2021.01.12 Kwaresima ni kipindi cha kupyaisha imani, matumaini na upendo kuanzia na kushirikisha na wenye shida na walio pweke. 2021.01.12 Kwaresima ni kipindi cha kupyaisha imani, matumaini na upendo kuanzia na kushirikisha na wenye shida na walio pweke. 

UJUMBE WA PAPA FRANCISKO,KWARESIMA 2021:PYAISHA IMANI,TUMAINI &UPENDO

Angalieni,tunapanda kwenda Yerusalemu.(Mt 20,18).Kwaresima ni kipindi cha kupyaisha imani,tumaini na upendo.Ndiyo mada inayoongoza ujumbe wa Papa Francisko wa Kwaresima 2021.Kila hatua ya maisha ni kupindi cha kuamini,kutumaini na kupenda.Wito huo uongoze katika mchakato wa safari ya uongofu,sala,kufunga,kushirikishana mali zetu na kukaa karibu na maskini na wagonjwa katika kipindi hiki,vitusaidie kupyaisha imani katika jumuiya zetu na kibinafsi

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko ametoa ujumbe  wa Kwaresima 2021 unaoongazwa kauli mbiu “Angalieni, tunapanda kwenda Yerusalemu”(Mt 20,18). Kwaresima ni kipindi cha kupyaisha imani, matumaini na upendo. Yesu wakati wa kuwatangazia mitume wake juu ya mateso, kifo na ufufuko wake kama mapenzi ya Baba, aliwaonesha wao maana ya kina ya utume wake na kuwaalika waungane naye kwa ajili ya wokovu wa ulimwengu. Ili kuweza kuingia katika mchakato wa safari ya kwaresima ambayo itupeleka hadi kuadhimisha Pasaka, tukumbuke yule aliye jinyenyekeza  akawa mtii hadi mauti, mauti ya msalaba (Fil 2,8). Katika kipindi cha uongofu, tupyaishe imani yetu, tuchote maji hai ya matumaini na kupokea kwa moyo uliowazi upendo wa Mungu ambaye anatubadili kuwa kaka na dada katika Kristo. Katika usiku wa Pasaka tutapyaisha ahadi zetu za ubatizo ili kuzaliwa wanaume na wanawake wapya, shukrani kwa kazi ya Roho Mtakatifu. Lakini tayari katika mchakato wa kwaresima kama ilivyo tayari mchakato wa safari yote ya kikristo  ipo chini ya mwanga wa ufufuko, ambao unaongoza hisia, mienendo na chaguzi za yule anayetaka kufuata Kristo. Kufunga, sala na kutoa sadaka kama inavyo wakilishwa na Yesu katika mahubiri yake ( Mt 6,1-18), ni hali na kielelezo cha uongofu wetu. Njia ya umaskini na kujinyima (kufunga), mtazamo na ishara mbili za upendo wa mtu aliyejeruhiwa (sadakaka ) na maziugumzo kama ya kitoto na Baba ( sala) vitaturuhusu kuwa na imani ya kweli na matumaini hai ya upendo.

Papa Francisko anaandika kuwa, imani inatuita kupokea Ukweli na ili kugeuka kuwa mashuhuda mbele ya Mungu na mbele ya kaka na dada zetu. Katika kipindi cha Kwaresima, kupokea na kuishi ukweli uliojionesha katika Yesu maana yake kwanza ni kujiachia hufikiwe na Neno la Mungu linalotangazwa, kizazi hadi kizazi kutoka kwa Kanisa. Ukweli huu siyo ujenzi wa akili iliyohifadhiwa katika akili ya wachache waliochaguliwa, wakuu au kutofautisha, lakini ni ujumbe tunaoupokea na ambao tunaweza kuuelewa, shukrani kwa akili ya moyo, ulio wazi kwa ukuu wa Mungu ambaye anatupenda kabla sisi wenyewe hatujawa na dhamiri. Ukweli huu ni Kristo mwenyewe ambaye alibeba hadi mwisho ubinadamu wetu na kutengeneza njia, ni ngumu lakini umefunguliwa kwa wote inawafikia katika utumilifu wa maisha.  Uzoefu wa kufunga, wa kuishi kwa kujinyima unapelekea wale wote wanaoishi urahisi wa moyo kugundua kwa upya zawadi ya Mungu na kuelewa hali halisi yetu ya ubinadamu kuwa sura na mfano ambao Yeye mwenyewe anajikamilisha. Kwa kufanya uzoefu wa kukubali umaskini, anayefunga anakuwa maskini na kukusanya utajiri wa upendo alioupokea na kushirikisha. Kwa maana hii mazoezi ya kufunga yanasaidia kupenda Mungu na jirani kama anavyofundisha Mtakatifu Tommasi wa Aquinas, upendo ni harakati inayozingatia umakini kwa mwingine, ikizingatiwa kama jambo moja na yeye mwenyewe (Fratelli tutti 93).

