Tafuta

2021.04.21 Katekesi ya Papa Francisko katika Maktaba ya Jumba la Kitume 2021.04.21 Katekesi ya Papa Francisko katika Maktaba ya Jumba la Kitume 

Papa Francisko.Hakuna anayezaliwa akiwa mtakatifu!

Katika katekesi ya Papa Francisko Jumatano tarehe 21 Aprili,ametafakari thamani ya sala ya sauti ambayo inazaliwa midomoni na kukumbusha kuwa maneno tunayotamka ndiyo pekee yanayokwenda kwa Munguna maswali ambayo Mungu anataka kusikiliza.Kila kiumbe kwa namna fulani anazungumza na Mungu,kwa sauti maneno,maombi wimbo na shairi.Na ni sala ya watu rahisi ya Baba Yetu tuliyofundishwa na Yesu mwenyewe.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika mwendelezo wa mada ya sala katika katekesi za Baba Mtakatifu Francisko, akiwa Maktaba ya Jumb la kitume, Jumatano tarehe 21 Aprili 2021 amejikita kufafanua kuhusu sala ya sauti. Akianza tafakari hiyo amesema: “Sala na mazungumzo na Mungu; na kila kiumbe kwa namna fulani anazungumza na Mungu. Kwa mwanadamu, sala ya sauti inageuka kuwa neno, maombi, wimbo, shairi… Neno linakuwa Mungu aliyejifanya mwili na katika mwili kila mtu, neno linarudi kwa Mungu katika maombi…  Maneno ndiyo uumbwaji wetu, lakini pia ni mama zetu, na kwa kipimo kingine yanatuunda”.  Papa Francisko amesema, “Maneno katika sala yanatufanya tukatishe hatari bila kuwa na uwanda mweusi, kwani katika malisho ya majani mabichi hutulaza, kando ya maji ya utulivu utuongoza. Na kutuandalia meza mbele yetu, machoni pa watesi wetu. Kama tunavyofundishwa kusali katika Zaburi ya 23. Maneno yanazaliwa kutokana na hisia lakini ambazo ni mchakato ulio kinyume cha safari, ambayo maneno uunda hisia hizo. Biblia inafundisha ili kila kitu kiweze kuonekana katika mwanga wa neno na hakika mtu hasibaguliwe au kukaguliwa. Hasa uchungu ni hatari ikiwa unabaki umefunikwa, yaani umefungwa ndani mwetu… Maumivu yaliyofungwa ndani yetu, ambayo hayawezi kujielezea au kutoa hewa, yanaweza kusababisha sumu ya roho. Ni mbaya ya kufa.

Maandiko matakatifu yatufundisha kusa kwa maneno na shauku

Kwa maana hiyo Maandiko matakatifu yanatufundisha kusali hata kwa maneno na hadi shauku. Waandishi wa maandiko matakatifu hawataki kukatisha tamaa mwanadamu. Wanatambua kuwa mwoyoni mwake zinakaa hata hisia zisizojenga, hadi kufikia chuki. Akuna hata mmoja anayezaliwa mtakatifu, na ikiwa hisia hizi mbaya zinabisha mlangoni mwa mioyo yetu lazima kuwa na  uwezo wa kuzifukuza kwa sala na kwa maneno ya Mungu. Katika zaburi tunapata hata vielezo vingi dhidi ya maadui, vilelezo hata vya walimu wa kiroho vinatufundisha juu ya  ibilisi na dhambi zetu; na wakati huo huo ni maneno ya hali halisi ya mwanadamu ambayo yameishia katika mzunguko wa Maandiko matakatifu. Wapo pale wanashuhudia. Sala ya kwanza ya binadamu daima ni ya sauti. Awali ya yote ni midomo inayotingishika.

Kusali siyo kurudia maneno lakini ni njia daima ya kusali

Hata kama sisi sote tunatambua kuwa kusali maana yake siyo kurudia maneno, walakini sala ya sauti ni ya uhakika zaidi na daima inawezekana kuisali. Hisia kinyume chake, hata kama ni neema daima haina uhakika: zinakwenda na kurudi, zinatuacha na kurudi tena. Si hiyo tu hata neema za sala hazitabiriki. wakati mwingine faraja ni nyingi, lakini wakati mwingine ni giza utafikiri zimeyeyuka zote. Sala ya moyo ni fumbo na uhakika, katika wakati fulani haipo. Sala ya midomo, ile ambayo inanong'onezwa au kusomwa kwenye kwaya, inapatikana kila wakati, na inahitajika kama kazi ya mikono. Katika Katekisimu ya Kanisa Katoliki inatufundisha juu ya hili na kuthibititisha kuwa: “sala ya sauti ni sehemu ya lazima ya maisha ya kikristo.  Wafuasi waliovutwa na sala ya kimya ya Mwalimu wao, hawa aliwafundisha sala ya sauti, kusema Baba yetu’ (KKK, 2701)”. Wafuasi waliomba Yesu “ tufundishe kusali na Yesu anatufundisha hata sisi sala ya sauti: Baba yetu. Na hapo kuna kila kitu katika sala hiyo, …Papa amesisitiza.

