Tafuta

2021.02.24 Prof. Roberto Bernabei ni Daktari binafsi wa Papa 2021.02.24 Prof. Roberto Bernabei ni Daktari binafsi wa Papa 

Profesa Bernabei ni daktari mpya binafsi wa Papa

Ameteuliwa na Papa Francesco,Profesa wa Chuo Kikuu Katoliki,Roma kuchukua nafasi ya Daktari Fabrizio Soccorsi aliyemhudia tangu 2015 hadi mauti yalipomfikia mwezi Januari uliopita.

Papa Francisko amemteua Daktari binafsi  Profesa Roberto Bernabei, ambaye ni Profesa katika Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu Roma. Alizaliwa huko Frenze, Italia tarehe 24 Janauri 1952. Baada ya kuhitimu masomo yake katika Tiba na Upasuaji katika Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu Roma mnamo 1976, amejishughulisha na Tiba ya Ndani na Magonjwa ya Mishipa ya Moyo. Yeye ni Profesa wa kawaida wa Tiba ya Ndani na Geriatrics na ni Mkurugenzi wa Shule ya Utaalam katika Geriatrics, Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu Roma; Vile vile Mkurugenzi wa Idara ya Uzee, Neurolojia, Mifupa na Sayansi ya Kichwa na shingo  na Mkurgenzi wa Mfuko wa Chuo Kikuu cha Agostino Gemelli (IRCCS,) Roma. Ni Mwanachama wa Chuo cha Ulaya kwa ajili ya madawa ya Uzee. Amechapisha kazi nyingi na kutoa michango ya kisayansi.

Uteuzi huo unafuatia kifo cha Professa Fabrizo Soccorsi  aliyekuwa daktari binafsi wa Papa tangu 2015, kilichotokea Jumamosi tarehe 9 Januari 2021 kwa sababu ya virusi vya Covid-19.  Papa Francisko tarehe 26 Januari 2021 alishiriki hata katika Ibada ya Misa Takatifu iliyoadhimishwa kwenye Kanisa la Bikira Maria Malkia wa Familia mjini Vatican, kwa ajili ya kumkumbuka na kumwombea Marehemu huyo aliyefariki dunia akiwa anakaribia miaka 79

24 February 2021, 16:25