Madhabahu ya Mama Yetu wa Uchungu Kibeho, Rwanda Madhabahu ya Mama Yetu wa Uchungu Kibeho, Rwanda 

Madhabahu ulimwenguni kusali rosari mwezi Mei ili janga liishe

Kila siku saa 12 jioni kutakuwa na sala ya Rosari Takatifu kwa utashi wa Papa Francisko kwa mwezi Mei ambapo yeye mwenyew atafungua na sala mwanzoni na kufunga mwishoni mwa mwezi wa Rosari.Madhabahu therethini ulimwengu ya Mama Maria yatawakilisha kusali kila siku ili wawe wahamasishaji wa waamini,falilia na jumuiya zote kusali Rosari Takatifu

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Madhabahu thelathini, yanayowakilisha ulimwengu wote, yataongoza kusali  Rozari kila siku kwa mwezi Mei katika mbio ya maombi yanayoongozwa na kaulimbiu: “Kutoka Kanisa lote Maombi yalipaa kwenda  kwa Mungu”, ambalo ni  wazo la Papa Francisko na kuhamasishwa na  Baraza la Kipapa la Kuhamasisha uinjilishaji Mpya na tukio hilo  ambalo litawahusisha kwa namna ya pekee madhabahu yote ulimwenguni, ili wawe wahamasishaji wa waamini, familia na jumuiya zote kusali Rosari Takatifu

Siku ya kwanza ya mwezi Mei, Papa atafungua kwa sala na kufunga mwishoni

Sala ya Rosari itafunguliwa na Papa Francisko siku ya kwanza ya mwezi Mei, na pia kuhitimisha na yeye mwenyewe manmo tarehe 31 Mei 2021. Sala ya Rosari Takatifu hiyo itatangazwa moja kwa moja na majukwaa rasimi ya Vatican, kuanzia saa 12.00 jioni kila siku. Ikumbukwa kuwa tangu Jumatatu tarehe 17 Aprili, hadi Jumamosi saa 6.00 za kila siku, sala ya Rosari Takatifu imeanza kwa mara nyigine tena katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro  Vatica, ikiongozwa na Kardinali Angelo Comastri,  Makamu mstaafu wa Papa katika Mji wa Vatican na Paroko mstaafu wa Kanisa hilo Kuu.

Rosari takatifu wakati wa wimbi la janga mnamo Machi 2020

Kipindi hicho cha sala kilikuwa kimeanzishwa mnamo Machi 2020 ili uongeza matumaini  waamini na aenye mapenzi mema wakati wa mwanzo wa wimbi la janga ambalo hata leo hii bado linaendelea na ambapo sasa inawezekana kufuatilia moja kwa moja kupitia Tovuti ya Vatican News na Masafa ya Radio  Vatican, Italia.

21 April 2021, 17:11