Papa Francisko:vita visingekuwapo ikiwa pangekuwa na urafiki kijamii!

Papa Francisko ametuma ujumbe kwa njia ya video kwa ajili ya Siku ya 23 ya Uchungaji kijamii huko Buenos Aires,Argentina,unaoongozwa na mada “utamaduni wa kukutana.Papa anasema wazingatie umakini wa dhamiri ambazo zinasonga mazungumzo kama gurudumu linaloendelea kukanyaga na kuharibu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Waraka wa mwisho unaonesha bayana juu ya uthibitisho wa Papa uliotolewa kwa njia ya video kwa washiriki wa siku tatu ya mkutano ambao utakaomalizika tarehe 5 Desemba 2020 ulioandaliwa na Jimbo kuu la Buenos Aires,  nchini Argentina kwa ajili ya siku ya 23 ya kichungaji kijamii. Ni tukio ambalo mara nyingi kwa miaka iliyopita, ilikuwa imeonesha na Kardinali wa wakati ule  yaani Belgoglio ambaye ni  Papa mwenyewe na ambaye mwaka huu shukrani kwa Waraka wa 'Fratelli tutti', Papa kwa hakika anatoa fursa ya kuwa suala hili liko moyoni mwake. Papa Francisko katika ujumbe huo amesema tutazame ulimwengu kama ulivyo. Vita kila kona. Itikadi na tamaa na ulimwengu kumegeka vipande.

Katika hali mbaya zaidi papa amesema ni katika vita na hali inayokuja ya ubaguzi na mizigo mikubwa ya taabu. Kinyume chake, na suluhisho, ni kuwa na urafiki kijamii, thamani hiyo ambayo inatukumbusha kuwa wito wetu ni ule wa maelewano, wa udugu na wa kuwa ndugu". Papa Francisko aidha amesema “Tunaishi katika vita ya tatu ulimwenguni vilivyogawanyika vipande vipande. Hii siyo urafiki kijamii”. “Unaona nchi nyingi mahali ambapo hawazungumzi bali wanapiga kelele. Kabla ya kumaliza mwingine tayari anadakia wazo la mwingine, tunajibu bila kusikiliza mwingine".  "Siyo rahisi kufanya urafiki kijamii bila kusikiliza, bila kumsikiliza mwingine. Ili kusikiliza mwingine lazima kuamini kuwa mtu mwingine analo jambo jema la kuniambia".

Papa Francisko amebainisha kuwa badala yake, mara nyingi, barabara ya uelewa kwa pande zote imewekwa na kuta. Kwa kufafanua amesema kuta mbili labda ni  maadui wakuu wa urafiki wa kijamii, kwanza ni itikadi zinazoamuru kila kitu. Wao huwa na amri,na itikadi zinasimamia kupokonya msimamo wa asili ya mwanadamu. Adui wa pili ni tamaa. Shauku mara nyingi hujaribu kuondoa nyingine. Na kuzuia mwingine ili asiweze kuchukua nafasi yake.

Kuna viini vizuri vya urafiki kijamii ulimwenguni, Papa anakiri, lakini anabainisha kwamba kwa bahati mbaya pia kuna maeneo ambayo yana watoto wasio na shule, watu wasio na maji, kwa neno  moja tunaweza kusema ni ulimwengu usio na hadhi Ni jambo ambalo limemfanya Papa Francisko kutoa maswali ya kujiuliza: Je! kuna urafiki wa kijamii? Ikiwa kuna urafiki wa kweli kijamii hatupaswi kuwa na vita na wala hakuna haja ya aina yoyote, au elimu ambayo haifanyi kazi vizuri [...] Kutokana na matokeo hayo tutagundua ikiwa kutakuwa na urafiki kijamii. Lakini tusisahau maadui wawili wakubwa: Itikadi ambayo inataka kutawala na kuchukua uzoefu wa watu, na tamaa, ambazo kila wakati ni kama gurudumu,linaendelea na kuharibu  (...) Msifikirie na vichwa vyenu katika mawingu badala yeke ni kutafakari kwa msimamo wima miguu ikiwa chini na takwimu halisi.

04 December 2020, 17:04