Kuwa wanyenyekevu kama wazee wanaosali kwa minong’ono

Papa Francisko akiendelea na tafakari kuhusu sala ya sauti amesema kuwa sisi sote tunapaswa kuwa na unyenyekevu kama wazee ambao katika Kanisa labda kwa sababu masikio yao hayasikii vema, wanasali kwa sauti ndogo zile sala ambazo walijifunza wakiwa wadogo, kwa kujazwa hivi na minong'ono. Ile sala haisumbui ukimya, bali ushuhudia imani ya kuweza kuabudu, kufanya mazoezi katika maisha yote, bila kuchelea kamwe. Waombaji hawa katika sala ya unyenyekevu mara nyingi ni waombezi wakuu wa maparokia. Wao ni mialoni ambayo kila mwaka hupanua matawi yao, hutoa kivuli kwa idadi kubwa ya watu. Ni Mungu tu anayejua ni lini na kwa kiasi gani mioyo yao ilikuwa imeungana na maombi hayo yaliyosemwa. Kwa hakika watu hawa pia walilazimika kukabiliana na  usiku na vipindi vya utupu. Lakini kwa sala ya sauti inawezekana kubaki mwaminifu. Ni kama nanga, inayoshikamana na kamba ili kukaa hapo, mwaminifu, pitisha chochote kinachopita na chochote kitakachotokea!

Tujifunze kwa msafiri wa kirusi Yesu “Kristo mwana wa Mungu tuhurumie”

Papa Francisko kwa kutoa ushauri amesema kuwa, Sisi sote lazima tujifunze kutoka kwa uthabiti wa yule msafiri wa Kirusi, ambaye anazungumziwa juu ya kazi yake maarufu ya kiroho ambaye, alijifunza sanaa ya sala kwa kurudia ombi lile lile tena na tena “Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, Bwana utuhurumie sisi wadhambi” (KKK, 2616; 2667).  Alikuwa anarudia hilo tu, “Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, Bwana, utuhurumie sisi wadhambi”.  Ikiwa neema zitakuja katika maisha yake, ikiwa sala siku moja itakuwa ya moto wa kutosha kutambua uwepo wa Ufalme hapa kati yetu, ikiwa mtazamo  utabadilishwa kuwa kama wa mtoto, ni kwa sababu ya sala iliyo rahisi ya kikristo. Hatimaye, inakuwa sehemu ya pumzi yake. Historia ya msafiri wa Urusi ni nzuri: ni kitabu rahisi ambacho kwa kila mtu anaweza kukisoma, na kwa maana hiyo Papa Francisko amependekeza kukisoma kwani  amesema, kitatusaidia kuelewa ni nini maana ya sala ya sauti.

Tusianguke katika kiburi cha kudharau sala ya sauti

Papa Francisko amesema,   hatupaswi kudharau maombi ya sauti. Kwa kutoa mfano amesema “Mtu anasema: “Eh, ni kwa watoto, kwa watu wasiojua; Mimi ninatafuta sala ya kiakili, tafakari, utupu wa ndani ili Mungu aje… ”: ameongeza  tafadhali! msiiangukie katika kiburi cha kudharau sala ya sauti. Ni sala rahisi, ile ambayo Yesu alitufundisha: Baba yetu, uliye mbinguni ... Maneno tunayotamka yanachukuliwa kutoka mikononi mwetu ; wakati fulani hurejesha ladha, huamsha hata mioyo iliyo na usingizi zaidi; zinaamsha hisia ambazo tulikuwa tumepoteza kumbukumbu. Na maneno haya yanatuongoza kwa mkono kuelekea uzoefu wa Mungu ... Na juu ya yote, ni wao tu, kwa njia ya uhakika, ambao huelekeza maombi ambayo anataka kusikia Mungu. Yesu hakutuacha kwenye ukungu. Alisema kuwa “Ninyi msalipo mseme hivyo. Na alitufundisha kusali sala ya Baba Yetu (Mt 6,9). Papa Francisko amehimisha.

21 April 2021, 15:45

Mikutano ya Baba Mtakatifu kwa siku za hivi karibuni

Soma yote >