Tafuta

Harakati za kutafuta watu katika vifusi kufuatana na tetemeko la ardhi huko Sulawesi, Indonesia. Harakati za kutafuta watu katika vifusi kufuatana na tetemeko la ardhi huko Sulawesi, Indonesia. 

Ukaribu wa Papa kwa watu wa Indonesia kwa pigo la tetemeko la ardhi!

Papa Francisko ametuma sala za rambi rambi kufuatia na waathirika wa tetemeko la ardhi lililokumba watu usiku wa manane katika kisiwa cha Sulawezi nchini Indonesia. Katika telegram yake iliyotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin,Katibu wa Vatican,ambayo amemtumia Balozi wa Kitume nchini humo anaonesha masikitiko na sala kwa ajili ya wote wanaoteseka na kuwatia moyo watu wanaoendelea kutoa msaada kuokoa watu waliofunikwa na vifusi.

Na Sr. Angela Rwezaula,-Vatican.

Jumamosi tarehe 16 Januari 2021, Papa Francisko amewatumia viongozi wa Kanisa na raia wa Indonesa salam za rambi rambi na mshikamano wake kufutia na tetemeko la ardhi lililotokea usiku wa manane mwishoni mwa wiki hii katika kisiwa cha Sulawezi. Katika telegram hiyo ambayo imetiwa saini na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin iliyoelekezwa kwa Balozi wa kitume nchini humo Askofu Mkuu Piero Pioppo, anaandika kuwa “kwa kupokea habari za kusitikisha juu ya janga na kupoteza maisha ya binadamu na uharibifu wa mali binafsi kutokana na  tetemeko la nguvu nchini Indonesia, Papa anaelezea mshikamano wa dhati kwa watu wote aambao wamepata janga la asili. Kardinali Parolini anawahikishia kuwa Papa anasali kwa ajili ya marehemu wote, na kwa ajili ya kupona wote waliojeruhiwa na wapate faraja wale wote ambao wanateseka”. Kwa namna ya pekee anawatia moyo mamlaka zote za Kanisa na Serikali, na wale wote ambao wanaendelea kujitikita katika juhudi za kusaidia. Na kwa wote, Baba Mtakatifu anahitimisha akiwabariki kwa baraka ya Mungu ili iwatia nguvu na matumaini.

Nyumba nyingi kwa wastani zimeanguka chini kabisa, na kuhesabu maporomoko makubwa na miundo mbinu kama barabara, ukosefu wa umeme kutokana na tetemko kubwa sana lilitokea usiku wa manane kati ya Alhamisi na Ijumaa hii, katika kisiwa cha  Sulawesi, na zaidi kitovu ni katika wilaya ya Mamuju, ambapo kwa mujibu wa kile kilichotangazwa na televisheni mahalia , mkuu wa masuala ya zima moto wilayani, Darno Majid, amaethibitisha kuwa idadi kubwa imeorodheshwa ya waathiriwa. Kwa sasa maelfu ya mlundikano wa watu wako katika sehemu za hifadhi ya muda. Na vikosi vya uokoaji vinaendelea kupambana na muda kwa ajili ya kuwaokoa watu ambao wako chini ya vifusi, japokuwa operesheni hiyo ina vizingiti kwa sababu ya ukosefu wa zana nzito za kufanyia kazi hiyo.

Katika mji mkuu wa wilaya maporomoko zaidi ya Hoteli na ofisi za serikali, kuna hata Hospitali, mahali ambapo wanatafuta njia za kuwaokoa wagonjwa na wahudumu wa afya. Hata hivyo kwa mujibu wa wataalam wa mambo ya hali ya hewa na matetemeko wanabainisha kwamba inawezekana kuendelea na mitetemeko hiyo, kwa maana baadaye  mingine ilisikika hata katika mikoa mingine na kusababisha nyufa nyingi za nyumba lakini bila kuathirika hata mmoja. Kisiwa cha Indonesia ni kikubwa ambacho kina watu karibu milioni 260, lakiniambacho mara kwa mara kinakumbwa na tetemeko, volkeno na vimbunga katika bahari ya Pasifiki, kwa maana hiyo ni  sehemu yenye tabia ya nguvu kali za matetemeko. Mwaka 2018 tetemeko kali lilikumba eneo la  Palu, na daima katika kisiwa hicho cha Sulawesi na baadaye kimbunga kikali kilicho sababisha vifo vya watu 4,000.

 

 

16 January 2021, 19:10