Papa Francisko:Bwana anajua kuwa sisi tunahitaji kubarikiwa na tubariki wengine!

Wakati tunatarajia mwaka huu kuzaliwa kwa upya na matibabu mapya,tusipuuzie tiba,kwa sababupamoja na chanjo ya mwili,inahitajika chanjo ya moyo na ndio tiba.Utakuwa mwaka mzuri ikiwa tutatunza wengine na kama vile Mama yetu anavyofanya kwetu sisi.Ni katika mahubiri ya Papa aliyoandaa katika sherehe za Siku Kuu ya Maria Mama wa Mungu yaliyosomwa na Kardinali Pietro Parolin kwa niaba yake tarehe Mosi 2021.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika masomo ya liturujia ya siku yanaonekana maneno matatu ambayo yanapata ukamilifu wake  kwa  Mama wa Mungu ambayo ni kubariki, kuzaliwa na kukuta. Ndivyo anavyoanaanza Papa Francisko katika mahubiri yake aliyooandaa katika siku kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu sambamba na siku ya 54 ya amani duniani, ambapo mahubiri   yamesomwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican,  tarehe Mosi 2021 akiwa anaongoza Misa Takatifu Siku Kuu kwa  niaba ya Papa Francisko kutokana na  maumivu ya mguu na katika mahubiri hayo amejikita kufafanua maneno hayo matatu; kubariki, kuzaliwa na kukuta.  Akianza na neno kubariki anasema katika kitabu cha hesabu, Bwana  anawaomba kwamba wahudumu wabariki watu wao na kusema “Hivi ndivyo mtakavyo wabarikia wana wa Israeli na mtawambia “Bwana akubariki” (6,23-24).  Papa Francisko anabainisha kuwa huo siyo ushauri rahisi tu bali ni ombi sahihi.

Ni muhimu makuhani kubariki watu wa Mungu na hata waamini wabariki

Hata hivyo amebainisha kuwa ni muhimu hata kwa leo makuhani wanabariki watu wa Mungu wao bila kuchoka; hata wanamini  nao wawe wachukuzi wa baraka na kubariki. Bwana anajua kuwa sisi tunahitaji kubarikiwa. Kabla ya yote aliyofanya baada ya kuumba aliona kila kitu ni  vema na hivyo ni vizuri kusema kwa  wengine. Lakini kwa sasa na Mwana wa Mungu, hatupokei maneno tu ya baraka bali baraka yenyewe, kwa maana  Yesu ni baraka ya Baba. Katika Yeye anasema Mtakatifu Paulo, anatubariki kwa kila baraka (Ef 1,3).  Kila mara  tunapoufungua moyo kwa Yesu, baraka ya Mungu inaingia katika maisha yetu. Papa Francisko anashauri kumpokea Maria kwa sabau Yeye anatupeleka katika baraka ya Mungu na kwa njia yake tubabarikiwa, lakini kwanza ni kujifunza kubariki kwa sababu Mama ni yeye  anatufundisha kubariki na ambaye ni baraka tunayoipokea ili tuweze kuitoa. Hata sisi tunatakiwa kubariki na kusema vema kwa jina la Mungu; Ulimwengu umechafuka vibaya kwa kusema vibaya na kifikiria vibaya wengine, katika jamii na sisi wenyewe. Lakini kusengenya kunaharibu, hufanya kila kitu kiharibike, wakati baraka inarudisha na kutoa nguvu ya kuanza upya

