Tafuta

Papa Francisko amesali kwa ajili ya waathiriwa wa janga la Himalaya!

India na Mashariki ya Mbali vimesikika katik maneno ya Papa leo hii mwishoni mwa katekesi yake Jumatano tarehe 10 Februari.Papa ameelezea ukaribu na waliojeruhiwa na kupotea aisha katika makasa uliotokea siku ya Jumapili iliyopita huko Himalay pia ametoa matashi mema ya amani,wema na udugu wanaojiandaa kusherehekea Mwaka Mpya wa Mwezi huko India.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mara naada ya katekesi yake Papa Francisko ameonesha ukaribu wake na kwa waathiriwa wa mkasa uliotokea siku tatu zilizopita Kaskazini mwa India, huko himalaya mahali ambapo sehemu ya kutunza majai ilbomoka na kusababisha mafuriko makali ambayo yalizingira na kukumba maeneo ya ujenzi wa mitambo miwili ya umeme. Papa anawaombea wafanyakazi waliokufa na familia zao,na kwa watu wote waliojeruhiwa na kupata madhara.

"Katika Mashariki ya Mbali na katika sehemu mbalimbali za ulimwengu, Ijumaa tarehe 12 Februari, mamilioni ya wanaume na wanawake wataadhimisha Mwaka Mpya wa Mwezi" Ni maneno ya Papa ambapo ameumia fursa hiyo kuwatumia salamu zake kwa wote na familia zao, pamoja na matashi mema ya  mwaka mpya ambao uweze kuzaa matunda ya udugu na mshikamano. Kwa wakati huu, ambao kuna wasiwasi mkubwa juu ya kukabiliwa na changamoto za janga ambalo linaathiri sio tu mwili na roho za watu, lakini pia kuathiri uhusiano wa kijamii, Papa ameonesha matumaini kwamba kila mtu ataweza kufurahiya afya kamili na utulivu wa maisha. Na hatimaye amewaomba wasali kwa ajili ya zawadi ya amani na kila wema, ameakumbusha kuwa hayo yote hupatikana kwa  njia ya wema, heshima, utabiri na ujasiri. Kamwe wasisahau kuwa na huduma ya upendeleo kwa maskini na wadhaifu.

10 February 2021, 15:54