Kwaresima ni kipindi cha kuamini au kwa akili ya kupokea kutoka kwa Mungu katika maisha yetu na kuruhusu yeye awe na makao yake ndani mwetu (Yh 14,23). Papa Francisko anasisitiza kuwa kufunga inamaanisha kutoa mambo yaliyo mengi ambayo hayafai, hata wingi wa habari, za kweli na uongo na uzalishaji wa kutumia, ili kuweza kufungua milango ya mioyo yetu, kwa yule anayekuja kwetu akiwa maskini wa kila kitu, lakini aliyejaa neema na ukweli (Yh 1,14), mwana wa Mungu mwokozi. Matumaini ni kama maji hai yanayoturuhusu kuendelea katika safari yetu. Msamaria ambaye aliombwa na Yesu maji ya kunywa katika kisima hakuelewa wakati Yeye anamweleza kwamba angempatia maji hai (Yh 4,10). Mwanzo alifikiria maji ya kawaida, kinyume Yesu alikuwa na maana ya Roho Mtakatifu, yale mbayo atampatia kwa wingi katika Fumbo la Pasaka na ambayo yanatupatia matumaini yasiyokatisha tamaa. Tayari katika kutangaza mateso yake na kifo, Yesu alitangaza matumaini anaposema “siku ya tatu nitafufuka) Mt 20,19). Yesu anazungumza wakati ujao ulio wazi wa huruma ya Baba. Kutumaini na Yeye na shukrani kwake ina maana ya kuamini kuwa historia haifungwi juu ya makosa yetu, juu ya vurugu zetu na ukosefu wa haki na juu ya dhambi ambazo zinasulibisha upendo. Maana yake ni kuchota kutoka katika moyo wake uliofunguliwa msamaha wa Baba. Katika muktadha wa sasa, wasiwasi ambao tunaouishi na ambao utafikiri ni udhaifu na hukosefu wa uhakika, kuzungumza tumaini inawezekana kuonekana kama mchezo. Kipindi cha kwaresima kimefanywa kwa ajili ya kushinda, kurudia kuwa na mtazamo wa uvumilivu katika Mungu ambaye anaendelea kuutunza Uumbaji wake wakati sisi mara nyingine tunauharibu (Laudato si’, 32-33.43-44).

Katika kuendelea kufufanua Papa Francisko anasema ni uzoefu wa mapatano ambapo anatushauri kwa shauku Mtakatifu Paulo: “ninyi kwa ajili ya Kristo hacheni mpatanishwe na Mungu” (2 Kor 5,20). Kupata msamaha katika Sakramenti ambayo ndiyo moyo wa mchakato wetu wa uongofu, tunageuka kwa mara nyingine tena kuwa wasambazaji wa msamaha, kutokana na kwamba sisi wenyewe tumeupokea, tunaweza kuutoa kwa njia ya uwezo kuishi mzungumzo ya ukarimu na kuwa na tabia ambayo inatia moyo aliye jeruhiwa. Msamaha wa Mungu hata kwa njia ya maneno yetu, ishara zetu, zinaruhusu kuishi Pasaka ya udugu. Katika kipindi cha Kwaresima, tunakuwa makini zaidi kusema maneno ya faraja, ambayo yanatia moyo na kutoa nguvu, yanatoa shauku, badala ya maneno ambayo yanadhalilisha, yanachochea, na kudharau (Fratelli tutti, 223). Wakati mwingine katika kutoa tumaini, inatosha mtu awe mkarimu, ambaye anaweka pembeni wasiwasi wake na dharura zake ili kuweka umakini, kutoa zawadi ya tabasamu, kusema neno la kuhamasisha, kuwezesha nafasi moja ya kusikiliza katikati ya kutokujali (Fratelli tutti 224). Katika kujiundia na katika sala ya kimya, tunapewa tumaini kama zawadi ambayo ni  kiongozi na mwanga wa ndani ambao unaangazia changamoto na chaguzi za utume wetu. Hapo ndiyo msingi wa kujiunda katika kusali (Mt 6,6) na kukutana  siri ya  Baba wa huruma.