 Kuzaliwa: Mwana wa Mungu alizaliwa na mwanamke 

Kuzaliwa ndiyo neno la pili ambalo Papa Francisko katika mahubiri haya yaiyosomwa, amelifafanua na kusema kuwa kile kinachosemwa na Biblia ni kwamba Mwana wa Mungu amezaliwa na mwanamke  kama watu, baada ya miezi tisa tumboni mwa mama, ambaye alijiachia kusukwa na ubinadamu. Ni tangu wakati huo ambapo Mama Maria anatuunganisha na Mungu kwa sababu katika Yeye Mungu alijishikamanisha na mwili wetu na hakuacha kamwe, ni yeye ambaye ni daraja kati yetu na Mungu. Kwa njia ya Maria tukakutana na Mungu kama Yeye anavyotaka, katika huruma, katika ukina wa ndani na katika mwili. Ndiyo kwa sababu Yesu siyo wazo lisilo shikika, ni la kweli alijifanya mwili na kuzaliwa na mwanamke na akakua katika uvumilivu. Wanawake wanajua uvumilivu huu wa subira: sisi wanaume mara nyingi hatujui na tunataka kitu mara moja; wanawake ni thabiti na wanajua jinsi ya kusuka nyuzi za maisha kwa uvumilivu. Je! Ni wanawake wangapi, mama wangapi kwa njia hii hufanya kuzaliwa maisha na kuzaliwa upya, wakitoa ulimwengu wa wakati ujao!

Pamoja na chanjo ya mwili inahitajika hata ya kiroho

Mafundisho ya Maria ni kwamba mtu yuko ulimwenguni kutoa uhai na sio kufa na kwamba hatua ya kwanza ya kutoa uhai kwa kile kinachotuzunguka ni kuupenda ndani mwetu. Uzuri unazaliwa katika moyo ambao lazima uwe safi, lazima kulinda maisha ya ndani, na sala. Moyo lazima uelimishwe kujali, yaani kuwajali watu na vitu, ni muhimu kutunza wengine, wa ulimwengu, kutunza kazi ya uumbaji,  kwani sio muhimu, anaelezea Papa Francisko, kujua watu na vitu ikiwa hatutunzani.  Mwaka huu, wakati tunatarajia kuzaliwa kwa upya na matibabu mapya, tusipuuzie tiba. Kwa sababu, pamoja na chanjo ya mwili, inahitajika chanjo ya moyo na  ndio tiba, Papa anasisitiza. Utakuwa mwaka mzuri ikiwa tutatunza wengine, na kama vile Mama yetu anavyofanya kwetu sisi. Kukutana:

Wachungaji walimkuta Maria, Yosefu na mtoto

Neno la tatu ambalo Papa amelifafanua ni kukuta. Wachungaji walimkuta Maria na Yosefu na mtoto katika familia rahisi, ambapo walimkuta Mungu ambaye ni mkuu katika udogo, nguvu katika huruma. Alikuwa malaika aliyewaita wachungaji, wakati ni neema inayowaita watu kumkuta Mungu ambaye amezaliwa na mwanamke na anarekebisha historia kwa upole, ambaye kwa msamaha wake hufanya kuzaliwa upya na ambaye faraja yake  inaangazia tumaini na ambaye uwepo wake unaleta furaha isiyo na kifani. Mungu huyu hakupotea kamwe, kwa sababu hapatikani mara moja tu; lazima apatikane kila siku.

Ili kupata nemma lazima kuwa hai

Kwa maana hiyo  haiwezekani kubaki tu,  na ili kupokea neema lazima mtu abaki akiwa hai. Mwanzo wa mwaka huu, shukrani kwa mafundisho ya Mama yetu, kwa maana hiyo anatuita kupata wakati wa kujikita kwa mtu. Wakati ni utajiri ambao sisi sote tunao, lakini tuna wivu nao, kwa sababu tunataka kuutumia kwa ajili yetu sisi wenyewe tu. Lazima tuombe neema ya kupata wakati kwa ajili ya  Mungu na kwa jirani yetu: kwa wale ambao wako peke yao, kwa wale wanaoteseka, kwa wale wanaohitaji kusikilizwa na kuwajali. Ikiwa tutapata wakati wa kutoa, tutashangaa na kufurahi, kama wachungaji. Mama yetu, aliyemleta Mungu kwa wakati, atusaidie kutoa wakati wetu.

01 January 2021, 16:13