Tafuta

2021.04.11 Misa katika Kanisa la Roho Mtakatifu, Sassia, Jumapili ya Huruma ya Mungu. 2021.04.11 Misa katika Kanisa la Roho Mtakatifu, Sassia, Jumapili ya Huruma ya Mungu. 

Papa Francisko:Ishi imani kikamilifu siyo nusu nusu&unapokea utoe

Katika Dominika ya Huruma ya Mungu Papa Francisko katika mahubiri yake amewaalika waamini wasiangukie katika tabia za sintofahamu,bali kuishi kwa kushirikisha na kuinamia majerahaya wale wenye kuhitaji na ndipo watagundua maana na huruma ya Mungu.Waishi huruma ya Mungu kwa imani kikamilifu na si nusu nusu bali walichokirimiwa watoe kwa wengine

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika maadhimisho ya misa Takatifu Dominika ya Huruma ya Mungu, Papa Francisko ameongoza maadhimisho hayo katika Kanisa la Roho Mtakatifu, Sassia karibu na Vatican ambayo ni madhabahu ya Mungu tarehe 11 Aprili 2021. Akianza mahubiri yake Papa amesema, Yesu Kristo mfufuka aliwatokea wanafunzi mara nyingi. Kwa uvumilivu anawatuliza mioyo yao iliyokuwa imekata tamaa. Baada ya ufufuko wake, anafanya hivyo kwa ufufuko wa wafuasi wake. Na wao baada ya kuamshwa na Yesu, walibadilisha maisha. Kabla ya maneno mengi na mifano ya Bwana ilikuwa imefanya kazi ya kuwabadilisha. Sasa wakati wa Pasaka inatokea jambo jipya. Hii inakuja katika ishara ya huruma. Yesu anawaamsha kwa huruma. Yesu anatimiza hilo kwa hurumaNa wao kwa kuhurumiwa wanakuwa wenye huruma. Papa ameongeza kusema kuwa wakati mwingine ni vigumu kuwa na huruma hasa usipojigundua kuwa umehurumiwa. Awali ya yote walihurumiwa kwa njia ya zawadi tatu: Ya kwanza Yesu anatoa amani kwao, baadaye Roho na mwisho kwa majeraha. Kwanza Yesu  aliwapa amani kwa maana Mitume hao walikuwa na huzuni. Walikuwa wamefunga milango kwa hofu, kwa woga wa kukamatwa na kuishia kama Mwalimu wao. Hata hivyo hawakuwa wamejifungia nyumbani tu, walikuwa wamejifungia nyumbani kutokana na kujuta. Ni kutokana na kwamba walikuwa wamemwacha na kumkana Yesu. Walikuwa wanahisi kutokuwa na uwezo, kutokuwa wema, kwa maana waliokosea. Yesu alipofika alirudia mara mbili na kusema: “Amani iwe kwenu. Halileta amani ambayo iliondoa matatizo ya nje, lakini amani ambayo pia inaongeza imani ya ndani. Na siyo amani ya nje tu, lakini amani ya moyo!

Papa amesema, Yesu alisema “amani na iwe kwenu kama Baba alivyonituma nami ninawatuma ninyi” (Yh 20,21). Ni kama ambavyo angeweza kusema: “Ninawatuma kwa sababu ninawaamini! Mitume hao walikuwa wamekosa amani ndani mwao. Amani ya Yesu iliwaondolea majuto yale ya kutotimiza wajibu. Amani ya Yesu iliwafanya kutenda utume. Siyo utulivi na siyo kula raha bali ni  kuondoka ndani mwao binafsi. Amani ya Yesu inatoa uhuru dhidi ya kujifungua binafsi na kuganda, inavunja minyororo ambayo inafunga moyo. Na mitume walihisi kuhurumiwa. Walihisi kuwa Mungu hakuwahukumu, hakuwanyenyekeza, lakini aliwaaamini. Ndiyo yeye anatuamini zaidi ya kile ambacho sisi tunaamini binafsi. Anatupenda zaidi ya sisi tunavyojipenda.Kwa Mungu hakuna anayekosea, hakuna hasiye na faida, hakuna anayebaguliwa. Yesu leo hii anarudia tena “amani kwako, wewe uliye na thamani mbele ya macho yake. Amani wewe ambaye ni muhimu kwake. Amani kwako wewe uliye na utume. Hakuna anayeweza kushika nafasi yako. Huwezi kubadilishwa. Na anakuamini wewe”.

