Katika maadhimisho ya Sikukuu ya Familia Takatifu, Baba Mtakatifu amewakumbuka, amewaombea na kuwafariji wale wote waliokumbwa na kutikiswa na ugonjwa wa Corona, CIVID-19. Katika maadhimisho ya Sikukuu ya Familia Takatifu, Baba Mtakatifu amewakumbuka, amewaombea na kuwafariji wale wote waliokumbwa na kutikiswa na ugonjwa wa Corona, CIVID-19. 

Sikuu ya Familia Takatifu: Faraja kwa Waathirika wa COVID-19

Baba Mtakatifu amewakumbuka, amewaombea na kuwafariji wale wote ambao wamewapoteza ndugu, jamaa na marafiki zao kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa Virusi vya Corona, COVID-19. Amewapongeza wafanyakazi katika sekta ya afya, wanaendelea kujisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya huduma kwa wagonjwa na wale wote walioathirika kutokana na Virusi vya Corona.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana kutoka kwenye Maktaba ya Kitume, Sikukuu ya Familia Takatifu ya Yesu, Maria na Yosefu, amewashukuru waamini na watu wote wenye mapenzi mema, walioshiriki pamoja naye kwa njia ya vyombo vya mawasiliano na mitandao ya kijamii katika tafakari na hatimaye Sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili tarehe 27 Desemba 2020. Baba Mtakatifu amewakumbuka, amewaombea na kuwafariji wale wote ambao wamewapoteza ndugu, jamaa na marafiki zao kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona, COVID-19. Amewapongeza wafanyakazi katika sekta ya afya, wanaoendelea kujisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya huduma kwa wagonjwa na wale wote walioathirika kutokana na Virusi vya Corona, COVID-19. Jambo la msingi ni kuhakikisha kwamba, watu wanajitahidi kudhibiti maambukizi mapya ya Virusi vya Corona, COVID-19 kwa kutekeleza itifaki dhidi ya maambukizi mapya ya Virusi vya Corona, COVID-19.

Katika maadhimisho ya Sikukuu ya Familia Takatifu ya Yesu, Maria na Yosefu, Baba Mtakatifu amewakumbuka pia wale wote wanaoendelea kuathirika kutokana na vita, kinzani na mipasuko ya kijamii sehemu mbalimbali za dunia. Mtoto Yesu aliyezaliwa mjini Bethlehemu, awajalie wote hawa utulivu wa ndani na nguvu za kutembea huku wakiwa wameungana kwa ajili ya mafao ya wengi. Baba Mtakatifu amewahimiza wanandoa na familia kuhakikisha kwamba, wanajitahidi kumwilisha katika maisha yao, maneno makuu yafuatayo; Naomba, kielelezo cha heshima na nidhamu kwa wengine ndani ya familia. Asante  ni alama ya kushukuru katika familia; Samahani, wakati ambapo kuna mikwaruzo na mipasuko ya kifamilia. Wanafamilia wasithubutu kwenda kulala, kabla ya kupatana, ili waweze kuwa na amani na utulivu wa ndani.

Papa: Covid-19

 

27 December 2020, 15:28