2021.03.21 Sala ya Malaika wa Bwana 2021.03.21 Sala ya Malaika wa Bwana 

Papa Francisko:tuwe na shauku ya kumwona Yesu kuanzia na Msalaba

Papa Franciso wakati wa tafakari yake kabla ya salaya Malaika wa Bwana ameelekezea uwajibikaji mkubwa kwa wakristo wote na jumuiya kwamba lazima kujibu kwa ushuhuda wa maisha ambayo yanatoa huduma.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Dominika tarehe 21 Machi 2021, kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, Papa Francisko akiwa tena katika maktaba ya kitume, Vatican, kutokana na janga linaloendelea sasa la virusi ameanza na tafakari inayohusu siku hii kwa kusema! “Injili ya Dominika ya tano ya Kwaresima, katika liturujia ambayo Injli ya Mtakatifu Yohane anaeleze matukio yaliyotokea wakati wa siku za mwisho wa maisha ya Kristo, mapema kabla ya mateso yake (Yh 12,20-33). Wakati Yesu alikuwa Yerusalemu kwa ajili ya siku kuu ya Pasaka, baadhi ya Wayunani wenye mashaka kuhusu Yeye alivyokuwa anatenda na kutumiza wanaonesha shauku yao ya kutaka kumwona. Kwa kumkaribia Mtume Filipo wakimwambia  sisi tunataka kumwona Yesu. Papa amesisitiza, hata sisi tukumbuke kuwa na shauku hiyo ya “kutaka kumwona Yesu”.

Filipo akamwambia Andrea na baadaye wote wakamweleza Mwalimu. Katika ombi la wayunani, tungeweza kutambua swali ambao wanaume na wanawake wa kila mahali na kila wakati, wanauliza kwa Kanisa na hata kwa kila mmoja wetu: tunataka kumwona Yesu”. Papa Francisko akiendelea ameuliza swali: na jinsi gani Yesu anajibu swali hilo.  Ni kwa wa namna ya kufanya ufikirie. Yeye anasema hivi: “saa imefika atukuzwe Mwana wa adamu (…)amini nawaambia chembe ya ngano isipoanguka katika nchi ikafa hukaa hali hiyo peke yake bali ikifa hutoa mazao mengi.”( Yh 12, 23-24). Kiukweli wao walienda mbali zaidi. Yesu kwa hakika anajionesha kwao, kwa kila mtu ambaye anataka kumtafuta, ni mbegu tayari kufa ili kuzaa matunda mengi. Ni kama kusema kwamba “ikiwa unataka kunijua na kunielewa, tazameni mbegu ya ngano ambayo inakufa katika ardhi, na tazameni msalaba”, Papa amehimiza.

Papa Francisko akifafanua zaidi amesema “hii inakufanya ufikirie ishara ya Msalaba ambao kwa karne nyingi umekuwa ishara ya ubora wa Wakristo. Yeyote hata leo hii anayetaka kuona Yesu na labda anatoka katika Nchi na tamaduni ambazo ukristo haujulikani sana, je anaona nini kwanza? Ni ishara ipi ya pamoja anayokutana nayo? Msalaba. Katika Makanisa katika nyumba za wakristo, hata wanauvaa katika miili yao. Umuhimu ni  kwamba ishara iwe thabiti na Injili: msalaba hauwezi kutoeleza upendo, huruma, zawadi ya kujitoa bila kujibakiza: ni kwa njia hiyo tu inawezekana kuwa kweli mti wa uzima na wa maisha ya tele.

Hata leo hii, watu wengi na mara nyingi bila kusema, kwa namna halisi, wanataka kuona Yesu, kukutana naye na kumjua. Kutoka hapa inawezekana kutambua uwezekano mkubwa wa sisi wakristo na jumuiya zetu. Hata sisi lazima kujibu kwa ushuhuda wa maisha ambayo yanatoa huduma, ya maisha ambayo yanajikita katika mtindo wa Mungu, yaani ukaribu, upendo upeo na huruma ambayo inakuwa katika huduma. Hii ni kupanda mbegu ya upendo na si kwa maneno ambayo yapeperushwa, lakini kwa mifano halisi, rahisi na ujasiri, si hukumu za kinadharia, badala yake ni ishara za upendo. Kwa maana hiyo Bwana kwa neema yake, atatufanya tuwe na matunda hata kama ardhi iliyokauka kwa sababu ya kutolewana, matatizo au mateso, au majidai ya sheria au maadili ya kikleri. Ardhi hii imekauka.

Ni kwa njia hiyo basi katika majaribu na katika upweke, wakati mbegu inakufa ndiyo kipindi ambacho maisha yanachanua, ili kuzaaa matunda yaliyokomaa kwa wakati wake. Ni katika msukano wa kifo na maisha tunaweza kufanya uzoefu wa furaha na matunda ya upendo wa kweli na ambao Papa amerudia kusisitiza kuwa uwe mtindo wa Mungu, wa ukaribu upendo upeo na huruma. Kwa kuhitimisha Papa Francisko amesema, Bikira Maria atusaidie kufuata Yesu, kutembea kwa nguvu na furaha ya kujua njia ya huduma, ili upendo wa Kristo uangaze kwa kila tendo letu na kugeuka kuwa daima mtindo wa maisha yetu ya kila siku.

TAFAKARI YA PAPA JUMAPILI 21 MACHI
21 March 2021, 14:30

Sala ya Malaika wa Bwana ni sala inayowakumbusha waamini Fumbo la Umwilisho na husaliwa mara tatu kwa siku: Saa 12:00 asubuhi, Saa 6:00 mchana na Saa 12:00, wakati ambapo kengele ya Sala ya Malaika wa Bwana hugongwa. Neno Malaika wa Bwana limetolewa kutoka katika Sala ya Malaika wa Bwana aliyempasha Bikira Maria kwamba, atamzaa Kristo Yesu na husaliwa Salam Maria tatu. Sala hii husaliwa na Papa kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro wakati wa Jumapili na Wakati wa Siku kuu na Sherehe. Kabla ya Sala, Papa hutangulia kutoa tafakari akifanya rejea kwa Masomo ya siku. Baadaye kunafuatia salam kwa wageni na mahujaji. Kuanzia Sherehe ya Pasaka hadi Pentekoste, badala ya Sala ya Malaika wa Bwana, waamini husali Sala ya Malkia wa Bwana, sala inayokumbuka Ufufuko wa Kristo Yesu na mwishoni, husaliwa Sala ya Atukuzwe Baba mara tatu.

Sala ya Malaika wa Bwana/ Malkia wa Mbingu ya hivi karibuni

Soma yote >