Umakini wa Papa Francisko kila kona hata kwa wanajeshi

Katika siku kuu ya Bikira Maria Mkingwa dhambi ya Asili,Papa amesimama kuwasalimia wanajeshi ambao wanalinda usalama katika mji wa Vatican na kuwapatia zawadi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko amehitimisha Siku Kuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili, kwa namna ya pekee yaani  nje ya ratiba. Akiwa anarudi mjini Vatican mara baada ya kutoa heshima na kuweka  maua ya mawaridi katika sanamu ya Bikira Maria katika Uwanja wa Hispania, kutembelea Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu kusali mbele ya Picha ya Maria Salus populi Romani, na kuadhimisha misa, aidha kupitia  katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Papa amesimama kwa gari mbele ya moja ya kituo kimoja mahali ambamo wanasimama Wanajeshi wa Italia kikosi cha walinzi wa usalama wa Mji wa Vatican.

Papa Francisko ametelemka kutoka ndani ya gari na kuwasalimia mmoja mmoja wa wanajeshi hao. Baada ya kuwashukuru kwa huduma yao wanayotoa Papa amewapatia zawadi. Je ni hisia gani ambazo tunaweza kufikiria wamekuwa nazo hawa wanajeshi ambao labda hawakuwa wanasubiri ishara ya upendo wa nama hiyo kuwaka kwa Baba Mtakatifu na aliowaonesha na zaidi hata kuwapatia mkono wake hawa wanajeshi ambao uwajibika kwa masaa ishirini nane, yaani usiku na mchana, katika mvua, jua kali, upepo, baridi na hata theruji!

09 December 2020, 16:41