Tafuta

2020.01.25 Maadhimisho ya Masifu ya jioni katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo, Roma 2020.01.25 Maadhimisho ya Masifu ya jioni katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo, Roma 

Papa Francisko:chuki zinazuia umoja,tupende ubinadamu ambao unateseka zaidi!

Katika Masifu ya jioni ya Siku kuu ya Mtakatifu Paulo,sambamba na kufunga Wiki ya 54 ya Maombi kwa ajili ya Umoja wa Wakristo,Kardinali Koch kwa niaba ya Papa ambaye hakuweza kushiriki kutokana na maumivu ya mguu,ameongoza masifu hayo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta na amesoma tafakari la Papa ambayo inawaalika Wakristo kusali na kuwa na upendo kwa wenye shida zaidi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika masifu ya pili ya jioni kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta, Roma kwenye fursa ya Sikukuu ya Mtakatifu Paulo Mtume wa Watu sambamba na kufunga Wiki ya 54 ya Maombi kwa ajili ya kuombea Umoja wa Wakristo, tarehe 25 Januari, Kardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Kikristo, amesoma mahubiri yaliyoandaliwa na Papa Francisko kutokana na maumivu ya mguu. Kabla ya kuanza kusoma Kardinali Koch ameelezea kuwa ni heshima ya kusoma mahubiri hayo na  kuwaomba wote wabaki wameungana na sala kwa ajili ya Baba Mtakatifu. Papa Francisko katika tafakari hiyo ameongozwa na kauli mbiu ya wiki: “Kaeni katika pendo langu” (Yh 15,9) na kwamba Yesu alihusisha ombi hilo katika picha ya mti na matawi yake, kama Injili ilivyoeleza. Bwana ndiye maisha na maisha ya kweli ambaye hasaliti matarajio, bali ni mwaminifu wa upendo na wala haupunguzi licha ya dhambi zetu na migawanyiko yetu.

Tumeunganishwa katika matawi kwa njia ya ubatizo na ndani ya Yesu

Katika maisha haya ambayo ni Yeye, sisi sote tumebatizwa na tumeunganishwa katika matawi ikiwa na maana kwamba tunaweza kukua na kuzaa matunda tu ikiwa tunabaki tumeungana na Yesu. Papa Francisko amehimiza kuwa makini jioni hiyo hasa kwa kutazama umuhimu wa umoja ambao una ngazi kuu. Ni kufikiria mti na matawi yake ambayo inawezakana kuyahusisha katika umoja ambao unaundwa na mzunguko kama pete tatu zilizounganishwa kama mfano wa kisiki. Akifafanua tafakari hiyo anabinisha kuwa, mzunguko wa kwanza ni ule wa ndani ambao ni kubaki na Yesu. Kutoka pale ndipo safari zote zinaanzia za kila mmoja kuelekea umoja. Katika hali halisi ya sasa, ya haraka na ngumu ni rahisi kupoteza umakini huo kutokana na mambo mengi yaliyopo pembeni, Papa anaonya. Wengi wanahisi kugawanyika vipande vipande ndani mwao na wasio na uwezo na wala  msimamo mahali popote, yaani  kukosa msimamo katika mambo mbali mbali ya maisha. Yesu anaeleza siri moja ya kuweza kuwa na msimamo hasa kwa kubaki na Yeye. Katika somo ambalo limesikika, linarudia mara saba mantiki hiyo (Yh 4-7.9-10), Papa Francisko amebainisha.

Bila  yeye hatuwezi kufanya lolote:sala na kuabudu

Yeye kwa hakika anajua kuwa bila Yeye hatuwezi kufanya lolote. Alituonesha hata jinsi ya kufanya kwa kutupatia mfano, ambao kila siku alikuwa nakwenda mahali pa faragha kwenye jangwa kusali.  Tunahitaji sala, kama  maji ya kuweza kuishi. Sala binafsi, namna ya kukaa na Yesu, kuabudu, ndiyo msingi wa kubaki na Yeye. Na ndiyo njia ya kukabidhi ndani ya moyo wa Bwana kila kitu kinacho jikusanya ndani ya mioyo yetu, matumaini na hofu, furaha na uchungu. Lakini zaidi, yanayojikita katika Yesu kwenye sala, tunafanya uzoefu wa upendo wake. Kuishi kwetu kunapata maisha kama vile matawi yanavyopata lishe kutoka katika kisiki. Huo ndiyo umoja wa kwanza, na ufungamanishwaji wetu kibinafsi, ni shughuli ya neema ambayo tunaipata kwa sababu ya kubaki ndani ya Yesu.

Mzunguko wa pili ni umoja na wakristo:kipimo ni upendo kwa mwingine

Mzunguko wa pili ni ule wa umoja na wakristo. Papa Franciso amebainisha kuwa sisi ni matawi ya mti huo huo, sisi ni vyungu vinavyowasiliana, wema na ubaya ambao kila mmoja anatenda unageukia wengine. Katika maisha ya kiroho yanatazamia hatima na sheria ya mzunguko. Kipimo ambacho tunabaki ndani yake Mungu, kinatufanya kuwakaribia wengine na katika kipimo ambacho tunawakaribia wengine tunabaki ndani ya Mungu. Hii ina maana kwamba ikiwa tunasaidia kwa roho na ukweli ndipo mahitaji ya dhati ya kupenda wengine yatakuwapo, kwa upande mwingine, ikiwa tunapendana na wengine, basi Mungu anabaki ndani mwetu (1 Yh 4,12). Sala haiwezi kutopelekea upendo, la sivyo inakua ni ibada ya bure. Haiwezekani kabisa kukutana na Yesu bila mwili wake, ambao umeundwa na viungo vingi, yaani kwa waliobatizwa wote, Papa amesisitiza. Ikiwa kuabudu kwetu ni kwema, upendo utakua kwa wote ambao wanamfuata Yesu na kutegemea na umoja wa kikristo ambamo tunatoka na kwamba  hata wale ambao siyo wa kwetu lakini ni wake. Hata hivyo mara kwa mara tunaona jinsi ambayo kupenda ndugu siyo rahisi kwa sababu haraka zinajitokeza kasoro, na udhaifu na kubaka ndani ya akili majeraha ya wakati uliopita.

