2021.04.05 KARDINALI CHIRISTIAN TUMI 2021.04.05 KARDINALI CHIRISTIAN TUMI  

Papa akumbuka Kardinali Tumi kuwa na maisha ya amani na mapatano

Papa Francisko anakumbuka Kardinali Christian Wiyghan Tumi wa Camerun aliyeaga dunia siku ya Jumamosi Kuu Takatifu akiwa na umri wa miaka 90 katika salam zake za rambi rambi alizomtumia Askofu mkuu wa Douala kuwa alikuwa mtu anajikita katika misha ya amani na mapatano.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Kardinali Tumi ameacha ishara isiyosahulika katika Kanisa na katika maisha ya kijamii na kisiasa katika nchi yake, kwa jitihada zake daima na ujasiri katika ulinzi wa demokrasia na uhamasishaji wa haki. Ndivyo Papa Francisko anamkumbuka Kardinali ambaye alikuwa askofu wa Yagoua, na baadaye kuwa Askofu Mkuu wa Garoua na Douala, katika telegramu yake aliyo muelekeza Akofu Mkuu Samuel Kleda, wa jimbo kuu la Douala nchini Cameruni. Kardinali Tumi aliaga dunia mnamo Jumamosi Kuu Takatifu, tarehe 3 Aprili 2021 akiwa na umri wa miaka 90.

Katika salamu zake za rambi rambi, Papa Francisko anaandika kuwa “kwa kufahamishwa habari hizo na uchungu wa kifo cha kaka yetu, Kardinali Christian Tumi, ninatamani kutoa salamu zangu za rambi rambi na muungano wa sala na Baraza la Makardinali, kwa familia na ndugu za marehemu, hata wale wote wanaoomboleza kutokana na kuguswa na msiba huo”.

Kardinali Tumi alikuwa ni mtu wa Mungu katika huduma ya amani na ya haki. Papa Francisko ameongeza kuandika kwamba mara baada ya kufikia hatua yake ya uzee kwa kustaafu, lakini Kardinali Tumi alibaki akiwa na uwezekano wa kutoa huduma kwa ajili ya amani na mapatano. Papa anasisitiza kuwa baada ya kuchaguliwa kuwa Kardinali na Mtakatifu Yohane Paulo II mnamo 1988 alikuwa mwaminifu kwa kushirikiana na Mapapa katika kupokea majukumu mbali mbali ndani ya Kanisa la Roma.

Kwa maana hiyo, sala ya Papa ni kwamba “Bwana aweze kupokea roho ya Mtumishi wake katika amani na furaha! Na ishara ya kutiwa nguvu katika kipindi hiki cha Pasaka ni kuielekeza kwa Askofu Mkuu ambayo ni Baraka ya Kitume, pamoja na familia yote ya Mungu na wapendwa wa marehemu Kardinali, hasa wale ambao wameweza kumzuka katika miaka hii na wale wote ambao watashiriki na kwenye ibada ya mazishi katika matumaini ya ufufuko.

06 April 2021, 15:22