Papa Francisko:tutazame Maria,tubadilishe maisha yetu kuwa zawadi!

Katika Siku kuu ya Bikira Maria wa Guadalupe,Papa Francisko ameongoza Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro ambapo katika mahubiri yake ameunganisha maneno matatu:wingi,baraka na zawadi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Leo ni siku ambayo Mama Kanisa anaadhimisha Siku kuu ya Bikira Maria wa Guadalupe, Msimamizi wa Bara la Amerika ya Kusini na ambaye kati ya tarehe 9 hadi 12 Desemba 1531 alitokea juu ya kilima cha Tepeyac, Kaskazini mwa Jiji la Mexico kwa mwanaume mmoja rahisi na wa asilia aliyeitwa Juan Diego na ambaye  alitangazwa kuwa Mtakatifu na Mtakatifu Yohane Paulo II, manmo 2002. Katika siku hii ambayo inakumbusha miaka 125 ya kivikwa taji kwa Mama Maria wa Guadalupe, Papa Francisko ameongoza Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Jumamosi tarehe 12 Desemba 2020 katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro Vatican, kwa ushiriki waamini wachache kufuatia na janga la sasa. Kwa kutazama sura ya Bikira Maria wakati wa mahubiri yake Papa amesema, tunaona uwazi wa wingi, baraka na zawadi katika historia ya maisha, kwa njia hiyo tafakari lake limezungukia maneno hayo matatu akitazama sura ya Mama yetu Maria.

Wingi

Katika kuanza kufafanua maneno hayo, Papa Francisko amesema kuwa Mungu daima anatoa kwa wingi na katika wingi. Yeye hatambui dozi, bali anatoa kwa wingi wake mkuu. Kasoro yake ni kutoa kwa ukarimu. Ni sisi ambao kwa asili na kwa ajili ya vikwazo vyetuna kwa ajili ya ulazima wa hesabu zetu hatujuhi kutoa kwa wingi, lakini Mungu anatoa kwa wingi na kabisa. Na mahali palipo na Mungu kuna wingi!

Baraka

Akiendelea na tafakari hiyo katika neno la pili amesema mkutano wa Maria na Elizabeth ulikuwa ni baraka. Kubariki maana yake ni kusema vema na Mungu tangu ukurasa wa kwanza wa Kitabu cha Mwanzo amezoea kuwa na mtindo wa kusema neno la vema. Kwa maana hiyo mtindo wa Mungu daima ndiyo wa kusema vema na kwa maana hiyo kulaani siyo mtindo wa wake, bali ni mtindo wa ibilisi, wa adui na ndiyo mtindo wa kutoa kwa kadiri, wa kutoweza kujitoa kabisa.  Mungu daima anasema vema na anaseka kwa haki, anasema hivyo akitoa kwa wingi na kusema vema huku akibariki.

Zawadi

Kwa kufafanua neono la tatu Papa Francisko amesema kuna zawadi ya Mungu ambayo inawakilishwa kama baraka. Hii ndiyo zawadi ambayo Mungu anayoiwakilisha na ambayo inataka kila wakati kuamsha kwa upya ule mchakato wa maonesho yake yote. “Aliye barikiwa yeye kuliko wanawake wote, alituletea baraka”. Kwa kutafakari picha ya Mama Yetu, Papa Francisko amesema kuwa “tumwombe Mungu kidogo atupatie ule mtindo wa Bwana kwa ajili ya kutoa kwa wingi, kusema vema, na siyo kulaani, na kubadilisha maisha kuwa zawadi.” Amehitimisha Papa Francisko.

12 December 2020, 18:09