Tafuta

Uwanja wa ndege Goma Drc Uwanja wa ndege Goma Drc 

Papa atoa salamu za rambi rambi kufuatia kifo cha wahudumu wa amani

Papa Francisko ametuma salamu za rambi rambi kwa rais wa Jamhuri ya Italia,kwa familia,wafanyakazi na marafiki wa watu watatu waliouawa katika shambulio dhidi ya ujumbe wa ubalozi wa Italia uliokuwa ukizuru ndani ya Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Drc.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ni kwa uchungu mkuu kufuatia na shambulizi lililotokea huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Drc, ambapo wamepoteza maisha kijana balozi wa Italia Luca Attanasio, afisa wake Vittorio Iacovacci na dreva wao wa Congo, Mustapha Milambo. Ndivyo Papa Francisko anaanza na maneno hayo katika ujumbe wa salamu za rambi rambi akizielekeza kwa Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella.

Ushuhuda wa Mwanadiplomasia na afisa wa ubalozi

Papa Francisko ametuma salamu za rambi rambi kwa familia za waathiriwa, kwa ndugu wa mwanadiplomasia, kwa kiungo kizima cha afisa wa ubalozi kutokana na “vifo hivi vya wahudumu wa amani na haki”. Na zaidi Papa anakumbuka vema mfano wa ushuhuda wa Balozi huyo, ambaye alikuwa ni mtu wa  thamani ya kibinadamu na kikristo, na daima akiwa mstari wa mbele katika kusuka mahusiano ya kidugu na maelewano; na kwa ajili ya kudumisha utulivu na mahusiano katikati ya umbu la nchì hiyo ya kiafrika.  Papa ameongeza kuwa, kama ilivyokuwa hata afisa wa balozi huyo, mtaalam na mkarimu katika kutoa huduma yake kwa jirani na aliyekuwa karibu ya kuunda familia mpya.

Sala ya Papa

Papa Francisko katika kuhitimisha salamu zake anainua “sala zake kwa Mungu kwa ajili ya marehemu ili wapumzike kwa amani, watoto hao wa taifa la Italia na kutoa ushauri wa kumwamini Bwana mpaji ambaye katika mikono yao iliyotenda mema isiweze kupotea na zaidi ikiwa imeteseka na kwa sadaka ya maisha. Kwa upande wa Rais wa Jamhuri ya Italia, wahudumu wake wa karibu na ndugu na wafanyakazi wa waathiriwa na wote ambao wanaomboleza kwa vifo hivi Papa anawapa kwa moyo baraka yake ya kitume.

24 February 2021, 10:17