MKUTANO WA XXVII HUKO WA IBEROAMERICAN MKUTANO WA XXVII HUKO WA IBEROAMERICAN 

Papa Francisko:Ulinzi wa maisha ni kipaumbele kuliko mafao ya kiuchumi!

Katika ujumbe kwa washiriki wa Mkutano wa XXVII wa wakuu wa Ibero-American huko Handora,unaangazia dharura zinazosababishwa na virusi vya corona.Baba Mtakatifu anakumbuka waathiriwa na mamilioni ya walioambukizwa.Amelezea wasi wasi na matokeo ya janga hilo juu ya vijana.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika ujumbe kwa ajili ya  Mkutano wa XXVII Ibero-American, ulioelekezwa kwa katibu mkuu, Bi Rebeca Grynspan Mayufis, Papa Francisko anafuatilia dharura zote zilizosababishwa  na janga la sasa hasa katika eneo la Amerika Kusini. Mkutano huo unajumuisha nchi 22, wakiwemo wawakilishi wa kudumu wa Vatican tisa. Kwa wote Papa anawakumbusha kila mtu muktadha mgumu hasa kutokana na athari mbaya za janga la Covid-19 katika maeneo yote ya maisha ya kila siku. Kwa maana hiyo ni mwaliko wa  Papa Francisko, ili jumuiya  yote ya kimataifa ijitoe, iwe na umoja, na roho ya uwajibikaji na udugu, katika kukabili changamoto nyingi ambazo zinaendelea, na zile zitakazokuja .

Papa Francisko katika ujube huo anakumbuka mamilioni ya waathiriwa na watu wagonjwa. “Janga hili halijatofautisha na limeathiri watu wa tamaduni zote, imani, matabaka ya kijamii na kiuchumi, ameandika na, ambaye pia ameelezea ufahamu wa familia za walioambukizwa. “sisi sote tunajua na tumepoteza mpendwa mmoja aliyekufa na virusii vya corona au ambaye alipata athari za maambukizo hayo. Sisi sote tunafahamu jinsi ilivyo ngumu kwa familia kutoweza kusimama karibu na marafiki au jamaa zao kuwapa ukaribu na faraja katika nyakati hizi. Sote tumeona athari ya hali hii mbaya inawaathiri watoto na vijana wengi na tunafuatilia kwa wasiwasi matokeo ambayo yanaweza kuwa nayo kwa maisha yao ya baadaye”.

Papa Francisko  wazo lake  namna fulani limewaendea madaktari, wauguzi, wafanyakazi wa afya, wapadre wa vikanisa vya hospitali  na  watu wa kujitolea kwa kazi ngumu ambayo, pamoja na kutibu wagonjwa, imewaweka hatari ya maisha yao: “Walikuwa wanafamilia na rafiki waliyemkosa”.  Vile vile  Papa Francisko katika ujumbe huo  ana utambuzi wa juhudi zilizofanywa katika kutafuta chanjo inayofaa ya ajili ya Covid-19 kwa kipindi cha muda mfupi. Papa hata hivyo amesema: “Chanjo inapaswa kuzingatiwa kama faida ya kwa ajili ya watu wote ulimwenguni”. Vile vila Papa katika ujumbe huo ni matumaini yake kwamba inawezekana kuunda mtindo mpya zaidi na zaidi wa mshikamano. Katika eneo hili, mipango ambayo inataka kuundwa ya aina mpya mshikamano inakaribishwa lakini kwa kulenga kuhakikisha usambazaji sawa wa chanjo na sio kwa kuzingatia vigezo vya kiuchumi tu, lakini pia kwa kuzingatia ya mahitaji ya kila mtu, hasa walio hatarini zaidi na wahitaji”.

Papa Francisko amesema kuwa mgogoro wa sasa, uwe ni fursa nzuri ya kutafakari tena ule uhusiano kati ya mtu na uchumi, ili kusaidia kushinda njia fupi ya kifo ambacho kinaishi kila mahali na kila wakati. Ili kufikia ufnisi huo, amesisitiza kuwa ni lazima kuunganisha juhudi ili kuunda upeo mpya wa matarajio ambayo lengo kuu sio kutafuta faida za kiuchumi, badala yake ni kuwa na  ulinzi wa maisha ya mwanadamu. Kwa maana hii, ni muhimu kuzingatia mfano wa kupona unaoweza kutengeneza suluhisho mpya, zinazojumuisha zaidi na endelevu, zinazolenga faida ya wote, na  kutambua ahadi ya Mungu kwa watu wote.

Papa aidha ametazama hali halisi za nchi zilizo katika mazingira magumu zaidi. Hasa kwa kuzingatia hitaji la kurekebisha deni la kimataifa, ambalo lazima lichukuliwe, kama sehemu muhimu ya jibu letu la kawaida kwa janga hili, kwani kujadiliwa tena kwa mzigo wa madeni ya nchi maskini zaidi ni ishara ambayo isaidie watu ili kukuza, kupata chanjo, afya, elimu na ajira. Ishara hii lazima iambatane na utekelezaji wa sera thabiti za uchumi na utawala bora ambao unafikia maskini zaidi. Na kwa kuhitimisha Papa Francisko ametoa ushauri kwa nchi zote ili kuonesha mshikamano zaidi kupitia mipango ambayo inahimiza maendeleo ya kiuchumi na uzalishaji, ili kila mtu aweze kutoka katika hali ya sasa na nafasi nzuri ya kupona. Ujumbe wa Papa amewaomba  sana viongozi wa kisiasa: “Hakuna jambo hili litakalo wezekana bila kuwa na utashi wa kisiasa ambao kweli una ujasiri wa kuamua ili kubadilisha mambo, hasa kutoa vipaumbele na ili maskini wasiwe ambao wanalipa bei kubwa kwa mikasa hii ambayo inaathiri familia yetu ya wanadamu".

21 April 2021, 17:29