2020.11. Katekesi ya Papa 2020.11. Katekesi ya Papa 

Papa Francisko:Mungu ni baba ni mama hachoki kamwe kubariki ulimwengu

Katika Katekesi yake Maktaba ya Jumba la Kitume,Papa amaeshauri kutolaani bali kubariki.Ikiwa wote wangekuwa wanafanya hivyo kwa uhakika pasingekuwapo na vita. Mungu anabariki lakini hata watu wanabariki na mapema wanagundua kuwa baraka ina nguvu maalum ambayo inasindikiza maisha yote kwa yule anayeipokea na kukubali katika moyo wa mtu abadilishwe na Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Katika tafakari ya Papa Francisko Jumatano tarehe 2 Desemba 2020 ya  Katekesi yake akiwa katika Maktaba ya kitume mjini Vatican,ambapo ni mwendelezo wa mada ya Sala, amesisitizia Baraka. Leo hii tunajikita juu ya ukuu wa Mungu unaohusu baraka. Katika mwendelezo wa tafakari kuhusu sala. Katika simulizi ya kazi ya uumbaji, kutoka Mwanzo (Mw 1-2), Mungu daima anaendelea kubariki maisha. Anabariki wanyama, (Mw.1,22), anabariki mwanamke na mwanaume (1,28) na hatimaye anabariki siku ya sababato, siku ya kupumzika na kufurahia kazi yake yote ya uumbaji (Mw 2,3). Ni Mungu anayetubariki. Katika sura za kwanza za Biblia kuna mwendelezo wa marudio  ya baraka. Mungu anabariki lakini hata watu wanabariki na mapema wanagundua kuwa baraka ina nguvu maalum ambayo inasindikiza maisha yote kwa yule anayeipokea na kukubali katika moyo wa mtu ajiachie kubadilishwa na Mungu (Vat. II, Sacrosanctum Concilium, 61). Papa Francisko akiendelea amesema kuwa mwanzo wa ulimwengu kuna Mungu ambaye anasema vizuri yaani anabariki. Yeye anaona kila kazi ya mikono yake ni njema na nzuri na anapofikia hatua ya mtu na uumbaji unakamilika na kutambua kuwa kila kitu alichokifanya kuwa ni Chema kabisa (Mw 1,31).

Kutoka hapo kidogo kidogo, uzuri ule ambao Mungu aliuweka katika kazi yake ukaanza kutelezwa na mwanadamu atageuka kuwa kiumbe kwa ujumla mwenye uwezo wa kueneza ulimwenguni mabaya na kifo; lakini hakuna lolote katu mbalo litaweza kufuta mhuri wa Mungu wa wema ambao aliuwekwa katika ulimwengu, katika asili ya kibinadamu, kwa sisi sote, uwezo wa kubariki na kufanya kubarikiwa. Mungu hakukosea katika uumbaji na wala kumuumba kiumbe binadamu. Matumaini ya ulimwengu yanakaa katika baraka ya Mungu kabisa. Yeye anaendelea kutakia mema, Yeye ni wa kwanza, kama asemavyo mshairi Péguy, kwamba “Anaendelea kutarajia wema wetu. Baraka kubwa ya Muungu ni Yesu Kristo, ni zawadi kubwa ya mwanaye”. Ni baraka kwa ubinadamu wote, ni baraka ambayo ilitukomboa sote. Yeye ni Neno la Milele ambalo kwalo Baba alitubariki wakati tulikuwa bado wadhambi (Rm 5,8), anasema Mtakatifu Paulo. Neno liliofanyika mwili na kutolewa kwa ajili yetu msalabani. Mtakatifu Paulo anatangaza kwa shauku kubwa ishara ya upendo wa Mungu na kusema “Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu; kwa watakatifu walioko wanaomwamini Kristo Yesu. Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo. Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake. Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa”. (Ef 1,3-6).

Papa Francisko amekazia kwamba hakuna dhambi ambayo inaweza kufuta kabisa sura ya Kristo aliyepo kwa kila mmoja wetu. Hakuna dhambi inaweza kufuta sura ambayo Mungu alitoa kwetu yaani sura ya Kristo. Unaweza kuisumbua lakini siyo kuindoa katika haruma ya Mungu. Mdhambi anaweza kubaki katika makosa yake kwa muda mrefu, lakini Mungu ni mwenye uvumilivu hadi mwisho akitarajia hatimaye kuwa moyo ule unafunguka na kubadilika. Mungu ni kama baba mwema na kama mama mwema, hata yeye ni kama mama mwema. Hachoki kamwe kupenda watoto wake hata kama wanakosea daima. Papa Francisko ametoa mfano wa kufikiria mara nyingi akiona watu wengi wakiwa katika foleni, yaani mama wengi wakitaka kuingia magerezani kuwaona watoto wao wafungwa. Hawachoki kamwe kupenda watoto haon a watambua watu wengi wanaopita wakiwa ndani ya basi huku waktoa hoja zao kwamba hawa hawaoni aibu…lakini wao wanakwenda mbele. Mfano huo ndiyo wa Mungu kwa kuwa sisi ni muhimu hata kama sisi ni wadhambi. Kwa maana yeye ni baba, ni mama na upendo safi. Yeye alitubariki milele na hachoko kamwe kutubariki.