Katika hatua ya pili, Yesu wa huruma aliwapatia mitume Roho Mtakatifu. Aliwapatia kwa ajili ya kuondolea dhambi (Yh 20, 22- 23).  Mitume walikuwa na makosa, walikuwa wamekimbia na kumwacha Mwalimu. Ni dhambi iliyowatesa, ubaya una ghara zake. Dhambi zetu kama isemavyo Zaburi zipo mbele daima”. Peke yetu hatuwezi kuzifuta. Ni Mungu tu anayeweza kuzifuta, ni Yeye kwa huruma yake anatufaya tutoke katika maovu yetu ya kina. Kama mitume wale, nasi tunahitaji kuacha kusamehewa. Msamaha katika Roho Mtakatifu ni zawadi ya Pasaka kwa ajili ya kufufuka ndani. Tuombe neema ya kuipokea, kuikumbatia Sakramenti ya msamaha. Lazima kusema ndani ya moyo “ “Nisamehe Bwana, ni kufungua moyo ili aweze kusamehe”. Na kutambua kuwa kiini cha kitubio sisi hatupo peke yetu na dhambi zetu, bali na Mungu na msahama wake. Hatuungami ili kuanguke,  bali kwa ajili ya kuamka. Sisi sote tunahitaji sana. Tunahitaji kama watoto wadogo, mara zote wanapoanguka wanahitaji kuamshwa na baba. Hata sisi mara nyingi tunaanguka. Na mkono wa Baba huko tayari kutusimamisha na kutufanya kwenda mbele. Mkono huu wa hakika na kuamini ni kitubio.  Ni sakramenti ambayo inamsha na haituachi tubaki chini ya sakafu ngumu na madhaifu yetu. Ni sakramenti ya ufufuko, ni huruma safi. Na anayepokea kitubio lazima ahisi uzuri wa huruma. Hii ndiyo njia ya wale wanaowapokea watu kuungama. Kuwafanya wahisi ule uzuri wa huruma ya Yesu ambaye anasamehe yote. Mungu usamehe yote.

Baada ya amani inayokarabati na msamaha unaoleta faraja ndiyo zawadi ya tatu ya Yesu kwa huruma ya wanafunzi wake anawatoa majareha yake. Katika madonda yake sisi sote tumepona (taz 1 Pt 2,24; Is 53,5). Je majeraha yanaweza kutuponesha kwa namna gani? Swali la Papa. Kwa huruma. Katika majeraha yake, kama Tomasi tunagusa kwa mikono mikono yetu ya kwamba Mungu anatupenda kwa kina hadi mwisho, aliyefanya majeraha yetu kuwa yake, aliyebeba katika mwilini wake kwa ajili ya udhaifu wetu. Majareha ni mkondo iliofunguliwa kati yetu na sisi ambao unapitishwa huruma yake katika maovu yetu. Majaeraha ni njia ambazo Mungu ameziweka wazi kwa sababu sisi tupate kuingia katika huruma yake na kugusa kwa mkono kwa yule aliye wake. Na tusiwe na shaka zaidi ya huruma yake. Kwa kuabudu, na kwa kubusu majeraha yake tunagundua kuwa kila udhaifu wetu umepokelewa katika huruma yake. Hii inatokea kwa kila Misa, mahali ambapo Yesu anatoa mwili wake uliojaa majeraha na mfufuka. Tunamgusa na Yeye anagusa maisha yetu. Na anafanya kushuka kwetu Mbingu. Majereha yake angavu yalipasua giza ambalo tunalibeba ndani mwetu. Na sisi kama Tomasi, tunampata Mungu, tunamgundua ndani na karibu kwa hisia nzito tunasema “Bwana wangu, Mungu wangu” (Yh 20,28). Yote hayo yanazaliwa hapa, na neema ya kuwa tumehurumiwa. Kutoka hapa tunaanza safari ya kikristo. Ikiwa tunahesabu uwezo wetu, kujitosheleza na miundo yetu na mipango yetu, hatutakwenda mbali. Ni pale ambapo tutapokea upendo wa Mungu tu tutaweza kutoa chochote kipya katika ulimwengu.

Kwa maana hii walifanya utume waliohurumiwa, waligeuka kuwa wenye huruma. Tunawaona katika somola kwanza. Katika kitabu cha Matendo ya mitume kinasimulia kuwa “wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu chochote alichonacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika. (Mdo 4,32. Hii siyo ukomusiti ni ukristo ulio safi. Na inashangaza sana ikiwa tunafikiria kwamba mitume hao hao kabla walikuwa wamegombania juu ya zawadi na nafasi muhimu kwamba ni nani angeweza kuwa mkuu kati yao (taz Mk 10,37; Lk 22,24). Na sasa wanashirikishana kila kitu, walikuwa na moyo mmoja na roho moja (Mdo 4,32). Je walifanyaje kubadilika hivi? Waliona katika mwingine huruma ile ile ambayo iliyo wabadilisha maisha yao. Waligundia kuwa na utume mmoja, msamaha na Mwili wa Yesu. Kushirikisha mali za nchi zikawa matokeo ya kawada. Maandiko yanaeleza tena kuwa, Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji (Mdo 4,34). Hofu zao zilikuwa zimeyeyuka kwa kugusa majeraha ya Bwana, na sasa hawana hofu ya kutibu majeraha ya wenye kuhitaji. Kwa sababu pale wanamwona Yesu. Kwa sababu pale kuna Yesu. Majeraha ya yule.

