2021.05.03 Mkutano wa kawaida wa umma kwa ajili ya kuridhia kutangazwa kwa watakatifu 2021.05.03 Mkutano wa kawaida wa umma kwa ajili ya kuridhia kutangazwa kwa watakatifu  

Papa Francisko aridhia kutangazwa kwa watakatifu 7

Papa Francisko ameongoza maadhimisho na mkutano wa kawaida kwa umma mjini Vatican wa kura juu ya mchakato wa kuwatangaza watakatifu saba.Tarehe ya kutangazwa kwao bado haikutolewa.Kardinali Semeraro amesema hawa walimshuhudia Kristo kwa zawadi yao ya maisha au kwa mazoezi ya upendo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko ameongoza masifu ya sala na mkutano wa umma wa kawaida  wa Mkardinali katika Jumba la Kitume Vatican  Jumatatu tarehe 3 Mei 2021 kwa ajili ya uchaguzi wa baadhi ya michakato ya kuwatangazwa wenyeheri kuwa watakatifu. Walioshiriki ni makardinali wakazi wa  Roma au waliopo Roma. Katika Mkutano huo Papa ameridhia wenyeheri 7 ili waandikwe kwenye kitabu cha Watakatifu katika tarehe ambayo itatangazwa. 

Wenyeheri 7

Wenyeheri hao 7 watatangazwa kuwa Watakatifu wakati wa Misa japokuwa tarehe bado haukitangazwa  kwa sababu ya janga la virusi vya sasa. Wenyeheri hawa ni Mwenyeheri Lazzaro, aliyejulikana  Devasahayam, mlei na shaihidi; mwenyeheri César de Bus, kuhani na mwanzilishi wa Shirika la Mapadre wa Mafundisho ya kikristo; Mwenyeheri  Luigi Maria Palazzolo, Kuhani na Mwanzilishi wa Shirila la Watawa wa kike Maskini linajulikana kama Taasisi ya Palazzolo; Mwenyeheri  Giustino Maria Russolillo, kuhani na mwanzilishi wa Chama cha Miito Mitakatifu na Shirila la Watawa wa kike wa Miito Mitakatifu; Mwenyeheri   Charles de Foucauld, kuhani wa jimbo; Mwenyeheri  Beata Maria Francesca wa Yesu   (zamani aliitwa Anna Maria Rubatto), Mwanzilishi wa Watawa wa sekolari Wakapuchini huko Loano; Mwenyeheri  Maria Domenica Mantovani, Mwanzilishi mwenzake na Mkuu wa Kwanza wa Shirika la Tawawa wadogogo wa Familia Takatifu.

Kardinali Semeraro: Watakatifu wapya ni waombezi wa neema na miujiza

Wenyeheri hawa si wa kushangaza watu wa Mungu kwa ajili ya nuru ya  fadhila zao tu, bali hata kwa njia ya maombezi yao neema na miujiza. Amesema hayo Kardinali Marcello Semeraro, rais wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza wenyeheri na watakatifu wakati akiwakilisha kwa Papa na Makardinali waliounganika pamoja katika Ukumbi wa mkutano. Ameweza kutoa ufupi  wa maisha yao kibinadamu na kiroho ya wenyeheri hao 7 katika nyakati tofauti na miito yao tofauti, na ambao kwa dhati waliweza kushuhudia kama zawadi kuu ya maisha hata katika mazoezi ya kishujaa ya upendo na fadhila, ambayo ni matunda ya Pasaka ya Kristo na chanzo cha matumaini.

03 May 2021, 16:02