WAATHIRIWA WA SHAMBULIZI LA KIGAIDI NCHINI INDONESIA WAATHIRIWA WA SHAMBULIZI LA KIGAIDI NCHINI INDONESIA 

Papa Francisko,asali kwa ajili ya waathiriwa wa shambulio la Indonesia!

Wakati wa sala ya Malaika wa Bwana,Papa Francisko amekumbuka na kusali kwa ajili ya waathiriwa wa vurugu kwa namna ya pekee,walioshambuliwa na kamikaze mbele ya Kanisa la Makassar nchini Indonesia.Katika mwaka wa pili wa janga Papa anawaalika waamini kufuata mfamo wa Mama wa Kristo ambaye alishiriki katika nafasi yake ya mateso huku akitunza taa ya matumaini ndani ya moyo wake.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Papa Francisko wakati wa tafakari, mara tu baada ya kumaliza Misa Takatifu katika kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na kabla ya sala ya Malaika wa Bwana tarehe 28 Machi 2021 amesema kuwa: “Ndugu wapendwa tumingia katika Juma Kuu Takatifu. Kwa mara ya pili tena tunaishi katika muktadha wa janga. Mwaka jana tulikuwa tumegutushwa, mwaka huu tumejaribiwa zaidi. Na mgogoro wa kiuchumi umekuwa mzito”. Katika hali hii ya kihistoria na kijamii, Mungu anafanya nini? Anachukua msalaba. Yesu anachukua msalaba kwa maana ya kujitwisha ubaya ambao unapelekea hali halisi ya ubaya wa kimwili, kisaikolojia na zaidi ubaya wa kiroho, kwa sababu, ubaya unatumia fursa ya mgogoro ili kupanda kukata tamaa, mahangaiko na magugu mabaya.

BARAKA YA PAPA
BARAKA YA PAPA

Katika hali hii ya kihistoria ya kijamii Mungu anafanya nini?

Papa Francisko anauliza swali kuwa na sisi? Je ni kitu gani tunapaswa kufanya? Anatuonesha Bikira Maria, Mama wa Yesu ambaye pia ni mwanafunzi wake wa kwanza. Yeye alimfuata mwanae. Alichukua sehemu yake ya mateso, ya giza, akaangaika na mchakato wa njia ya msalaba wa mateso huku akihifadhi ndani ya moyo wake taa ya imani. Kwa neema ya Mungu hata sisi tunaweza kufanya safari hiyo.

MATAWI YA MITENDE
MATAWI YA MITENDE

 

Tusali kwa ajili ya waathiriwa wa shambulio nchini Indonesia

Papa Francisko akiendelea amesema “Na katika njia ya msalaba wa kila siku, tunakutana na nyuso nyingi za kaka na dada zetu walioko kwenye matatizo na tusipitie mbali, badala yake tuache ili moyo ushutuliwe na huruma na kuwakaribia. Kwa wakati huu, kama Mkirene, tunaweza kufikiria kwanini  iwe mimi? Lakini baadaye tutagundua zawadi ambayo sisi bila kustahili imetugusa.  Vile vile Papa amesema: “Tusali kwa ajili ya waathiriwa wote wa vurugu kwa namna ya pekee wale waathirika wa shambulio lililotokea leo hii asubuhi nchini Indonesia mbele ya Kanisa Kuu la Makassar. Mama Maria atusaidie na ambaye anatutangulia katika njia zetu za imani”. Papa amehitimisha.

MISA YA MATAWI KATIKA KANISA KUU LA MT. PETRO
MISA YA MATAWI KATIKA KANISA KUU LA MT. PETRO
28 March 2021, 14:06