Tafuta

Papa Francisko:Mt.Adalberto alikuwa mtu wa imani,sala na nguvu!

Papa akikumbusha siku kuu ya mfiadini na msimamizi wa nchi ya Poland,Askofu Adalberto ambaye alikuwa ni mtu wa imani ya kina,sala na nguvu, ufiadini wake ukawa ndiyo mwanzo wa utambulisho wa Kanisa hilo.Kwa lugha ya kiitaliano:kipindi cha Pasaka ambacho bado tunaendelea kukiishi,kisaidie ndani mwetu roho Mtakatifu ili kuishi maisha mapya yaliyojaa upendo na shauku.Amekumbua wazee,vijana,wagonjwa na wenye ndoa wapya.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Mara baada ya katekesi yake, Jumatano tarehe 21 Aprili 2021 akiwa katika Maktaba ya Jumba la kitume Vatican, Papa Francisko ametoa salamu mbali mbali kwa lugha tofauti, kwa lugha ya kipoland, Papa Francisko amekumbusha siku kuu ya Mtakatifu Adalberto, Askofu na shahidi ambaye ni msimamizi wa chi ya Poland, inyaoadhimishwa kila tarehe 23 Aprili. Alikuwa ni mtu wa imani ya kina, sala na nguvu, ufiadini wake ukawa ndiyo mwanzo wa utambulisho wa Kanisa nchini Poland. Kwa maombezi yake kwa Mungu wao waweze kupata ujasiri katika imani, na kukua kibinadamu, kijamii na kiroho katika nchi yao. Papa amewabariki kwa moyo wote.

kwa lugha ya kiitaliano amesema kipindi cha Pasaka ambacho bado tunaendelea kukiishi, kisaidie kuzaa ndani mwetu roho Mtakatifu ili kuishi maisha mapya yaliyojaa upendo na shauku. Wazo lake kama kawaida ni kwa ajili ya wazee, vijana, wagonjwa na wanandoa wapya. Papa amesema kuwa katika kipindi hiki cha Pasaka, amewaalikwa kutafakari fumbo la Ufufuko wa Kristo ambaye utukufu wa Bwana unaweza kuwa kwa kila mmoja chemi chemi mpya ya nguvu katika safari kuelekea wokovu.

Kwa upande wa lugha ya kiarabu, Papa amesema wasiogope ikiwa neema ya sala utafikiri inaishia gizani, badala yake ni kuelendelea kusali hata kwa sala rahisi ya kikristo, ili iwe sehemu ya pumzi ya maisha ambayo inatufanya tuone uwepo wa Ufalme wa Mungu, hapa, na kati yetu. “Bwana awabariki nyote na awalinde kila wakati dhidi ya maovu yote!

Na katika ujumbe mfupi Papa Francisko kwa njia ya mtandao wa kijamii hasa katika siku ambayo katekesi yake amejikita kwenye sala ya sauti amesema “Tusiache sala rahisi ambazo tulijifunza tukiwa wadogo ndani ya familia na ambazo zinahifadhi kumbu kumbu na katika moyo. Ndiyo njia hakika ya kuweza kufika katika moyo wa Mungu.

21 April 2021, 16:02