Papa Francisko ameuliza swali: Je unataka kuhakikisha kuwa Mungu amegusa maisha yako. Hakikisha ikiwa unainamia madonda ya wengine. Leo hii ni siku ya kujiuliza. “Mimi ambaye nimepokea mara nyingi amani ya Mungu, msamaha wake, huruma yake, ninayo huruma kwa wengine? Mimi ambaye mara nyingi nimemwilishwa Mwili wake, ninafanya chochote kushibisha ambaye ni maskini? Tusibaki na sintofahamu. Tusiishi imani nusu ya anayepokea lakini hatoi, anayepokea zawadi lakini hajifanyi zawadi. Tulihurumiwa, tugeuke kuwa wenye huruma. Kwa sababu ikiwa upendo unaishia ndani mwetu tu, imani inakauka ndani bila kuzaa matunda, bila wengine haiwezi kuwa mwili. Bila kazi ya huruma inakufa (Yk 2,17). Tuuishe amani, kutoka na msamaha na majeraha ya Yesu wa huruma. Na tuombe neema ya kugeuka kuwa mashuhuda wa huruma. Ni kwa njia hiiyo tu imani itakuwa hai. Na maisha yanaunganika. Ni kwa njia hiyo tu tutatangaza Injili ya Mungu kwamba ni Injili ya huruma. Papa Francisko amehihitimisha na kukaa kimya kabla ya sala ya Nasadiki.

PAPA FRANCISKO DOMINIKA YA HURUMA

 

11 April 2021, 16:28

Sala ya Malkia wa Mbingu ni nini?
 

Utenzi wa Malkia wa Mbingu ni kati ya tenzi nne za Bikira Maria (nyingine ni:Tunakimbilia Ulinzi wako,  Salam Malkia wa Mbingu, Salam Malkia). Kunako mwaka 1742, Papa Benedikto XIV alipoandika kwamba, waamini wasali Sala ya Malkia wa Mbingu wakiwa wamesimama, kama alama ya ushindi dhidi ya kifo, wakati wa Kipindi cha Pasaka, yaani kuanzia Domenika ya Ufufuko wa Bwana hadi Sherehe ya Pentekoste. Hii ni Sala ambayo husaliwa mara tatu kwa siku kama ilivyo pia Sala ya Malaika wa Bwana: Asubuhi, Mchana na Jioni ili kuweka wakfu Siku kwa Mwenyezi Mungu na Bikira Maria.

Utenzi huu kadiri ya Mapokeo ulianza kutumika kunako karne ya VI au Karne X, lakini kuenea kwake kunaanza kujitokeza katika nyaraka mbali mbali kati kati ya Karne ya XIII, ilipoingizwa kwenye Kitabu cha Sala za Kanisa cha Wafranciskani. Hii ni Sala inayoundwa na maneno mafupi manne yanayohitimishwa na Alleluiya na sala ya waamini wanaomwelekea Bikira Maria, Malkia wa mbingu, ili kufurahia pamoja naye kuhusu Fumbo la Ufufuko wa Kristo Yesu.

Papa Francisko tarehe 6 Aprili 2015 wakati wa Sala ya Malkia wa Mbingu, siku moja baada ya Sherehe ya Pasaka, aliwashauri waamini kuwa na moyo wa furaha wanaposali sala hii. “Tunamwendea Bikira Maria, tukimwomba afurahi, kwa sababu yule Mwanaye mpendwa aliyekuwa amemchukua mimba amefufuka kweli kweli kama alivyosema; tunajiaminisha kwa sala na maombezi ya Bikira Maria. Kimsingi furaha yetu ni mwangi wa furaha ya Bikira Maria kwani ndiye aliyetunza na anaendelea kutunza matukio mbali mbali ya maisha ya Yesu. “Tusali sala hii kwa furaha ya kuwa waana wa Mungu ambao wanafurahi kwa sababu Mama yao anafurahi”

 

Sala ya Malaika wa Bwana/ Malkia wa Mbingu ya hivi karibuni

Soma yote >