Papa: Akiwa na wakuu na timu ya wachezaji kutoka Padua Papa: Akiwa na wakuu na timu ya wachezaji kutoka Padua 

Papa Francisko:Ikiwa hakuna roho ya timu hakuna mchezo wa kweli

Papa Francisko akikutana na viongozi wa timu na wachezaji kutoka Genova amewasahuri njia za kweli za kuweza kushinda michezo ambayo amesema ni kuwa timu moja na upendo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko Ijumaa tarehe 12 Machi 2021 amekutana na kuwasalimia viongozi timu ya wachezaji kutoka Genova, Italia ambapo amewasalimia na kuwashukuru kwa ujio wao. “Mchezo kwa upande wa Papa amethibitisha kuwa, ni muhimu wenye kuwa na tabia mbili. “Ya kwanza ni ile  timu ya umoja kwa maana ya kufanya kazi kwa pamoja kama kikundi na siyo pekee”. Papa amesema “Ikiwa hakuna timu hakuna mchezo” maaana  ya roho ya timu.

Kwa kufafanua zaidi Papa amesema kinyume chake wale ambao wanataka kufanya peke yao, mwisho wake hawana lolote wanalolifanya au labda wanatafuta sifa yao na kuharibu timu”. Kwa mtazamo wa pili, Papa amesema wao wasipoteze roho ya upendo. Na hiyo ni kwa sababu “Mchezo wa kweli ni wa upendo, angalau kila mara kutunza upendo huo”. Kwa maana hiyo Papa amesisitizia juu ya mambo hayo mawili: “kuwa Timu moja na roho ya kweli ya upendo”. Hatimaye Papa ameaomba wasali kwa ajili yake na kuwapa baraka.

12 March 2021, 16:26