Papa katika siku ya Mama Dunia:Ni wakati wa kutenda kwa dhati!

Katika ujumbe kwa njia ya video katika fursa ya siku ya kimataifa ya Mama Dunia,Papa amesisitizia mgogoro wa Janga la Covid-19 uliounganishwa na mazingira kwa binadamu umefikia ukomo.Ni wakati wa kutenda kwa dhati.Papa anatoa wito wa umoja kuthibiti na maombi yake kwa viongozi wa ulimwengu watende kwa ujasiri na ukweli.Anawatia moyo Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi ulioandaliwa na rais Biden pia ametoa salamu fupi.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Hatuna muda mwingine wa kusubiri, kwani majanga mawili ya kidunia yanajionesha: mabadiliko ya tabianchi na Covid. Ndivyo yamesikika maneno ya Papa Francisko kwa lugha ya kispanyola kwa njia ya video katika siku ya Mama Dunia “Earth Day 2021”, tarehe 22 Aprili ambayo inaongozwa na kauli mbiu “Restore Our Earth”,  Siku ya “Rejesha Dunia yetu”. Katika ujumbe wake Papa Francisko anawaalika wote kuwa na matendo ya dhati ya kutunza kazi ya uumbaji, akikumbusha jinsi ambavyo mgogoro huu hauwezi kutufanya tuondokane nao tukiwa tunafanana tulivyokuwa awali, bali tunaitwa kuwa bora zaidi au itakuwa mbaya zaidi. Ujumbe kwa  njia ya video wa Baba Mtakatifu umeanza na kutoa wito hasa kutoruhusu mapendekezo muhimu ya ulinzi wa sayari kuanguka. Kwa muda fulani tumeanza kujua zaidi kuwa maumbile yanastahili kulindwa, na  kwamba mwingiliano wa kibinadamu na bioanuwai ya Mungu lazima ufanyike kwa umakini na heshima kubwa ya  utunzaji wa bioanuwai, na  utunzaji wa asili amesisitiza Papa.

Hizi ndizo nyanja ambazo pamoja na janga tumejifunza zaidi na zaidi. Papa pia amezungumzia kile kilichotokea wakati, wa karantini, kicuizi cha kipekee kwa mujibu wa kanuni za serikali za kitaifa kwa ajili ya dharura ya kiafya, kwamba ulimwengu ulibadilika kwa kasi. Janga hili pia limetuonesha kile kilichotokea wakati ulimwengu ukisimama, hata ikiwa kwa miezi michache tu. Athari  juu ya hali ya asili na mabadiliko ya tabianchi kwa nguvu, ni kwa njia ya kusikitisha kuwa chanya  au sio? Ni swali la Papa. Hali hiyo inahitaji hatua ya wakati unaofaa, isiyo ya kuahirishwa. Kwa maana hiyo Papa anafikia kitovu cha ujumbe wake kwa njia ya video. Kwa ufupi, janga la Covid limetufundisha utegemezi huu na ushirikishwaji huu wa sayari. Na majanga ya ulimwengu, Covid na hali ya hewa, yanaonesha kuwa hatuna muda wa kungojea. Wakati huo amesisitiza zaidi kwamba, kama Covid-19 inatakiwa kuwa na zana ya kukabiliana na ndiyo njia ya kuweza kushinda mahangaiko. Njia zipo Papa amebanisha na hivyo ni wakati wa kuchukua hatua, kwa maana tuko kwenye ukomo!

Papa Francisko akiendelea kwa maana hiyo amekumbuka msemo wa kizamani wa kispanyola akiwaalika watu kuchukua hatua pamoja, hasa kwa kuchochewa na uharaka na tayari kuanza njia mpya za ubunifu. “Mungu husamehe kila wakati, ila sisi wanadamu tunasamehe kidogo, na maumbile hayasamehi tena”, amesema. “Na wakati uharibifu huu wa asili unasababishwa, ni ngumu sana kuuzuia. Lakini bado tuna wakati”. Kwa maana hiyo ni mwaliko wa “kutoka katika mgogoro huo kwa ubora: “Mgogoro hatutoia tukiwa  sawa, tutatoka bora au mbaya zaidi. Hii ndio changamoto, na ikiwa hatutoki bora tunapitia njia ya kujiangamiza” . Ubinadamu unaweza, kubadilisha mwendo wa matukio kwa kulinda kazi ya Uumbaji. Ni wito kwa kwa viongozi wa ulimwengu ambapo Papa amesema: “Wote na mimi pia tuungane nanyi, tuwasihi viongozi wote wa ulimwengu kutenda kwa ujasiri, kufanya kazi kwa haki na kusema ukweli kila wakati kwa watu, ili watu wajue jinsi ya kujilinda kutokana na uharibifu wa sayari, jinsi ya kulinda sayari kutokana na uharibifu mara nyingi tunazochochea”.

Papa Fransisko ametoa wito wa uthabiti na ili wasishike njia ya kujiangamiza, lakini kwa kufanya kazi kwa ujasiri na umoja kuunda sayari ya haki, usawa na salama kwa mtazamo wa mazingira. Katika salamu fupi, kwa lugha ya kispanyola ameageukia washiriki wa  Mkutano wa viongozi wa ulimwengu juu ya mabadiliko ya tabiachi, ulioandaliwa na utawala wa Biden, katika afla ya Siku ya Mama Dunia. Papa Francisko amekumbusha kwamba mpango huo unatuweka wote katika safari ya kuelekea katika kilele cha mkutano  wa Glasgow ,lakini kabla ni busara zaidi kuchukua jukumu la utunzaji wa asili ya uumbaji, ambayo ni zawadi tuliyoipokea  na kwamba lazima tuitunze, na tuendeleze mbele. Ni changamoto ambayo inachukua umuhimu mkubwa sana hasa wakati wa magonjwa ya milipuko, ambayo tunaweza kuwa bora au kuwa mbaya zaidi. Wasiwasi wetu Papa amehitimisha  “ni kuona kuwa mazingira yanakuwa safi, yanatakata  na kwamba yanahifadhiwa ipaswavyo. Na kutunza maumbile ya dunia ni kwa sababu yaweze  kututunza hata sisi”.

Kwa kuanzisha mnamno tarehe 22 Aprili 1970 huko Marekani, Siku ya  Mama Dunia kila mwaka hutuma ujumbe ulio wazi ili kuishi kwenye sayari yenye afya kwamba  ni haki ya wakazi wote, lakini pia ni wajibu. Uendelevu, vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, uhifadhi wa bioanuwai, vita dhidi ya uchafuzi wa mazingira na ulinzi wa mifumo ya ekolojia ndio nguzo za mpango huu mkubwa wa ulimwengu, ulioanzishwa miaka 51 iliyopita. Hapo awali iliadhimishwa ulimwenguni kila baada ya miaka kumi, lakini baadaye tangu toleo la 2000 ikawa hafla ya kila mwaka inayoweza kuhusisha watu wapatao bilioni kupitia mipango, pamoja na ile ya kweli, kwenye mtandao wa kijamii katika Tovuti: earthday.org.  Mada kuu ya Siku ya Dunia 2021 ni “Rejesha Dunia Yetu”, iliyotolewa kwa mipango ambayo kila mmoja wetu anaweza kufanya kurejesha mazingira ya Dunia kuwa bora zadia kwa afya yetu sote.

23 April 2021, 09:42