Tafuta

2021.05.05 Katekesi ya Papa 2021.05.05 Katekesi ya Papa  

Papa Francisko:Sala ya moyo ni pumzi ya uhusiano wa mtu na Mungu

Wakati wa katekesi ya Papa Francisko ameendeleza sala na kujikita kufafanua juu ya taamuli,kwamba sala ya moyo ni kama pumzi ya uhusiano wa binadamu na Mungu.Katika Injili upo wito mmoja msingi wa kumfuata Yesu katika njia ya upendo.Matendo ya dhati na taamuli ni kitu kimoja.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko kwenye mwendelezo wa sala na ambapo Jumatano tarehe 5 Mei 2021, amejikita kufafanua taamuli au sala ya moyo kwa lugha nyingine kutafakari. Papa amesema: Kipimo cha taamuli cha mwanadamu na ambacho bado sio sala ya moyo ni kama vile chumvi ya maisha kidogo ambayo inatoa ladha, yaani ladha kwa siku zetu. Unaweza kutafakari kwa kutazama jua linalochomoza asubuhi, au miti ambayo inakuwa kijani wakati wa kipindi cha kuchanua, unaweza kutafakari kwa kusikiliza muziki au wimbo wa ndege, kusoma kitabu, mbele ya kazi ya sanaa au kito ambacho ni uso wa mwanadamu. Carlo Maria Martini, aliyekuwa ametumwa kama Askofu wa Milano, aliita barua yake ya kwanza ya kichungaji “Kipimo cha kutafakari cha maisha”: kitu kweli, wale ambao wanaishi katika jiji kubwa, ambapo kila kitu, tunaweza kusema ni bandia na, ambapo kila kitu kinafanya kazi, huhatarisha kupoteza uwezo wa kutafakari. Kutaafakari awali ya yote sio njia ya kwanza ya kufanya, bali  ni njia ya kuwa yaani ya kutafakari.

Papa amesema kuwa kufanya sala ya moyo haitegemei macho, bali moyo. Na hapa ndipo sala inatumika, kama tendo la imani na upendo, kama pumzi ya uhusiano wetu na Mungu. Sala hutakasa moyo  na, pamoja nayo, pia huangaza mtazamo, ukituwezesha kufahamu ukweli kutoka upande mwingine. Katekisimu inaelezea mabadiliko haya ya moyo kutokana na sala, ikinukuu ushuhuda maarufu kutoka kwa Mtakatifu wa Ars, alisema: “Taamuli ni mtazamo wa imani inayomkazia macho Yesu. Ninamtazama na Yeye ananitazama” ndivyo alikuwa anasema Mtakatifu mkulima wa Ars wakati akisali  mbele ya Tabernakulo. […]. Nuru ya mtazamo wa Yesu inaangazia macho ya moyo wetu, anatufundisha kutazama yote katika mwanga wa ukweli wake na huruma kwa ajili ya watu wote ( KKK 2715). Yote hayo yanazaliwa hapo kutoka katika moyo ambao unahisi kutazamwa kwa upendo. Kwa maana hiyo hali halisi inatafakariwa kwa mtazamo tofauti. Ninamtazama na  Yeye ananitazama.

Ndiyo hivyo katika taamuli ya upendo,  ni tabia ya sala ya kina, haina haja ya maneno mengi. Inatosha mtazamo, inatosha kuamini kwamba maisha yamezungukwa na upendo mkubwa na mwaminifu ambapo hakuna lolote linaweza kutengenisha katu. Yesu alikuwa mwalimu wa mtazamo huo. Katika maisha yote hakukosa nyakati , nafasi, ukimya, muungano wa upendo ambao unaruhusu kuishi na ili usizingirwe ndani ya majaribu yasiyokosekana, bali kuweza kuhifadhi kwa kina ule uzuri. Siri yake ilikuwa ni uhusiano na Baba wa Mbinguni. Papa Francisko kwa kutoa mfano amekumbusha tukio la Yesu kung’ara sura. Katika Injili zinaonesha tukio hilo katika wakati mgumu wa utume wa Yesu, mahali ambapo alizungukwa  na kuongezeka kwa vipingamizi  na kukataliwa.

Hadi wafuasi wale wengi hawakumuelewa na wakaondoka; mmoja wa tenashara, akaibua wazo la kumsaliti. Yesu alianza kuzungumza wazo juu ya mateso na kifo ambacho kilikuwa kinamsubiri huku Yerusalemu. Ni katika mantiki hiyo ambapo Yesu alipanda juu ya mlimamrefu faragahani  akiwa na Pietro, Yakobo na Yohane. Injili ya Marko inasema “ akageuka sura yake mbele yao; mavazi yake yakimeta-meta, meupe mno, jinsi asivyoweza dobi yoyote duniani kuyafanya meupe hivyo (Mk 9,2-3). Kwa hakika katika wakati ambapo Yesu hakueleweka, na wakati kila kitu kinaonekana kufifia katika njia ya kutokuelewana, hapo ndipo taa ya kimungu inang'aa. Ni nuru ya pendo la Baba, ambalo hujaza moyo wa Mwana na kubadilisha sura ya Mtu mzima.

Baadhi ya walimu wa masuala ya  kiroho wa zamani walielezea kutafakari tofauti na matendo, na waliibua miito hiyo inayokimbia ulimwengu na shida zake ili kujitoa kabisa kwa ajili ya maombi. Kiukweli, ndani ya Yesu Kristo katika nafsi yake na katika Injili hakuna tofauti kati ya sala ya kiroho na kutenda, hapana. Katika Injili ndani ya Yesu hakuna ubishi. Inawezekana mawazo hayo yalitokana na  ushawishi wa mwanafalsafa wa Kineoplatonic lakini kwa hakika hizo ni imani mbili ambazo sio za ujumbe wa Kikristo.

Kuna wito mmoja mkuu katika Injili na huo ni kumfuata Yesu kwenye njia ya upendo. Hii ndiyo kilele na ndiyo kitovu cha kila kitu. Kwa maana hii, upendo na taamuli au sala ya kiroho ni sawa, vinasema kitu kimoja. Mtakatifu Yohane wa Msalaba alisema kuwa kitendo kidogo cha upendo safi ni muhimu sana kwa Kanisa kuliko kazi nyingine zote zilizowekwa pamoja. Kwa maana ya kwamba kinachotokana na sala na sio kutoka atika dhana ya nafsi yetu, kile kinachosafishwa na unyenyekevu, hata ikiwa ni kitendo cha upendo wa faragha na kimya, ndio muujiza mkubwa zaidi ambao Mkristo anaweza kuufikia. Na hii ndiyo njia ya sala ya kutafakari kwa moyo: na tazama, ananitazama! Kitendo hiki cha upendo katika mazungumzo ya ukimya na Yesu hufanya vizuri sana kwa Kanisa.

05 May 2021, 16:00

Mikutano ya Baba Mtakatifu kwa siku za hivi karibuni

Soma yote >