2021.02.07  Bango la Marathon ya Ulimwenguni kuhusu Maombi mtandaoni Dhidi ya biashara haramu ya binadamu na utumwa mamboleo. 2021.02.07 Bango la Marathon ya Ulimwenguni kuhusu Maombi mtandaoni Dhidi ya biashara haramu ya binadamu na utumwa mamboleo. 

Papa Francisko:Uchumi bila biashara haramu ni uchumi wa utunzaji

Katika Ujumbe kwa njia ya Video katika fursa ya Siku ya Sala na Tafakari Kimataifa dhidi ya Biashara Haramu ya Binadamu na utumwa mamboleo, iadhimishwayo kila tarehe 8 Februari,sambamba na kumbukumbu ya Mtakatifu Josephine Bakhita,Papa anakataa mitindo ya kiuchumi ambayo imejifananisha na mitindo ya siasa za utumwa mbamboleo.Badala yake iwe yenye ujasiri wa kuchanganya faida halali na kuhamasisha ajira na hali nzuri ya kufanya kazi.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Papa Francisko ametuma ujumbe kwa njia ya mtandao kwa washiriki wa Mkutano katika Siku ya VII ya Sala na Tafakari Kimataifa dhidi ya Biashara Haramu ya Binadamu na utumwa mamboleo iadhimishwayo kila tarehe 8 Februari, sambamba na kumbukumbu ya Mtakatifu Josefina Bakhita. Papa Francisko katika ujumbe huo kwa njia ya video anawageukia wote ambao wanafanya kazi katika nyanja hiyo ya kudhibiti biashara haramu ya watu, na ambao leo hii wameunganika kiroho kuadhimisha Siku hii kwa sala huku wakiongozwa na kauli mbiu mwaka huu 2021: “Uchumi bila biashara haramu ya binadamu na utumwa”. Ni furaha yake kutambua kuwa mwaka huu katika mikutano mbali mbali ya sala kwa njia mazungumzo ya kidini na imeunganishwa hata barani Asia. Ujumbe wake ameupanua kwa watu wote wenye mapenzi mema ambao wanasali, wanajibidisha, wanasoma na kutafakari kwa ajili ya kukomesha biashara haramu ya watu; na zaidi kama ilivyokuwa kwa Mtakatifu Josephine Bakhita ambaye leo kilitutujia ikumbumbukwa siku yake na aliyepata kufanya uzoefu wa biashara haramu katika maisha yake. Siku hii ni muhimu, kwa sababu itusaidia wote kukumbuka janga hili baya na kutiaa moyo ili tusiacha kusali na kupambana pamoja. Tunaweza kutafakari na kuwa na dhamiri ambayo daima inasindikizwa na ishara za dhati, na kwa ajili ya kufungua njia za kuendelezwa kijamii. Lengo kubwa ni kwamba mtu yoyote ambaye anafanyishwa utumwa aweze kuwa huru na kuwa mstari wa mbele wa maisha yake na kuwa sehemu hai ya ujenzi wa wema wa pamoja.

Papa Francisko amesema hii ni Siku ya sala. Ndiyo kuna haja ya kusali kwa ajili ya kusaidia waathirika wa biashara haramu ya binadamu na watu ambao wanasindikiza mchakato wa ufungamanishwaji na kuweza kuwaingiza kwa upya katika jamii. Kuna haja ya kusali ili kuweza kujifunza kukaribisha kama ubinadamu na kutia moyo yule mwenye uchungu na mahangaiko, kwa kuzingatia matumaini yaliyo hai. Kusali ili kuwa walinzi wa asubuhi wenye uwezo wa kung’amua na kufanya changuzi alekezi kwa wema. Sala inagusa moyo na kusukuma katika mantendo ya dhati, matendo bunifu, yeye ujasiri ambao unachukua wajibu hata kuthubutu katika imani na nguvu ya Mungu ( Mk 11,22-24). Kumbu kumbu ya Mtakatifu Bakhita  ni wito wa nguvu katika suala hili la imani na sala. Ushuhuda wake unarudia tena kusikika ukiwa hai hata sasa! Na ni wito wa kuweka watu katikati walioathirika na biashara hiyo, familia zao na jumuiya zao. Ni wao ambao wako katikati ya sala zetu. Mtakatifu Bakhita   ndiye kiongozi wa siku hii na kwa wote  walioko  katika huduma hiyo ( Lk 17,10), Papa amehimiza.  Papa Francisko akiendelea amependea kushirikisha baadhi ya tafakari na matendo yanayo tazama mada waliyochagua “ uchumi bila bishara haramu ya binadamu” na mambo mengine wanaweza kupata katika ujumbe wake alioutoa katika tukio la ‘Economy of Francesco’, kunako tarehe 21 Novemba 2020, amethibisha Papa.