Uzoefu mzuri na wa nguvu ni ule wa kusoma maandiko haya ya baraka inayotlewa hata katika magereza au katika jumuiya yoyote ya kusaidia watu waweze kuondokana na mabaya. Ni uzoefu mzuri wa kusikiliza mtu ambaye amebarikiwa licha ya kuwa na makosa makubwa ambayo Baba wa Mbinguni anaendelea kuwatakia mema na kutumani kuwa hatimaye watajifungulia wema. Na ikiwa wale ndugu wa karibu sana wamewaachaa, kwa maana wapo  wengi ambao wanawaacha kwa kuwa siyo kama wale mama ambao wanajipanga foleni ili kuwaona watoto wao ambao wanahukumiwa hawawezi kurudia hali halisi;  lakini kwa Mungu daima ni watoto. Mungu hawezi kufuta sura yake iliyomo  katika mwanaye, yaani kwa kila mmoja wetu. Mara nyingi inaonekana miujiza ya wanaume na wanawake ambao wanazaliwa upya. Kwa sababu wapoka  ile baraka inayowazesha  kurudia  kuwa wana. Kwa sababu neema ya Mungu inabadilisha maisha, inatuchukulia jinsi tulivo lakini haituachi kamwe jinsi tulivyo.

Papa Francisko akitoa mfano mwingine amesema tufikirie kile alichofanya Yesu na Zakayo (Lk 19,1-10). Wote walikuwa wanamtazama vibaya; Kinyume chake Yesu akaweza kuonesha wema, na tangu hapo hamu ya kutamani kumwona Yesu, ikamfikia huruma inayokomboa. Kwa maana hiyo ilimbadilisha kwanza moyo na baadaye maisha ya Zakayo. Katika maisha ya wale watu wadhaifu na waliokataliwa Yesu alikuwa anawaona kama baraka ya Baba. Kwa mfano yule waliyemuona kama mtoza ushuru na kufanya mambo mabaya lakini Yesu alikuwa anaona ishara kubwa ya baraka ya Baba na huruma yake. Sentesi yake inayorudiwa kila wakati kwamba “aliona huruma” inapelekea kumsaidia na kumbadilisha moyo. Na zaidi, yeye alifikia kujidhirisha kuwa ni yeye mtu mwenye kuhitaji (Mt 25,31-46).  Katika neno hilo ambalo ni Protokali ya mwisho ambayo sisi sote tutahukumiwa ni Matayo 25, ambapo Yesu anasema “nilikuwa hapo, mwenye njaa, uchi, mfungwa, hospitalini, ni mimi nilikuwa hapo. Kutoka kwa Mungu anayebariki, hata sisi tujibu kwa kubariki, Mungu alitufundisha kubariki na tunatakiwa kubariki. Ndiyo sala ya sifa, ya kuabudu, na kushukuru.

Katika katekesimu ya Kanisa katoliki imeandikwa “sala ya baraka ni jibu la binadamu kwa zawadi ya Mungu, kwa kuwa Mungu anabariki, moyo wa mtu unaweza kujibu kwa kubariki Yesu ambaye ni kisima cha kila baraka”(n. 2626). Sala ni furaha na shukrani. Mungu hakusubiri kwamba tuongoke ili kuanza kupendana, bali alifanya hayo kabla tulipokuwa bado wadhambi. Hatuwezi kubariki Mungu tu anayetubariki, lakini tubariki yote katika Yeye, watu wote, kubariki Mungu na kubariki ndugu, kubariki ulimwengu na ndiyo mzizi wa upole wa kikristo, uwezo wa kuhisi kubarikiwa na uwezo wa kubariki. Kama sisi sote tungekuwa tunafanya hivyo kwa hakika pasingekuwapo vita. Dunia hii inahitaji baraka na sisi tunaweza kutoa baraka na kupokea baraka. Baba anatupenda. Kwa upande wetu inabaki furaha tu ya kumbariki na furaha ya kumshukuru na kujifunza kutoka kwake na siyo kulaani bali kubariki. Na hapa kuna neno kwa watu ambao wamezoea kulaani, watu ambao kila wakati wana neno baya, laana mdomoni mwao, hata mioyoni mwao. Kila mmoja wetu anaweza kufikiria: je! Nina tabia hii ya kulaani hivi? Na kumwomba Bwana neema ya kubadilisha tabia hii kwa sababu tuna moyo uliobarikiwa na kutoka katika moyo uliobarikiwa, hivyo laana haiwezi kutoka. Bwana atufundishe kamwe kutolaani, bali kubariki.

02 December 2020, 14:53