Tafuta

2020.09.16 Katekesi ya Papa katika Uwanja wa Mtakatifu Damas, Vatican. 2020.09.16 Katekesi ya Papa katika Uwanja wa Mtakatifu Damas, Vatican.  Tahariri

TAHARIRI:Katika mwaka wa kuwekwa karantini upo ukaribu wa Papa!

Katika mwaka 2020,bila ziara za kitume kimataifa na katekesi chache kwa uwepo wa waamini wachache,Papa Francisko amewasindikiza kwa njia ya sala katika Misa kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Marta waamini wote ulimwenguni.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mwaka 2020 wa Papa Francisko kama ilivyo kwa kila mmoja, amekumbwa na janga. Hapakuwapo na ziara yoyote kimataifa, na katekesi chache kwa uwepo wa watu wachache wakati wa kumalizika kwa  kiangazi na baadaye kuzuka kwa wimbi la pili la maambukizi.  Na maadhimisho ya liturujia kwa umma akiwa ilikuwa na ushiriki waamini wachache sana. Kile kilicho kosekana ni mawasiliano ya moja kwa moja kila siku na watu, yaani kwa kusalimiana na kupeana mikono, kubadilishana zawadi za vikofia na mikutaniko  ya mitazamo wakati wa mikutano.

Hata Papa Francisko katika  mtindo  wake ameweza  kujikita na  utume wake kwa njia ya kidigitali, akibaki nyumbani na kufanya kazi  zake huku akiwawasiliana kwa njia yamitandao na zaidi kupiga simu. Ndivyo anaandika Dk. Andrea Tornieli, Mhariri Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano katika Tahariri yake ya mtazamo wa huduma ya kichungaji ya Papa Francisko kwa mwaka 2020 unaomalizika. Katika Taariri hiyo Dk. Tornielli anaandikìka kuwa,  mwaka kwa upande wa Papa umekuwa na   Wosia wa  Querida Amazonia, ambao unasimulia mang’amuzi  ya Sinodi ya mwezi Oktoba 2019 ya Maaskofu  ambayo ilichapishwa katika mkesha wa kuzuka kwa janga  ikitolewa mwito wa nguvu wa kutazama kile ammbacho kinatokea  katika Kanda iliyosahulika. Kuna maelekezo ya njia za thati kwa ajili ya ekolojia ya kibinadamu ambayo itambue maskini, na kwa ajili ya kuthamanisa utumaduni  vilevile kwa ajili ya Kanisa la kimisionari lenye uso wa kiamazonia.

Baada ya kuona kuwa labda Covid -19 inaanza kupungua makali yake kidogo huko Italia, Papa alianza tena Katekesi zake  kwa kujikita katika kiini cha jinsi gani tunataka kujenga wakati ujao baada ya janga. Na hatimaye mwezi Oktoba Papa akatoa zawadi ya Waraka mwingine wa “Fratelli tutti”, yaani, “wote ni ndugu”, ambao unaelekeza udugu na urafiki wa kijamii kama jibu la vivuli vya chuki, vurugu na ubinafsi ambao utafikiri unashamiri katika ulimwengu ambao unajikuta na siyo tu virusi vya corona, lakini hata na vita, ukosefu wa haki, umaskini na mabadiliko ya tabianchi. Tukio ambalo halitasahulika kwa wote anaandikia Dk Tornielli  ni lile la tarehe 27 Machi, wakati Baba Mtakatifu anamwomba Mungu wa huruma aweze kuingilia kati na kuokoa binadamu aliyekumbwa na janga. Chini ya mvua katika uwanja wa Mtakatifu Petro, bila kuwa na watu, yaani uwanja ukiwa wazi lakini ambao ulikuwa unatazamwa na mamilioni ya watu kwa njia ya vyombo vya habari na mitando ya kijamii,  ili kusali kwa kuomba neema hii.

Dk. Tornielli aidha akiendelea na Taariri hii anasema, Papa alitelemka katika ngazi akichechemea na kulezea jinsi ambavyo sisi sote tuko katika mtumbwi mmoja na kwamba siyo rahisi kujikoa sisi wenyewe. Akibusu miguu ya msalaba wa Mtakatifu Marceli ambao una hisotria yake kutamaduni, kwani umekuwa  ukipelekwa katika maandamano wakati wa  matukio ya kizamani kama haya ya  majanga. Papa alibariki kwa Ekaristi Takatifu mji wa Roma na ulimwengu mzima wakati ikisikia milio ya honi za magari yaliyokuwa yanabeba watu mahututi kipindi cha karantini. Haiwezekani kusahau jambo moja muhimu ambalo lilisindikiza watu ulimwenguni kote hasa lile la maadhimisho ya Misa za Papa Francisko katika sehemu ya kwanza ya mwaka 2020. Katika kipindi hicho kilijaa hofu kubwa na mahangaiko. Misa zilikuwa za kila siku katika Kikanisa cha mtakatifu Marta kuanzia saa moja asubuhi; kwa miezi mitatu mfuasi wa mtume Petro alibisha hodi  kila siku katika nyumba zetu, alitualika si tu kusikiliza hotuba kuu au ndefu za katekesi lakini pia zaidi kusikiliza maneno ya Maandiko matakatifu, anasisitiza.

Yote hayo yalikuwa yalitukia katika kuhubiri  bila kuandika na mahubiri mafupi yakifuatia kuabudu Ekaristi  mara baada ya misa. Watu wengi waliweza kufuatilia, hata sehemu ambazo muda huo ulikuwa ni usiku wa manane lakini walifutilia kwa njia ya mitandao na televisheni. Kila kona ya dunia, iwe Ulaya, Asia, Amerika zote, Afrika, na Australia kila mmoja litafuta namna ya kuweza kumsikiliza na kusali na Papa. Ukaribu wa watu wa Mungu, na kuwasindikiza kumehitimishwa na na Misa za kushirikishana  skrini kila sehemu ya ulimwengu, na kuonesha kile ambacho ni muhimu  na kwa upande wa Papa kuwa mchungaji wa Kanisa la ulimwengu, mwombezi wa binadamu aliyejeruhiwa, shuhuda wa Injili ambayo ni kazi ya familia nzima ya binadamu na kwa mitindo mara nyingi  isiyotarajiwa na iliyofichika. Amehitimisha  taariri yake Dk, Tornielli katika kuonesha ukaribu wa Baba Mtakatifu kwa watu wake kwa njia ya sala na matendo mema.

29 December 2020, 11:36