Pope Francisko akutana na  wanafunzi wa Codogno,Italia Pope Francisko akutana na wanafunzi wa Codogno,Italia 

Papa akutana na wanafunzi wa Codogno:Shule ni mahali pa urafiki

Papa Francisko amekutana na baadhi ya wanafunzi kutoka Taasisi ya Ufundi ya Ambrosoli wa Mkoa wa Lombardia Italia,mahali walipogundua kesi ya kwanza ya Covid-19,.Papa amewakumbusha kuwa shule ni mahali pa kugeuka kuwa wazalendo wenye uelewa na uwajibikaji na kuishi urafiki wa kweli na si wa kidigitali.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Jumamos tarehe 232 Mei 2021, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wakuu na wanafunzi wa Taasisi ya Ambrosoli ya Codogno Italia, ni kutoka katika Mkowa wa Lombardia ambao kwa mara ya kwanza waligundua kesi ya kwanza ya Covid-19.  Mkutano wao ulikuwa ufanyike mwezi Februari iliyopita katika maadhimisho ya mwaka wa kuanza wa Janga la virusi barani Ulaya na hasa katika mji wa Codogno. Walipotoa pendekezo lao, alikuwa ameona kuwa ni muhimu kuwapokea kwa sababu shule yao katika muktadha wa jaribio gumu, inawakilisha ishara ya matumaini. Papa amesema awali ya yote kwa sababu shuleni ni mahali pa kuelimisha …. Pili kwa sababu ni taasisi ya ufundi wa utaalam, mahalia ambapo ni kujiandaa na kazi hasa ajira ambayo ni moja yenye kuwa na waathiriwa wengi kutokana na janga hili. Kwa maana

Katika miezi hii habari ni ambali mbali mbali zimefika za uzoefu chanya walizoishi makundi ya walimu, na wanafunzi Italia na katika nchi nyingine. Uzoefu ambao umejionesha kuwa kizazi kinapokutana na walimu na ndoto za wanafunzi hakuna virusi ambavyo vinaweza kuwasimamisha. Vijana wa kike na kiume wana nguvu, shauku ambazo chachu kwa kusinidikizwa na heima ya watu wazima na ili kuweza kutoa matunda ya kushangaza. Kwa kunuu mkuu wa taasisi hiyo alivyosema kuwa kuna haja ya wakufunzi ambao wawe walimu wenye maana kuu ni muhimu kutumia kichwa, akili na mikono. Lakini pia kuna jambo moja ambalo ni muhimu ambalo ni moyo, papa amesisitiza. Mambo haya matatu lazima yanaendane pamoja katika shule kama yanavyosukana katika maisha. Kichwa, moyo na mikono ni mzunguko daima wa kuzingatia na mwanenendo: “Moja inakosekana: moyo wako. Lugha tatu: ile ya kichwa,  ya moyo na ya mikono. Kufikia ule mshikamano ambapo mtu anafikiria kile anachosikia na kufanya, mtu husikia kile anachofikiria na kufanya, mtu hufanya kile anachohisi na anafikiria. Huo ndiyo uthabiti...” Uhusiano kati ya wanafunzi hata na walimu umekuwa mgumu kwa miezi ya mtaala wa shule lakini sasa Papa amewatika matashi mema wanapoanza tena.

Papa aidha hakukosa kuelezea juu ya mitandao ya kijamii na kusema kuwa, vijana kwa sasa ni watoto wa jamii ya kidigitali ambao imefungliwa katika njia mpya za ufahamu na katika mawasiliano, lakini  amebainisha kuwa tunatambua vema kuna hata hatari za kujifungia binafsi, na kuona hali halisi inazidi  kupitishwa na chujio ya ujuu ujuu wa kukuza uhuru wetu. Uzoefu wa janga la katika suala la uhusiano wa kiurafiki, unaweza kutoa chachu kwao ambao sasa wameelewa, kwa kiasi kikubwa ule ugumu katika matumizi ya zana za umbali, ambazo zinapaswa  hata hivyo kutumiwa kwa uangalifu wa  akili na utashi. Papa amesema: "Na jambo lingine ninalotaka kuwambia: “kwa hakika ninyi mmesikia mara nyingi wanasema kuwa lazima tuwatunze vijana kwa sababu wao ni siku zijazo. Hapana,  kwa sababu ninyi ni wa wakati wa sasa. Mtakuwa wa wakati ujao ikiwa mtakuwa wa wakati wa sasa. Ninyi ni wakati uliopo wa jamii. Bila vijana, jamii karibu imekufa. Ninyi ni wa wakatu uliopo kwa sababu mnaleta mambo mapya. Msisahau hilo”.

Papa Francisko amehitimisha kwa kuwatakia mema katika kufunga mwaka wa shule na si kupata matokeo mazuri lakini kwa ajili ya nyuso zao. Kila mmoja aweze kuhisi ishara na shauku, kumshukuru Mungu kwa ajili ya fursa waliyo nayo ya shule, mahali pa kukuza akili, mikono na moyo, mahali pa kujifunza kuishi kuwa na uhusiano ulio wazi, wa heshima, wa ujenzi; mahali pa kuwa wazalendo wenye kuwa na uelewa na uwajibikaji.

22 May 2021, 15:44