Je ni kwanini Baba anakata na kupunguza matawi?

Hapa ndipo unakuja msaada wa matendo ya Baba ambaye ni kama mtaalam wa kilimo (Yh15,1), kwani anajua vizuri kwamba “kila tawi lisilotoa matunda, analikata na kila tawi ambao linatoa matunda analipunguza matawi ili liweze kuzaa matunda mengi (Yh 15,2). Baba anakata na kupunguza. Ni kwa nini? Ni kwa sababu ili kupenda tunahitaji kuondokana na wale ambao wanatupeleka nje ya njia na kutupindisha, kwa kujizuia kuzaa matunda, amebainisha Papa Francisko. Kwa njia hiyo anaomba tusali kwa Baba ili aweze kuondoa ndani mwetu chuki dhidi ya wengine, kushikilia malimwengu yanayotuzuia umoja na kuacha nafasi ya pili ya matawi ya ardhi hii kuwa na vizingiti vya wakati ambavyo leo hii vinatuondoa katika Injili.

Mzunguko wa tatu ni wa ubinadamu wote, Roho Mtakatifu anatuwezesha kusamehe

Papa Francisko akijikita kufafanua mzuko wa tatu wa umoja amasema huo ni mpana na ambao ni ubinadamu wote. Hii tunaweza kutafakari kwa mantiki ya Roho Mtakatifu. Katika mti ambao ni Yesu, yeye ni kiini kinachofikia sehemu zote. Lakini Roho Mtakatifu anayevuvia mahali ambapo anataka na kupelekea anakotaka penye umoja. Yeye anatupelekea kupenda, si tu kwa yule anayetutakia mema na kufikiria kama sisi, lakini wote, kama Yesu alivyotufundisha.  Anatuwezesha kusamehe maadui na mabaya tuliyopata. Anatusukuma kuwa hai na wabunifu wa upendo. Anatukumbusha kuwa jirani siyo tu anayeshirikishana thamani zetu na mawazo yetu, bali hata sisi tunaalikwa kuwa karibu na wote, kuwa wasamaria wema wa ubinadamu ulioathirika, maskini ambao leo hii wamelala njia za ulimwengu  na ambao Mungu anatamani kuwainua kwa huruma yake kuu. Roho Mtakatifu ambaye ni mdau wa neema, atusadie kuishi neema ya bure ya kupenda hata wale wasio stahili, kwa sababu upendo ulio safi na usio tafuta faida ambao Injili inafundisha ndiyo unazaa matunda. Kwa kuwa na  matunda ya mti, na upendo wa bure mtatambuliwa  kuwa sehemu ya maisha ya Yesu.

Kupenda daima maskini na zaidi wenye kuhitaji

Roho Mtakatifu anatufundisha uhakika wa upendo kwa ajili ya kaka na dada ambao tunashirikishana ubinadamu, ambao Kristo aliunganisha yeye  mwenyewe, na kutupelekea kuwapenda  daima maskini zaidi na wenye kuhitaji (Mt 25, 31-35). Kwa kuhudumia pamoja, tutajigundua kuwa ndugu na kukua pamoja katika umoja. Roho Mtakatifu ambaye anapyaisha nchi, anatushauri  kuhudumia hata nyumba yetu ya pamoja, kufanya uchaguzi wa dhati juu ya namna tunavoishi na kutumia, kwani kinyume chake katika kuzaa matunda ni unyonyaji na kuharibu rasilimali msingi ambayo kwa walio wengi wanakosa. Roho Mtakatifu huyo huyo, mkuu wa mchakato wa safari ya kiekumene awezesha jioni hiyo kusali kwa pamoja, Papa ameomba. Na wakati wakifanya uzoefu huo wa umoja ambao unazaliwa na matashi ya Mungu kwa sauti moja, Papa amependa kuwashukuru wote ambao kwa Wiki hii wamesali na wataendelea kusali kwa ajili ya umoja wa wakristo. Amewasalimia wawakilishi wa Makanisa na Jumuiya za Kanisa ambao walikuwapo, vijana wa kiorthodox wa nchi za mashariki ambao wanasoma Roma kwa msaada wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya uhamasishaji wa Kikristo, mapofesa, na wanafunzi wa kiekumene wa Taasisi ya Bossey ambao walikuwa waungane nao, lakini hawakuweza kufika Roma kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, lakini wamefuatilia kwa njia ya mitandao. Papa amewaomba wabaki wameungana katika Kristo na Roho Mtakatifu ambaye ameuisha katika mioyo yetu atufanye kuhisi kuwa wana wa baba, kaka na dada kati yetu familia ya kibinadamu. Utatu mtakatifu, umoja wa upendo utafanye kukua katika umoja.

TAFAKARI YA PAPA WIKI YA UMOJA WA KIKRISTO

 

25 January 2021, 18:51