cha askari 147 wa Uswiss ambao walipoteza maisha kwa kumlinda Papa Clement VII, wakati wa vita vya Roma mnamo 1527.

Hata hivyo kutokana na  hali ya kiafya ya sasa, hafla hiyo itafanyika bila kuwa na hadhira na kulingana na kanuni za sasa dhidi ya Covid. Kikosi hiki kilinzishwa na Papa Julius II, mnamo 1506, ambapo Walinzi wa Uswiss sasa wanaongozwa na Kanali Christoph Graf. Kazi yao ni kusimama katika milango yote ya Vatican, kutekeleza huduma za utaratibu na uwakilishi wakati wa sherehe za Papa na mapokezi ya serikali na kulinda Baraza la Makardinali  ikitokea dharura ya kiti kuba wazi.

06 May 2021, 16:46