Kuishi kwarezima na tumaini ina maana ya kuhisi kuwa ndani ya Yesu Kristo, shuhuda katika kipindi kipya katika Mungu ambaye anafanya mambo yote mapya (Uf 21,1-6). Maana ya kupokea tumani la Kristo ambalo anatoa maisha juu ya msalaba na ambapo Mungu anafufuka siku ya tatu, ni kuwa tayari kujibu kila mmoja sababu ya tumaini ambalo limo ndani mwetu (1 Pt 3,15).  Upendo ambao unaishi katika nyayo za Kristo, kwa umakini na katika huruma ya  kila mmoja ni zaidi ya kielekezo cha imani yetu na matumaini yetu. Upendo unafurahia kuwa mwingine anakua. Tazama ndiyo maana mwingine anateseka anapomwona mwingine akiwa huzuni na  aliye na upweke, mgonjwa, hasiye na nyumba na mwenye kuhitaji. Upendo ni mwamko wa moyo unaotoka ndani mwetu na ambao unazaaa, ufungamanishaji na  kushirikishana na muungano. “Kuanzia na upendo kijamii inawezekana kuendelea katika kuelekea ustaarabu wa upendo ambao sisi sote tunaweza kuhisi kuitwa. Katika mzunguko wake, upendo ni wa ulimwengu ambao unaweza kujenga ulimwengum mpya kwa sababu hauna hisia tasa, walakini namna bora  ya kufikia njia muafaka za maendeleo kwa wote (Ft, 183). Upendo ni zawadi ambayo inatoa aina ya maisha yetu na shukrani kwa yule anayefikiria hasiye kuwa navyo kama mjumbe wa familia yetu moja, rafiki na ndugu. Kile kidogo kinaposhirikishwa kwa upendo hakiishi kamwe, bali kinageuka kuwa hifadhi ya maisha na furaha. Hii ilijitokeza katika unga na mafuta ya mjane wa Sarepta ambaye alimpatia mkate nabii Eliah(1Wafal17,7-16) na ni sawa na mikate iliyobarikiwa na Yesu akaimega na kuwapa mitume wake ili wawagawie umati ( Mk 6,30-44). Hii inajitokeza hata katika sadaka yetu ndogo au kubwa inayotolewa kwa furaha na urahisi.

Kuishi Kwaresima ya upendo ina maana ya kumtunza ambaye anajikuta katika hali ya mateso, ya kutupwa au uchungu kwa sababu ya janga la covid-19. Katika muktadha mkubwa usio na uhakika wa kesho, kwa kukumbuka neno la Mungu alilomwambia mtumishi “Usiogope, maana nimekukomboa”( Is 43,1), tutoe kwa upendo wetu neno la imani na kufanya mwingine ahisi kuwa Mungu anampenda kama mtoto. “Ni kwa njia ya mtazamo wenye maono tu ambay unabadilisha upendo  hadi kumpelekea kukaribisha kwa hadhi mwingine, maskini ambao wanajulikana na kusifiwa katika hadhi yao kuu, kuheshimiwa katika mtindo wao na katika utamaduni wao na kwa maana hiyo ukweli wa ufungamanishwaji katika jamii. Papa Francisko katika kuhitimisha ujumbe wa kwaresima 2021, anasema kila hatua ya maisha ni kupindi cha kuamini, kutumaini na kupenda. Wito huo wa kuishi Kwaresima kama mchakato wa safari ya uongofu, sala na kushirikishana mali zetu, utusaidie kurudi kwa upya katika kumbu kumbu zetu kijumuiya na kibinafsi, imani ambayo inakuja kutoka kwake Kristo aliye hai, tumaini ambalo linaongozwa kwa uvuvio wa Roho na upendoa ambao ni kisima kisicho kauka na ndiyo moyo wa huruma ya Baba. Mama Maria wa Mwokozi, mwaminifu chini ya miguu ya Msalaba na katika moyo wa Kanisa, atusaidie kwa uwepo wake mpole na baraka ya Mfufuka itusindikize katika safari ya kuelekea katika nuru ya Pasaka. Ujumbe wa Papa Franciskoi ulitiwa saini katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Laterano Roma tarehe 11 Novemba 2020, katika Kumbu kumbu la liturujia ya Mtakatifu Martino wa Tours.

12 February 2021, 11:30