Uchumi bila biashara haramu ni uchumi wa utunzaji: Kwanza kabisa Papa Francisko amesema uchumi unaweza kuchukuliwa kama utunzaji wa watu na asili kwa kutoa uzalishaji na huduma ya kukuza wema wa pamoja. Uchumi ambao unatunza kazi, kwa kuunda fursa za ajira na ambazo hazinyoji wafanyakazi,  katika hali mbaya na kufanya kazi kwa masaa ya kuzidi kiasi. Janga la Covid limeongezea ubaya huo  na kusababisha hali kuwa ngumu ya unyonyoji katika kazi; ukosefu wa nafasi za kazi umewaadhibu watu waathirika wa biashara katika mchakato wa kuweza kujikwamua na kuingizwa tena katika jamii. Katika wakati huu ambao utafikiri hakuna suluhisho na kupoteza maisha ni vema kusisitiza mshikamano kijamii ambao unatokana na kufafanua  kuwa wahusika wa udhaifu wa mmoja na mwingine ni katika kutunza na maana ya uchumi wa mshikamano (Fratelli tutti, 115).  tufanye kazi kwa ajili ya msimamo ambao unaunganisha na mshikamano. Tunaamini kuwa mshikamano ambao unaratibu vizuri, unatoa mahali pa ujenzi kijamii zaidi katika usalama na msingi

Nafasi ya Pili Papa Francisko amesema, uchumi bila biashara ya utumwa ni uchumi ambao una sheria ya soko inayohamasisha haki na siyo kutenga na kutazama mafao maalum. Biashara ya haramu ya watu inapata ardhi yenye rutuba katika mfumo wa ubepari mamboleo, katika udhibiti wa masoko ambao unakusudia kuongeza faida bila mipaka ya maadili, bila mipaka ya kijamii, na bila mipaka ya mazingira (Fratelli tutti 202).  Ikiwa wanafuata mantiki hiyo ni mfumo wa kufuata mahesabu ya faida na kutokuwa na faida. Chaguzi hazifanyiki kwa mantiki kimaadili, bali kufuata mafao yao binafsi, na mara nyingi  wamevaa kwa ujanja sura ya huduma ya kibinadamu au ya mazingira. Chaguo hazifanyiki kwa kutazama watu: watu ni moja ya idadi tu pia ya kutumiwa.

Papa francisko akifafanua pendekezo lake  la tatu, amesema kwa njia hiyo uchumi bila bishara haramu ni uchumi jasiri, kwani unahitajika ujasiri.  Sio kwa maana ya kukosa uaminifu, shughuli za hatari katika kutafuta mapato rahisi. Hapana, na sio ujasiri wa kawaida ambao unahitajika katika hilo. Kinyume chake ni shauku ya kujenga kwa uvumilivu, kupatana na ambao hautazami daima faida kwa haraka bali matunda ya kupata na kwa muda mrefu hasa kwa watu. Ujasiri wa kuunganisha uhalisi wa familia na kwa uhamasishaji wa ajira na hali ya hadhi ya kazi.   Katika kipindi cha mgogoro wa sasa, ujasiri huo bado ni wa lazima. Ametoa mfano pia katika mgogoro wa biashara haramu ya mafuta, na kwamba wote tunajua  na tunaona kila siku. Katika mgogoro wa biashara haramu ya mafuta inahitaji kwa maana hiyo  hata kuongeza uchumi ambao unajibu mgogoro kwa namna ya upeo wa mbali, njia ya kudumu, na msimamo. Kwa kuhitimisha amehimiza kuweka yote katika sala zetu kwa namana ya pekee leo hii na kwa maombezi ya Mtakatifu Bakhita. Papa anasali kwa ajili yao na kwa wote kusali kwa ajili ya watu wote waaathirika wa biashara hii haramu ya binadamu na utumwa mamboleo.

08 February 2021, 16:08